Asili Ya Green Guard Ya CCM na Changamoto Kwa CHADEMA

Asili Ya Green Guard Ya CCM na Changamoto Kwa CHADEMA

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Posts
4,850
Reaction score
9,436
Uamuzi wa Chadema kuanzisha ulinzi wake binafsi kama chama cha siasa umepokewa kwa hisia tofauti miongoni mwa jamii ya watanzania; Suala hili limezua two major schools of thought; Upande wa kwanza napenda kuuita the Mwigulu Nchemba’s school of thought kutokana na ukweli kwamba yeye ndiye kiongozi wa juu zaidi katika CCM aliyetoa maoni yake juu ya uamuzi huu wa Chadema; Kwa kundi hili, hoja ya msingi ni kwamba uamuzi huu wa Chadema ni kinyume cha Katiba ya nchi, lakini muhimu zaidi ni kwamba kitendo hiki sio tu kina historia ya ugaidi bali pia kinajenga mazingira ya fujo, ugaidi na nchi kutotawalika, among other things; Upande wa pili wa hoja napenda niuite Edwin Mtei’s School of thought kutokana na ukweli kwamba kama muasisi wa Chadema, Mzee Mtei ametoa msimamo wake rasmi kuunga mkono uamuzi wa Chadema kuunda ulinzi wake kamili kama taasisi; Kwa kundi hili, hoja ya msingi ya ni kwamba udhaifu wa serikali chini ya CCM umepelekea kuibuka kwa serious gap katika suala la ulinzi wa umma; Ni katika mazingira haya ambayo yanatawaliwa na de-professionalization and politicization of the country’s security system, Chadema wamebaini kwamba, wao kama chama pamoja na wafuasi wao hawawezi tena kuwa salama katika ushindani wa siasa ndani ya demokrasia yetu bila ya kwanza kujiundia mfumo wa ulinzi na salama wao binafsi kama taasisi;

Katika mjadala wangu wa leo, nia yangu sio kujadili ni upande upi upo sahihi na upande pi haupo sahihi, badala yake its just an attempt kujadili asili ya militarization of politics katika muktadha wa nchi yetu, hasa kwa kurejea kidogo kwenye historia ya nchi yetu; Nimechukua uamuzi huu baada ya kuona serious gaps katika mjadala unaoendelea hivi sasa ambao kwa bahati mbaya upo zaidi outward looking kuliko inward looking; Kwa maana nyingine, mjadala uliopo una ‘import’ experiences za nje ya nchi kuhusiana na suala husika badala ya kuangalia experience ya ndani ya nchi yetu ya Tanzania ambazo zipo wazi kwa wale wanaojali kutumia muda wao kuelewa historia yetu kama taifa; Kama tutakavyobaini, suala husika has always and will always remain to be the “Youth Question”;

TANU ilizaliwa July 7, 1954 as a reorganization ya TAA, mchakato ambao uliongozwa na young “ACTION GROUP”; Vijana hawa walikuwa western educated & exposed na walikuwa wana lead comfortable urban lives; Kazi ya awali ya kundi hili la vijana hawa wa kizazi kipya ilikuwa ni kutoa ahadi kwa wananchi (weusi) kwamba TANU itasimimia vyema masuala yote muhimu kwa manufaa ya wengi (tofauti na mkoloni), hasa Political, Social and Economic Empowerment; Kwa mfano, kwa kuanzia, TANU ilifuata nyayo za makundi kama vile “The Wazaramo Union” by appealing to African racial sentiments against wafanyabiashara wa kiasia (wahindi) na kuahidi kwamba wata short circuit hawa middle men (wahindi) kwa kuanzisha maduka na vyama vya ushirika ambavyo ni African based n.k;

Wananchi wengi walianza kujawa na matumaini juu ya malengo na ahadi hizi za TANU: Pamoja na mafanikio haya ya TANU, changamoto kuu mbili zikaanza kujitokeza kuelekea miaka ya mwisho ya 1950s: Kwanza ilikuwa ni suala la je – ni kwa kiasi gani TANU ingefanikisha welfare kwa umma na pia kujijengea uhalali wa Kisiasa (political legitimacy) ndani ya Tanganyika? Na pili ambayo ni muhimu zaidi kwa mjadala wetu wa leo ni je – role ya Vijana katika chama (TANU) ingekuwa nini, ndani ya chama ambacho kilikuwa katika mapambano ya ndani kwa ndani kuhusiana na generational conflicts (wazee na vijana) kuhusiana na nafasi za uongozi katika chama na jamii kwa ujumla? Kufuatia changamoto hii, muda sio mrefu, TANU ikagundua kwamba ili ifanikiwe, strategy muhimu ilikuwa sio nyingine bali udhibiti wa fujo/civil disorder ambayo ilikuwa imminent kutokana na ukubwa wa matumaini ya wananchi (hasa vijana) juu ya matunda ya uhuru per TANU’s promises wakati wa harakati za uhuru; Ni katika reorientation hii ya kiitikadi i.e. transformation kutokea ahadi ya maisha bora kwa wananchi to prevention of fujo ya umma (vijana), taratibu TANU nationalists wakajikuta wakianza kuwa na “a shared concern” na Serikali ya mkoloni, kwani kwa Mwalimu na washauri wake, ikaanza kuwa obvious kwamba ikulu ya TANU faced changamoto kubwa kwani isingeweza kufanya mastaajabu yoyote ya maana kwa wananchi per ahadi za TANU in the 1950s;

