Yericko Nyerere, standtruth, kasimba g, et al,
Nimeonelea nirudi kujadili baadhi ya hoja zenu muhimu zinazosisitiza juu ya mapungufu ya hoja yangu katika bandiko namba moja; lakini kabla ya yote, nadhani nimeeleweka kwenye bandiko namba moja nilikuwa nina nia gani kwani hili niliweka wazi kabisa, hasa kuhimiza kwamba lengo langu sio kujadili upande upi upo sahihi bali kutoa a historical account juu ya domestic forces mbalimbali ambazo zilitengeneza mazingira ya militarization of party politics, kisha to set a stage for a discussion juu ya wapi tuende, hasa baada ya kuelewa juu ya tatizo la kuwa external oriented katika kujadili suala husika - yani kuepuka kujadili kwa kuangalia jinsi gani vyombo husika vili emerge nchi za wenzetu badala ya kuangalia jinsi gani hilo lilitokea nyumbani; ni kwa mantiki hii nikajadili pia kwamba chama cha kupigania uhuru (TANU) kimeacha a movement legacy ambayo imekuja kuwa emulated na chadema nyakati hizi kutokana na ukweli kwamba pamoja na malengo yake mazuri, TANU haikuweza kumaliza kazi yake to empower wananchi - economically, socially and politically; ni katika muktadha huu, naomba nisisitize tena historia ni kama inajirudia kwani wananchi walio wengi wanalilia for the "second independence", huku chadema sasa wakiwa katika position ya TANU, huku to a certain extent, CCM ikiwa katika position ya mkoloni, hence the deepening hostility between ccm and chadema inayopelekea kukua kwa tatizo la national insecurity and instability kutokana na a serious gap in the functioning of the national security system ambayo it is increasingly becoming deprofessionalized and politicized; Swali linalofuatia ni je:
Solution ni nini, chadema waendelee na uamuzi wao au ccm ibadilike?
Hili ni swali la msingi lakini nitakuwa mwongo kama nitasema nina majibu; sana sana nina maoni yangu ambayo nitaendelea kuyatoa kwa jinsi mjadala huu utakavyoendelea;
That said and done, naomba nijadili kidogo juu ya historia ya mfumo wa kisiasa Tanzania; ingawa inawezekana baadhi yenu msione relevance yake na mjadala husika, nina amnini itasaidia angalau wachache kwa matumizi ya 'terms of reference' hata huko mbeleni; Sehemu kubwa wa yafuatayo ni elimu niliyopata kwa kujisomea makala na vitabu mbalimbali kuhusiana na historia ya nchi yetu, kwa mfano kazi za Dr. Max Muya, wa idara ya siasa UDSM na wengine wengi;
Tanganyika ilikuwa nchi ya vyama vingi wakati wa uhuru 1961; Taifa lilirithi katiba ya mfumo wa vyama vingi;vilikuwepo vyama vikuu vinne:
1) TANU
2) UTP (cha serikali ya mkoloni)
3) ANC (Zuberi Mtemvu)
4) AMNUT
Baada ya uhuru, vyama vingine vitatu vya siasa vilisajiliwa baada ya uhuru (kati ya 1962 na 1963):
1)People Convention Party (PCP)
2)African Independence Movement (AIM)
3)Peoples Democratic Party
Kwa vile mjadala huu unaegemea zaidi siasa za Tanzania bara, sitajadili vyama vya siasa vilivyokuwepo zanzibar zaidi ya kuvitaja (ASP, ZNP, ZPPP na UMMA); Pia nadhani sina haja ya kujadili kwanini taifa likaamua kufuata mfumo wa chama kimoja kwani sababu hizi zipo in the open, lakini kwa wale wasioelewa hili ni kama ifuatavyo kwa kifupi:
Kwanza - ilionekana kwamba, vyama vya TANU na ASP ndio vyama halali vya umma - yani vilikuwa ndivyo vyombo halali na vya uhakika vilivyounganisha nguvu ya umma na taifa - yani vyama vya wafanyakazi, wakulima, ushirika na vikundi vingine vya kiraia katika mapambano dhidi ya ukoloni na usultani ili kuleta uhuru; Pili, iliaminiwa kwamba mara tu baada ya uhuru, uongozi mpya wa wazalendo ulikabiliwa na tishio la mgawanyiko wa taifa katika misingi ya ukabila, udini, rangi na majimbo; ili kuondokana na hatari hii, ikaonekana ni muhimu kitovu cha madaraka nchini kuwa chini ya "chama" badala ya "bunge";
