Asilimia 90 ya watanzania tumeshagundua kwamba hawa viongozi wamehongwa kwa ajili ya bandari

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,293
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Ndugu zangu,,, hapa nchini kwetu ukiwa mtu makini, mwenyekujitambua, mwenye uwezo wa kudhibiti mihemko, mwenye mawazo na akili iliyohuru bila kukontroliwa na mtu mungine ambae ataitumia akili yako kwa faida yake na familia yake huku akikuacha wewe ukidhalilika, ukiwa mwenye kutafakari kwa kina juu ya mstakabali wa nchi na future za wananchi, hakika utaweza kuona madudu mengi yaliojificha nyuma ya migongo ya viongozi wenye njaa. Kuona huko kunaweza kufanikiwa kupitia historia zao, maneno yao, na vitendo vyao.

Fikiria kiongozi mkubwa wa chama cha siasa anafika Kariakoo, badala ya kuwaeleza watu sera za chama chake, badala ya kuwaeleza watu namna watakavyofaidika, au taifa litakavyosonga mbele kimaendeleo na huduma bora kwa wananchi kutokana na sera hizo endapo chama chake au chao kitafanikiwa kushika dola.

Yeye anakuja na upepo wa bandari kwa kuwaeleza watu maneno mawili matatu ya kuuponda mkataba wa bandari bila kuonesha sehemu anayodai kuwa haifai, baada ya hapo anaanza kuomba michango na baadae akishachangiwa chake anatokomea anapokujua yeye kununua nyama, mchele, mafuta na mahitaji mengine ya lazima huku waliomchangia wengi wao wakienda kula dagaa na ugali usiku ule.

Sasa mtu mwenye akili unajiuliza kama mtu ana njaa hadi anaamua kuwakamua wale anaodai kwamba anawasaidia, je atashindwa kupokea hongo atakayohongwa na kundi lenye lengo la kumtumia kupush ajenda zao mbele.

Kama anachukua hadi elfu ya masikini muuza pilipili wa Kariakoo atawezaje kukataa milioni 1 au 2 ya wale wapitisha madawa ya kulevya bandarini, wezi wa vifaa vya magari na mizigo mbali mbali bandarini, wakwepa kodi na ushuru wa bandarini?

Jibu utapata kwamba jamaa amehongwa ili awapambanie waliomuhonga, na hizo za Kariakoo anazitumia kununua mahitaji yake ya siku. Ndio maana tunasema hawa viongozi wanapambana kwa sababu ya njaa zao na wakishapata chao wanatokomea kula na familia zao. Mnaosubiri kupata maendeleo kupitia viongozi hawa, hamna tofauti na mtu anaesubiri nazi ianguke kutoka juu ya mkungu.
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Ndugu zangu,,, hapa nchini kwetu ukiwa mtu makini, mwenyekujitambua, mwenye uwezo wa kudhibiti mihemko, mwenye mawazo na akili iliyohuru bila kukontroliwa na mtu mungine ambae ataitumia akili yako kwa faida yake na familia yake huku akikuacha wewe ukidhalilika, ukiwa mwenye kutafakari kwa kina juu ya mstakabali wa nchi na future za wananchi, hakika utaweza kuona madudu mengi yaliojificha nyuma ya migongo ya viongozi wenye njaa. Kuona huko kunaweza kufanikiwa kupitia historia zao, maneno yao, na vitendo vyao.
Nog een keer, a u.b?
 
Nini ushauri wako sasa?,tuufate
 
Punguza jazba jibu hoja s wacha polojo ming zisizo na maana
Uyo ni mwanasiasa ulitaka aseme nn na km anaongea pumba mbona mlimpiga risasi
Km hao wanasiasa wanaongea vtu visivyo eleweka mbona mjomba wako jiwe aliwaibia kula zao uchaguzi wa 2020
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Ndugu zangu,,, hapa nchini kwetu ukiwa mtu makini, mwenyekujitambua, mwenye uwezo wa kudhibiti mihemko, mwenye mawazo na akili iliyohuru bila kukontroliwa na mtu mungine ambae ataitumia akili yako kwa faida yake na familia yake huku akikuacha wewe ukidhalilika, ukiwa mwenye kutafakari kwa kina juu ya mstakabali wa nchi na future za wananchi, hakika utaweza kuona madudu mengi yaliojificha nyuma ya migongo ya viongozi wenye njaa. Kuona huko kunaweza kufanikiwa kupitia historia zao, maneno yao, na vitendo vyao.
Kwani wewe ndio msemaji wa watanzania?
 
Badala ya kuendelea kuota, bora ungeamka na kuanza kutafakari ni kazi au biashara gani nyingine ya halali ufanye ili ujiingizie kipato cha halali baada ya ile uliyozoea bandarini ya kuiba vifaa vya magari ya watu bandarini na kwenda kuviuza mitaani kufa.
Mafisadi mnamangamanga, mmezoea kuuza nchi kwa mikataba mibovu safari hii tunagawana mbao mmetuchosha, migodi, ngorongoro, kia, Richmond, bandari nk sasa basi, kama mbwai na iwe mbwai majizi wakubwa nyie.
 
Viongozi wa ccm na hela wala sio geni!
Rushwa na ccm sawa na; damu na mwili, pipa na mfuniko, uji na mgonjwa, sindano na uzi,ngariba na kisu!
Mkuu wenzako wanaongea propaganda hizi kwa lengo la kupata michango mbali mbali huko Kariakoo, pia kupewa hela na wezi wa bandarini ili kuendelea kusomesha watoto wao walioko belgiji, Marekani na Kanada, huku wewe chawa wao ukitumika kueneza propaganda zao bila kupewa chochote.

Ni aibu na inasikitisha sana, ila ndo hivyo siku zote wajinga ndio waliwao.
 
Back
Top Bottom