Uyole CTE
Member
- Apr 17, 2015
- 7
- 12
Historia ya mkoa wa Mbeya imegawanyika katika vipindi tofauti tofauti kabla ya uhuru na baada ya uhuru, Mji wa Mbeya ulianzishwa na wakoloni waingereza mnamo mwaka 1927, Wakati huo dhahabu ilianza kupatikana sana katika milima iliyopo karibu na Mbeya hadi Chunya hivyo Mbeya ulikuwa ni mji wa mapumziko kwa Wazungu kutokana na hali yake nzuri ya hewa.
katika kipindi cha ukoloni ulifahamika kama "Southern highland provience" kwa kujumuisha baadhi ya maeneo ya mikoa ya Iringa na Rukwa na baadaye Mbeya. Asili ya neno Mbeya imekuwa na nadharia kadha wa kadha ambazo zinaelezwa na wataalam na wazee mbalimbali, Baadhi ya nadharia hizo ni pamoja na:-
1. Ibheya - Chumvi
Nadharia hii inaeleza kuwa asili ya Neno Mbeya ni neno la kisafwa "Ibheya" lenye maana ya chumvi, Hii inatokana wafanyabiashara kufika katika mji huu na kubadirishana mazao yao kwa chumvi iliyokuwa ikipatikana kwa wingi kipindi hicho. Ikapeleka wenyeji kuita eneo hili Ibheya kama sehemu ya kubadilishia chumvi na mazao, kutokana na sababu za kimatamshi ikapelekea wageni kuzoea kutamka na kuandika Ibheya.
2. Agamba mbeye - Kamlima Mbeye
Nadharia hii inaeleza kuwa jina Mbeya limetokana na Mlima uliopo nyuma ya Chuo cha Kilimo Uyole (Agricultural Research Institute -ARI- Uyole) uliojulikana kwa jina la kisafwa kama Agamba Mbeye (kamlima Mbeye kwa kiswahili) Ambao hivi sasa ni maarufu sana kwa jina la Mlima ugari, ni mlima ambao una muonekano wa mviringo, sehemu za chini umeota nyasi japo si nyingi sana kama ilivyo sehemu ya juu ambayo haioti nyasi kabisa, hivyo ikawa sehemu nzuri ya kupumzikia wageni ili kupata hewa nzuri na muonekano mzuri wa mji, kutokana na changamoto za kimataishi ikapelekea wageni kuliendeleza sana jina la eneo kama Mbeya kimaandishi na kimatamshi.