Ili kukamilisha lengo hili, mikakati na mbinu mbalimbali ya "kisheria" na "kisiasa" ilitumiwa kukiwezesha chama (TANU baadae CCM) kudhibiti utawala wa nchi;TANU ilikuja na mbinu kuu sita kufanikisha lengo husika:
1) Kudhibiti vyama vya wafanyakazi
2)Kudhibiti wakulima, wafugaji na vyama vyao (ushirika)
3) Dola
4)Utumishi Serikalini
5)Vyombo vya habari
6)Vyombo vya ulinzi na usalama
Ningependa kujikita katika eneo relevant na mjadala huu yani eneo namba sita hapo juu:
Madaraka ya TANU (later CCM) katika kudhibiti utawala wa nchi yalikuwa strengthened zaidi kwa kuunganishwa kwa vyombo vya dola, hasa majeshi ya ulinzi na usalama; hii ilienda hand in hand na kueneza mafunzo na nidhamu ya kijeshi; hatua ya kuunganisha chama na vyombo vya usalama zilianza 1964 baada ya a mutiny attempt;kufuatia this attempt, jeshi likavunjwa;
MUHIMU:
Wakati wa kuliunda upya jeshi, uandikishaji wa wanajeshi wapya ulitegemea uanachama wa TANU au Umoja wa Vijana (TYL); vigezo hivi vilitumika kwa ajili ya ajira katika vyombo vingine vya ulinzi wa raia - polisi, magereza na UWT; kufuatia hatua hii, watendaji wote katika vyombo hivi walipatiwa mafunzo ya itikadi ya chama kupitia mpango wa "elimu ya siasa"; kazi hii ilisimamiwa na makamisaa wa chama; ili kutumiza malengo yake ya kudhibiti utawala wa nchi, TANU ilifanya mabadiliko kadhaa katika katiba yake;kwa mujibu wa mabadiliko hayo, majeshi ya ulinzi na usalama yalifanywa kuwa MKOA wa chama Kiuongozi;Kwa hali hiyo, majeshi hayo yakaingizwa katika muundo wa chama kitaifa; hii ni sehemu ya sababu kwanini katika kipindi hicho hicho, sekretarieti ya chama ngazi ya taifa kwa mara ya kwanza ikaunda "Tume ya ulinzi na usalama"; Tume hii iliundwa kwa madhubuti kabisa on merit ya wajumbe wake - viongozi wakuu wa chama na serikali ya TANU na maafisa wa ngazi za juu katika vyombo vya ulinzi na usalama walikuwa ni among members wa tume hii;
Ni rahisi kuona kwamba chini ya muundo huu, chana kiliweza kudhibiti vilivyo vyombo nyeti vya dola na kwa njia hiyo, cgama kiliweza kutawala na pia kurekebisha na kusimamia nidhamu katika sekta nyingine za jamii easily;
Pia kuingiza vyombo vya ulinzi na usalama katika siasa kulifuatiwa na uteuzi wa wanajeshi kushika vyeo vya kisiasa; wanajeshi walipewa ruksa kugombea nafasi za kisiasa katika chama na vyombo vya dola;
MUHIMU:
Vile vile, jamii kwa ujumla wake iliingizwa katika mfumo wa kijeshi na kwa hali hii, ikawa rahisi kuthibiti taifa kwa amri (badala ya majadiliano) kama ilivyo suala la nidhamu ndani ya vyombo vya usalama; ilipofika mwaka 1971, mpango kabambe wa kuimarisha ulinzi wa umma ukaanzishwa;kwa mfano, kila mtu mzima raia wa Tanzania alitakiwa kuhudhuria mafunzo ya mgambo yaliyoendeshwa na maafifa wa JWTZ; pamoja na malengo ambayo pengine yalikuwa mazuri, athari ya hatua hii ikawa ni pamoja na ujenzi wa jamii ya raia wanaopokea amri kutoka juu bila ya kushiriki katika majadiliano;katika kuimarisha mtindo huu, maafisa wa chama walipatiwa mafunzo katika shule za kijeshi/intelligence na baadae walitakiwa kuripoti katika ofisi za chama;
Kwa kuhitimisha, kuna umuhimu wa kutambua historia ya nchi yetu inatueleza nini kuhusiana na mbinu na mikakati iliyotumiwa na ccm enzi ya mfumo wa chama kimoja, kuthibiti na kuendesha taifa, hasa suala zima la vyombo vya ulinzi na usalama; Ni imani yangu kwamba tukichanganya hoja zangu za bandiko namba moja pamoja na hoja za bandiko hili, tutakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuelewa kwa kina suala zima la militarization of party politics chini ya mfumo wa chama kimoja, madhara yake chini ya mfumo wa vyama vingi, na nini kifanyike kulinusuru taifa na machafuko;
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums