Asilimia 88 za Lissu zimsaidie Magufuli kujitafakari

kwani magufuli aligombea haya mambo gani ya ajabu kweli mnayaleta....hivi pale kumbe alishindanishwa magufuli na lissu???wale ni wanasheria wamemchagua rais wao wa sheria anayewafaa.
 
'I believe our ties are much stronger than any passing disagreement or misunderstanding,or stances or finger pointing et al this is why I just read and quit.I'll opine at an appointed time,not now!
You are right. My optimism was a reflection from 88% win. I too,remain silent but with much trust to to TLS presda elect.
 
Yaani Lissu kachaguliwa kuongoza chama cha kufa na kuzikana cha mawakili unataka Magufuli ajitafakari nini?acha kumlinganisha Rais wetu na wanaharakati wapuuzi
Hiki kweli chama cha kufa na kuzikana maana ni sheria pekee inayoweza kukulazimu kufa/kunyongwa endapo other causes of death are not ready. Pia sheria inaweza kuamuru uzikwe au usizikwe mpaka wanasheria wakubali au hata ikikaidiwa sheria yaweza kuamuru ufukuliwe. Mkuu umefikiria mbali kuhusu kufa na kuzikana!
 
Tuachane na tafiti za kupikwa za Twaweza, kuchaguliwa kwa Lissu kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika kwa ushindi wa 88% ni statement kubwa sana kwamba jamii ya Watanzania walioelimika wanamwelewa Lissu na vyama vya Upinzani kuliko wanavyomwelewa Magufuli, CCM na Polisi Wake...

Hiyo maana yake ni kuwa Magufuli hakubaliki miongoni mwa Wasomi na hata miongoni mwa watumishi wa Umma kwa sababu katika uchaguzi huo wa TLS mawakili na wanasheria wa serikali pia waliwakilishwa kwa wingi wa kutosha tu na kura zao wamempa Lissu...

Kwa hali hii, kiongozi mwungwana angetumia uchaguzi huu kama fursa ya kujitathmini na kujirekebisha na kuwa na nia ya kuendesha nchi kwa haki!
sioni busara hizo kwa magufuli anaamini ktk mabavu na si uwezo wa kufikiri.
 
hapo sasa ndo utaskiaa matamkoo yanavyoanza kupungua sasa maana alikuwa akilala akiamka anakuja na jipya sasa saizi watanyokaaaaa sasa
 
Kwa sisi tunaomjua Tundu Lissu, wanasheria mmeula wa suya. Tusubiri inshallah Mwenyezi Mungu atupe uzima. Ni muda tu utatupatia matokeo ya uongozi wa Lissu kwa TLS. Lissu, Mrema, Mtikila (RIP) ni kapu moja. Hawa na wanaharakati na wabinafsi; hakuna kiongozi hata mmoja hapo.
 
Ushindi wa Lisu hakika ni wa kufurahisha sana hasa kwa watanzania wasio na itikadi Kali ya Mlengo wowote wa Kisiasa.Najuwa kwa watu wa chama chake furaha walionayo haina kifani. Hongera kwake raisi Mteule wa TLS.
 
Kama Lissu angekuwa mpuuzi kama unavyodai basi mkuu wako wa kaya asingekosa usingizi kwa ajili yake
Mkuu..Jamaa wanaomkatakamata wanajua fika kuwa wanampandisha umaarufu ndani ya upinzani. Amini usiamini wanajua hilo. Sasa Jiulize kwanini wanataka awe maarufu ndani ya upinzani? Kama hauna kifua usitafute jibu la hilo swali maana linaweza kuwa si zuri kwako.
 
Yaani Lissu kachaguliwa kuongoza chama cha kufa na kuzikana cha mawakili unataka Magufuli ajitafakari nini?acha kumlinganisha Rais wetu na wanaharakati wapuuzi
Tatizo la kuota ndevu ukiwa mtoto mchanga ndio hilo limekufanya uwe na mawazo mgando sio Kosa lako ni Kosa la waliokuleta duniani, shame on you
 
MAJUKUMU YA TANGANYIKA LAW SOCIETY
KUANZISHWA
Tanganyika Law Society ilianzishwa kwa sheria ya Bunge No.30 ya mwaka 1954. Kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha sheria, chama hiki kina hadhi ya shirika(corporate status) hivyo kinaweza kushtaki na kushtakiwa, kumiliki mal ink kama taasisi nyingine zenye hadhi ya kisheria (legal entity).

