Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Kwa nilivyosikia mimi neno shikamoo maana yake ni "niko chini ya miguu yako.

Pia nimesikia hilo neno ni la kitumwa na lilikuwa linatumiwa na watumwa kuwaonyesha heshima wakuu wao.

Kuna baadhi ya watu nawajua hawapendi kupewa shikamoo na hata wakipewa hawajibu marahaba.

Je kama hili neno ni la kitumwa, kwanini sisi tuendelee kulitumia kama neno linaloashiria heshima?

Kama lilitumika kuwakandamiza mababu zetu kwanini na sisi tulipe nafasi? Au tunalitumia kama wenzetu Wamarekani weusi wanavyo tumia neno "nigga" ambalo lilitumika kudharau mababu zao na kulifanya la kwetu sasa?





 
Hapo umechukua uhalisia wa neno, lakini katika kiswahili neno hili linatumika kama salamu, tazama mfano mwingine:

mambo: haina maana ya salamu lakini watu wanatumia kama salamu.

upo hapo?
 
MwanaFalsafa1,

Kwa asili neno hilo kweli lilimaanisha hicho ulichosema. Lakini ujue lugha inazaliwa, inakua na kubadilika kadiri jamii inavyobadilika kufuatana na wakati. Kumbe katika lugha nyingi - si Kiswahili tu - misamiati imenyumbuka, kubadilika na hata kuwa na maana tofauti na ile ya mwanzo. Ndiyo maana kuna kitu kinaitwa etymology ya neno au msamiati.

Kwa hiyo neno "shikamoo" lenye asili ya Kiarabu lilimaanisha kujidunisha chini ya bwana. Lakini kadiri muda ulivopita, na hasa neno lilivoingia katika lugha ya Kiswahili, lilibadilika maana yake badala ya ile kitumwa likamaanisha Heshima ya mdogo kwa mkubwa wake. Kumbe likawa na maana chanya badala ya ile hasi.

Kumbe wanaokataa kupokea "shikamoo" hawajui tu. Waelimishwe wajue kwamba kwa leo tena kwa Kiswahili lina maana nzuri tu japo kiasili likuwa na maana hasi ya kudhalilisha.
 
Last edited by a moderator:
Ndio maana linatumika kumsalimia mtu aliyekuzidi umri, kwa ajili ya heshima uliyonayo kwake.......
 
Ndio maana mtoto hawezi kumsalimia mtoto mwenzake "Shikamoo" au watu wenye umri unaolingana hawasalimiani shikamoo.....
SALAMU YA SHIKAMOO NI KWA AJILI YA KUMSALIMIA MTU ALIYEKUZIDI UMRI TUU.............
 
Nafikiri matumizi yake kwa sasa ni tofauti na zamani. Kama ndiyo hivyo hata maana yake pia itakuwa imebadirika na kuchukuliwa kama linavyotumika kwa sasa yaani salamu za mdogo kwenda kwa mkubwa.
 
MwanaFalsafa1,

Kila kitu ulichoandika hapo juu umepatia. Ni neno la kitumwa kweli lakini ndio hivyo mababu zetu kwa kupenda umwinyi wakaliendeleza tu. Mara nyingi mimi huwa nalikuwepa neno hilo kwa kutumia "asalam aleykum".
 
Last edited by a moderator:
Sawa ni salamu ya mdogo kwa mkubwa lakini inakuwaje pale inapotokea unashindwa kukadiria kwa haraka umri wa unayemsalimia na umri wako? Unapompa mtu shikamoo kumbe ulitakiwa wewe kupewa hiyo shikamoo, hapa huwa haileti picha nzuri kwakweli
 
Sawa ni salamu ya mdogo kwa mkubwa lakini inakuwaje pale inapotokea unashindwa kukadiria kwa haraka umri wa unayemsalimia na umri wako? Unapompa mtu shikamoo kumbe ulitakiwa wewe kupewa hiyo shikamoo, hapa huwa haileti picha nzuri kwakweli
Nawapa shikamoo walionizidi miaka mitano au zaidi. Sio rahisi nikaenda fyongo
 
kila kitu ulichoandika hapo juu umepatia.ni neno la kitumwa kweli lakini ndio hivyo mababu zetu kwa kupenda umwinyi wakaliendeleza tu.mara nyingi mimi huwa nalikuwepa neno hilo kwa kutumia "asalam aleykum" .

