MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
Kwa nilivyosikia mimi neno shikamoo maana yake ni "niko chini ya miguu yako.
Pia nimesikia hilo neno ni la kitumwa na lilikuwa linatumiwa na watumwa kuwaonyesha heshima wakuu wao.
Kuna baadhi ya watu nawajua hawapendi kupewa shikamoo na hata wakipewa hawajibu marahaba.
Je kama hili neno ni la kitumwa, kwanini sisi tuendelee kulitumia kama neno linaloashiria heshima?
Kama lilitumika kuwakandamiza mababu zetu kwanini na sisi tulipe nafasi? Au tunalitumia kama wenzetu Wamarekani weusi wanavyo tumia neno "nigga" ambalo lilitumika kudharau mababu zao na kulifanya la kwetu sasa?
Pia nimesikia hilo neno ni la kitumwa na lilikuwa linatumiwa na watumwa kuwaonyesha heshima wakuu wao.
Kuna baadhi ya watu nawajua hawapendi kupewa shikamoo na hata wakipewa hawajibu marahaba.
Je kama hili neno ni la kitumwa, kwanini sisi tuendelee kulitumia kama neno linaloashiria heshima?
Kama lilitumika kuwakandamiza mababu zetu kwanini na sisi tulipe nafasi? Au tunalitumia kama wenzetu Wamarekani weusi wanavyo tumia neno "nigga" ambalo lilitumika kudharau mababu zao na kulifanya la kwetu sasa?
Nianze na kuuliza , nini maana ya neno "shikamoo"?
Kuna sehemu nimeona na kusikia kuwa maana yake ni "nipo chini ya miguu yako". Salamu ambayo watumwa walikuwa wanawasalimia mabwana zao (kama maana niliyotoa si sahihi naomba msaada wenu kurekebisha hapo).
Asa swali langu ni dogo tu, Je mpaka sasa bado kuna utumwa hapa Tanzania?!
Ni kutuko maana mpaka mtu mzima mwenye akili zake bila hata aibu anallilia "shikamoo" alaf baada ya hapo anajisifu kuwa eti 'Tanzania hakuna utumwa'
Hivi hili baraza la Kiswahili wanafanya kazi gani sasa?
Nimejaribu kuchunguza kidogo na kubaini kuwa salamu ni kujuliana hali au kutakiana heri! mfano, kwa Kingereza wanasalimia "Good morning" wakimmaniasha asubuhi njema "Good evening" wakimaanisha jiono njema n.k, kwa Kihaya kuna "Ma' Olailoota" mama umalalaje/umeamkaje (kama sijakosea) najua kuwa kuna salamu za makabila mangine mengi tu wakijuliana hali na kutakiana heri. Lakini Kiswahili chetu kinashangaza, eti shikamoo!
Kwa mimi napendelea zaidi "habari za saa hizi", "za saa hizi" au hata "mambo" inatosha sana kulliko hata shikamoo. Ila kutana na kibabu fulani kiambie "za saa hizi" utasikia "mtoto anajifanya amekua huyu eenh!!"
mimi naishia hapo kwa leo.
Nawasilisha Hoja!!
Wadau, labda ni vyema kushare nanyi suryey ambayo tuliifanya muda kidogo, nayo ni kuhusu salam ya 'Shikamoo'.
Katika suryey yetu tukagundua kuwa;
1. Watu wengi hawajui maana ya neno 'Shikamoo' zaidi ya kusema kuwa ni heshima, wengine wakasema ina maana ya 'nipo chini ya miguu yako'
2. Asili yake ni ya kitumwa,yaani walioinzisha hawaitumii kama salamu yao ya kawaida ila walioipokea ndio wanaitumia katika matumizi yao ya kila siku.
3. Ime simama katika kuangalia umri, kitu ambacho muda mwingine ni ngumu kujua au kukisia umri wa mtu sababu waweza muamkia mtu kumbe ni mdogo wako
4. Imejengwa katika nidhamu ya uoga, ndio maana ni rahisi kumkuta mtu mkubwa kiumri ana msalimu mtu mdogo kiumri sababu tu anayeamkiwa ana nguvu kubwa kifedha au kimadaraka.
