Asili ya jina MWANZA ni wapi?

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,681
1,698
Wakuu, sasa hivi naangalia mechi ya CAF champions league kati ya timu za ZESCO na Mbabane Swallows mjini Ndola, Zambia. Mara kaingia mchezaji wa ZESCO kipindi cha pili akiitwa Mwanza J.. Ikaniijia kichwani hapa kwetu tuna mji/mkoa tunaouita Mwanza na pana majina ya " SiMwanza " nikaona nitupie hapa JF kwa magwiji wa historia watatiririka kujua asili ya jina hili ni wapi?
 
Sidhani kama upo sahihi. Nyanza ni Nyanza tu na Mwanza ni Mwanza tu. Nimekupa majina ya watu hasa kusini mwa nchi yetu.
Hilo jina halina mahusiano na jamii zilizopo Zambia,ni majina tu yanaingiliana,
 
Inasemeka kulikuwa mganga maarufu wa kike alikuwa akiitwa ng'wanang'wanza aliishi maeneo ya kemondo hapo mjini kati sijui kama niko sahihi wengine tumehamia tu tukitokea congo
 
Inasemeka kulikuwa mganga maarufu wa kike alikuwa akiitwa ng'wanang'wanza aliishi maeneo ya kemondo hapo mjini kati sijui kama niko sahihi wengine tumehamia tu tukitokea congo
Sasa ikawaje usiitwe Ng'wanza ?
 
Mwanza inatokana na jina la Ng'wanzalima,mfugaji alieishi nera/machemba hivo basi kutokana na tabia ya qasukuma ya kufupisha majina walikuwa wakimwita ''ng'wanza" kwani usukumani kama we ni YOHANA wanakuita YOHA,MOHAMED utaitwa MOHA au MED kwa kuwa kulkuwa na mwalo kamanga wa kuvukia na mwalo nera wa kuoga na kunyweshea mifugo wakoloni walipofika wakaamua kuweka makao maeneo ya kwa Ng'wanza[lima] ikaanzia hapo kuitwa Ngw'anza ila kutokana na wajerumani kushindwa kuitamka na kuiandika Ng'wanza wakawa wanatamka 'mwanza' ambayo ipo hadi leo,pia kwa kuongezea tu wasukuma hawaiti mwanza bali huita NG'WANZA labda wakiwa wanazungumza kiswahili ndo hutumia jina mwanza
 
Back
Top Bottom