MALENGO YA KUANZISHWA KWAKE.
Kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria ya TLS sura ya 307 malengo ya kuanzishwa TLS ni:
(a) Kulinda na kukuza viwango vya taaluma ya sheria na mwenendo wa wanasheria nchini Tanzania;
(b) Kuwezesha upatikanaji wa maarifa ya kisheria kwa wanachama wake na watu wengine;
(c) Kuisaidia serikali na mahakama katika mambo yote yanayohusu sheria, utawala wa sheria na utekelezaji wa sheria;
(d) Kulinda na kuusaidia umma wa watanzania yanayohusu au kuendana au kutokana na sheria;
(e) Kumiliki mali na kuziendeleza kwa faida ya kutimiza malengo yake kwa mujibu wa sheria;
(f) Kuchangisha au kukopa fedha kwaajili ya uendeshaji wa shughuli zake;
(g) Kujihusisha na uwekezaji wa fedha au rasimali nyingine kama TLS itakavyoona inafaa;
(h) Kufanya kitu kingine chochote kila kinachoendana au kuwezesha kutekeleza malengo yake.

UANACHAMA
Kwa mujibu wa kifungu cha 7 kinachoanzisha sheria hiyo, mtu yeyote aliyesajiliwa kuwa wakili anakuwa mwanachama wa TLS moja kwa moja bila kujaza fomu. Hata hivyo kifungu cha 8 kinaruhusu watu wengine kama Mwanasheria mkuu wa serikali, mwandishi wa sheria za serikali, wanasheria wa serikali na watu wengine wenye sifa za uwakili, kuomba kuwa wanachama wa TLS na watakuwa wanachama iwapo watakuwa wametimiza masharti ya kuwa wanachama.

UONGOZI
TLS inaongoizwa na Rais, Makamu wa Rais, Mhazini na wajumbe wengine saba. Hawa ndio wanaunda Baraza kuu(Governing Council). Viongozi wa Governing Council huchaguliwa kila mwaka. Hivyo ndio kusema U-rais wa TLS ni wa mwaka 1 tu. Chini ya Chombo Hiki kuna Sekretarieti ambayo huongoza shughuli z akila siku za chama. Hawa ni waajiriwa kabisa. Wanachama wengine wote hukutana kwenye Mkutano mkuu unaoitwa Annual General Meeting.
TLS pia kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha sheria yake, kupitia Baraza lake, imepewa uwezo wa kutunga kanuni mbalimbali za kujiendesha. Hii ni pamoja na kanuni za uchaguzi, kanuni za uanachama, nk.
Nadhani hii itakuwa imekusaidia kidogo kuielewa TLS.
 
Wamempa umaarufu wao wenyewe, kwa kumogopa kupita kiasi. Na 2020 ashauriwe kugombe urais, maana ataendelea kupata umaarufu mkubwa.
 
Subiri kikao cha bunge mwezi ujao unaletwa muswada wa kuunda chombo kipya.Tundu Lissu ataongoza TLS kwa mwezi mmoja tu,baadae kinakuwa chama cha kukopa na kuweka
lakini hilo halitaondoa ukweli kwamba wantanzania wasomi hawalizishwi na mwenendo wa mkuu wa nchi
 
Yaani Lissu kachaguliwa kuongoza chama cha kufa na kuzikana cha mawakili unataka Magufuli ajitafakari nini?acha kumlinganisha Rais wetu na wanaharakati wapuuzi
Ukikutana na Mwakyembe muulize kwa nini alikuwa anataka kuhakikisha rungu lake linafanya kazi kwenye hiki chama 'cha kufa na kuzikana' cha mawakili
 
Back
Top Bottom