5. Imepitwa na wakati, yaani wengine hawataki kabisa kuisikia ama wanajishusha umri, ndio maana mtu anaamkiwa anasema poa, au salama.
6.Imesababisha ugomvi au wengine kutosalimiana kwa sababu tu hakuna anayependa kuwa mdogo.
Wadau toeni mapendekezo yenu juu ya kile mliona na mnavyodhani juu ya suala hili...
Wachangiaji mbalimbali waliandika
"Ni kweli shikamoo lina asili ya utumwa..".
Je kuna mtu mwenye uhakika?
Kuna utafiti wa kihistoria?
Jibu "marahaba" ni umbo la salamu ya kawaida ya Kiarabu huko wanasalimiana "marhaba" na jibu ni "marhabteen" (=marhaba mara mbili).
Jinsi ilivyo "Shikamoo" ni moja kati ya salamu katika tamaduni mbalimbali zinazotambua tofauti ya cheo.
* Zamani watu wa Ulaya walipiga magoti mbele mkubwa wakimsalimu;
* watu wa Uajemi walijulikana kwa desturi ya kujitupa chini kabisa ardhini mbele ya mkubwa;
* katika sehemu ya Asia ya kusini watu husalimiana kwa kufunga mikono yote miwili (karibu kama wakatoliki wakisali) na kama ni mkubwa wanashika mikono juu ya kichwa kama ni cheo sawa mbele ya uso na kama ni mdogo chini ya kichwa kifuani.
Tamaduni zilizobadilika sana watu waliacha mara nyingi aina hizi za kusalimia angalia Marekani ambako watu hupeana tu sauti kama "hai" (Hi!) isiyo na maana ndani yake.
Ni juu ya watu kuamua. Binafsi sioni ubaya kumpa mzee maskini heshima ya kifalme kwa kumsalimia kwa "shikamoo".
Nakumbuka watoto wangu walipofika Kenya mara ya kwanza waliwasalimu watu wazima kwa "shikamoo" kote tulikoenda madukani n.k. Walilalamika saaana ya kwamba hawa Wakenya hawakujibu! Ni kweli- nje ya Mombasa hawajui kabisa.
Maana ya shikamoo ni hii ambayo inatumika sasa na Waswahili, hiyo uliyoitoa haipo katika kamusi tunazotumia. Inawezekana ilikuwa inatumika zamani wakati wa utumwa, lakini lugha hubadilika, maneno hubadilika na halikadhalika maana za maneno nazo sio tuli.
Tanzania hakuna utumwa, huu ni mfumo wa maisha na hauwezi kuamuliwa na uwepo wa neno moja tu katika lugha nzima. Kung'amua uwepo wa utumwa ni lazima tuchunguze mifumo ya maisha ya Watanzania na sio kutazama neno moja kisha kuhitimisha.
Watu wazima huwa 'wanalilia' hiyo shikamoo kwa kuwa ndio utaratibu wa jamii kuwa salamu hii itatoka kwa mdogo kwenda kwa mkubwa. Kama ambavyo tu mtu huyu huyu mzima anavyolilia kupishwa siti kwenye daladala wakati haijaandikwa popote.
Baraza la Kiswahili la Taifa hutunga sera ya Lugha pamoja na kuishauri Serikali masuala mbalimbali yanayohusu lugha. Kiswahili hakishangazi, bali kina namna yake ya pekee ya kutazama salamu (Salamu kama kujuliana hali, na salamu kama ishara ya heshima). Wanaofahamu lugha ya kibantu yenye dhana hii pia wanaweza kuja kutufahamisha. Ukishangaa ya Kiswahili inabidi ushangae pia na Kifaransa ambapo majina yake huwa na jinsia (eti kuna gari la kike na la kiume... Inachekesha eeh?)
Kupendelea kutumia aina fulani ya salamu ni haki yako, lakini isije kukugharimu ukweni siku moja (natania tu).
Hoja yako umeiwasilisha vema, karibu sana.