Mzee Wenger vipi bwana? hata hiyo pia siyo asilia tumekopi mahali!
Labda ungekuwa unasema "habari za saa hizi, za leo, za siku nk"

Au uwe unasalimia kilugha, huwa hakina ukubwa au udogo;
Solowenyo.......inajibiwa solowenyo
Mihanyenye ....... Misaha
Wabonaki........Nabonakantu
Ulmphola...........
Nazinginezo... zinasidia sana kuikwepa shikamoo, upo?
 
Ndio maana linatumika kumsalimia mtu aliyekuzidi umri, kwa ajili ya heshima uliyonayo kwake.......

Hili neno hata mimi huwa linanipa maswali nikifikiria historia. Kwani TUK (Taasis ya Uchunguzi wa Kiswahili) katika tafiti zao mbalimbali hawajaweza kupata neno lingine kutoka makabila yaliyopo Tanzania kama mbadala wake?

Kwenye kabila langu kwa mfano, hakuna neno linalofanana na shikamoo! Zipo salamu za kila wakati zenye kuonyesha heshima kwa waliokuzidi umri. Naamini hata makabila mengine wanayo.

Ila inavyoonekana SHIKAMOO IS HERE TO STAY!
 
Mimi huwa inanikera kumsalimia shiakamoo mtu ninayemzidi umri at. kwa sababu ni shemeji yako Mkubwa yaani dada mkubwa wa mke au mama mdogo wa mke amabye labda unamzidi miaka 10. mambo ya uswahilini utakuta wanaidai kabisa. Kwangu shikamoo siyo salaam mbaya kwa anayekuzidi umri zaidi ya miaka 5
 
Bado ukweli uko palepale kwamba hili neno lilikuwepo kukandamizwa watumwa(haswa sisi weusi), iweje tulichukue na kulifanya letu?

Kama WoS alivyo sema kwani hamna neno mbadala? Iweje kumuambia mtu nipo chini ya miguu yako iwe heshima? Kwani lazima tuige kila kitu? Au sasa ni sisi tunaendeleza utumwa wa kimawazo bila pingu na kengele?

Nawashukuru wachangiaji wote hata wale ambao tuna mawazo tofauti.
 
Last edited:
Ni kweli shikamoo lina asili ya utumwa, lakini kama walivyotanabaisha wachangiaji wengine lugha hukua na sehemu moja wapo ya ukuaji wa lugha ni kama haya mabadiliko tunayoyaona kwenye neno shikamoo.

Na sio neno hili pekee ambalo limekuwa "adopted" katika kiswahili kwa maana nzuri tu japo mwanzo yalikuwa na asili fulani ya uduni hivi, mfano neno 'rabeka' ni neno ambalo lilitumika na mwanamke kumuitikia mume wake, na lina asili ya kiarabu pia, na kwa jinsi ilivyokuwa wanawake kwa waarabu walikuwa hawathamini sana, lakini sasa linatumika kama heshima ya mwanamke kumuitikia mumewe hasa katika ukanda wa pwani, neno jingine ni ' naam' ni neno lilikuwa linatumika kukubali kitu au jambo, lakini kwa sasa kwenye kiswahili linatumika kama kiitikio cha heshima kwa mtoto wa kiume aitwapo.

Yapo maneno mengi tu kama mem sahib, sasa linatumika kama mamsapu nk
 
Ok inajulikana kuwa shikamoo ni salaam unayompa mtu aliyekujizi umri (sifahamu kama kuna age limit) Ila Kuna wababa wengine especially binti wa kike akimwambia shikamoo humjibu "salama tuu binti hujambo".And why is that?.
 
Ok inajulikana kuwa shikamoo ni salaam unayompa mtu aliyekujizi umri (sifahamu kama kuna age limit) Ila Kuna wababa wengine especially binti wa kike akimwambia shikamoo humjibu "salama tuu binti hujambo".And why is that?.

SF,
Hii inatokana na kwamba - unapotanguliza shikamoo ni kama umeweka kizuizi cha heshima.Anapokataa kuitika inavyotakiwa ni kwamba alikuwa ana mpango mwingine na wewe na anashangaa barrier ya nini tena?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…