Asilimia 88 za Lissu zimsaidie Magufuli kujitafakari

Ki Mun

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
3,443
4,386
Tuachane na tafiti za kupikwa za Twaweza, kuchaguliwa kwa Lissu kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika kwa ushindi wa 88% ni statement kubwa sana kwamba jamii ya Watanzania walioelimika wanamwelewa Lissu na vyama vya Upinzani kuliko wanavyomwelewa Magufuli, CCM na Polisi Wake...

Hiyo maana yake ni kuwa Magufuli hakubaliki miongoni mwa Wasomi na hata miongoni mwa watumishi wa Umma kwa sababu katika uchaguzi huo wa TLS mawakili na wanasheria wa serikali pia waliwakilishwa kwa wingi wa kutosha tu na kura zao wamempa Lissu...

Kwa hali hii, kiongozi mwungwana angetumia uchaguzi huu kama fursa ya kujitathmini na kujirekebisha na kuwa na nia ya kuendesha nchi kwa haki!
 
Tuachane na tafiti za kupikwa za Twaweza, kuchaguliwa kwa Lissu kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika kwa ushindi wa 88% ni statement kubwa sana kwamba jamii ya Watanzania walioelimika wanamwelewa Lissu na vyama vya Upinzani kuliko wanavyomwelewa Magufuli, CCM na Polisi Wake...

...hiyo maana yake ni kuwa Magufuli hakubaliki miongoni mwa Wasomi na hata miongoni mwa watumishi wa Umma kwa sababu katika uchaguzi huo wa TLS mawakili na wanasheria wa serikali pia waliwakilishwa kwa wingi wa kutosha tu na kura zao wamempa Lissu...

SUre kama ana hekima lakini!! Vitu ambavyo ni adimu kwake!!
 
Polisi wanajielewa, hata Lisu alipotoka sero aliwashukuru kwa kuwa na utu!
 
Daaaaaah safi sana

Ushindi muruwa kabisa! Wingi wa mawakili wameonyesha imani kubwa waliyo nayo kwa mtoto wetu huyu, msomi wetu, raia wetu mwenye usongo na nchi yake, sio kwa sababu yuko upinzani ila kwa utu anaoishi nao. Amepigania haki sio kwa kuwa amekuwa Chadema bali hata kabla kabisa! Tundu Lisu, umeamua kuteswa, kudhulumiwa na kutukanwa na watawala kwa ajili ya watawaliwa. Sikupi hongera ila pole! Sitashangilia bali nitatafakari majukumu mazito uliyojiongezea! Sitakunywa wiski nisije nikasinzia nikakuacha wewe mwenyewe ukihangaika. Umepewa fimbo itumie vyema. Uwe mwangalifu zaidi, watesi wako wameumia na watafuta njia mbalimbali ili ushindwe kuitumia hio fimbo. Tupo pamoja ingawaje hatujui mbele wala nyuma, utusaidie tuweze kujua tukae upande gani ili haki isisiginwe tena. Wewe ni jemadari wetu!
 
Yaani Lissu kachaguliwa kuongoza chama cha kufa na kuzikana cha mawakili unataka Magufuli ajitafakari nini?acha kumlinganisha Rais wetu na wanaharakati wapuuzi
 
Back
Top Bottom