Kufuatia hali hii, kuanzia miaka ya mwisho ya 1950s, mikutano ya hadhara ya TANU kwa ujumla ikaanza kuwa ya Amani na Utulivu ingawa kuna nyakati kulitokea vurugu kidogo hasa pale baadhi ya viongozi wa TANU walipokuwa wanaichingea serikali ya mkoloni kwa wananchi na kupelekea umma kuhamasika kutaka mabadiliko ya haraka; Muda sio mrefu, serikali ya mkoloni ikaanza kuhofia kwamba kitendo cha viongozi wa TANU kuichongea serikali kwa wananchi kungepelekea umma kubeba the same rhetoric kwa kasi kubwa na kulazimisha mapinduzi nchini; Hivyo, serikali ya mkoloni ikaja na sheria iliyohimiza TANU ‘to make obedience to law and order’ kama sehemu muhimu ya siasa zake za majukwaani; Pamoja na mivutano hii, for TANU’s interest, TANU ikaanza to adopt into colonial government’s commitment ya: kuletea wananchi maendeleo pamoja sambamba na prevention of public disorder, hasa pale TANU ilipoanza kukamata State Power kuelekea uhuru wa Tanganyika;

Hii ilikuwa ni a major ideological transformation kwa upande wa TANU i.e. from itikadi ya kukomboa wananchi dhidi ya utawala dhalimu wa kikoloni by any means necessary na kuwapatia wananchi matunda ya uhuru, to an ideology ya kuletea maendeleo wananchi sambamba na maintenance of civil order; Katika muktadha huu, pia vijana wakaanza kupata ‘a new social category’ (tofauti na awali) ambapo sasa wakaaza kuwa young bureaucrats na wenye authority (at times kuliko wazee), kwani tofauti na miaka ya nyuma ambapo wazee ndio walikuwa na prominence katika jamii, TANU ilifanikishwa kuwapatia vijana umuhimu katika jamii kufuatia nafasi zao za kazi za umma;

Kuna suala muhimu ambalo lilijotokeza katika kipindi hiki that’s worth mentioning: muda mchache kabla ya uhuru, TANU ilikuja na uamuzi kwamba – civil order was to rest on the party discipline, not state control, na suala hili lika trickle down kutokea kwenye kamati za juu za chama (TANU) kwenda kwenye matawi mbalimbali katika Tanganyika based on gender and generation; Ikumbukwe pia kwamba wazo la kuunda jumuiya ya Vijana na Umoja wa Wanawake ndani ya TANU ililetwa na young activists mwaka 1954, wazo ambalo lilitekelezwa miaka miaka miwili baadae (1956) ambapo TANU YOUTH LEAGUE (TYL, baadae UVCCM) ilizaliwa kama jumuiya ya kwanza ya chama cha TANU chini ya Joseph Nyerere; Lengo kuu la kuundwa kwa TYL ilikuwa ni kusaidia TANU katika suala zima la kudumisha NIDHAMU, UTULIVU, na kudhibiti FUJO, hasa miongoni mwa vijana nchini Tanganyika, hasa wale ambao hawakufanikiwa kuendelea na elimu, hivyo kuwa jeshi la the uneducated and unemployed youths mitaani; Hivyo TYL ilikuwa na jukumu kubwa la kukabiliana na kundi hili kwa niaba ya TANU;

Huko vijijini, TANU Youth League ilichukua traditional roles, kwa mfano, kwa Mwanza, TYL took over shughuli za Basumba (Young Men) ambao walikuwa na jukumu la ku discharge communal labour/tasks katika ngazi za vijiji, recruiting wanachama wapya wa TANU, kukusanya kodi, deal with self – help projects vijijini n.k; Mkoani Dar-es-salaam, TANU ilivutia sana vijana ambao walikuwa ni underemployed & unemployed, kundi ambalo lilianza kuleta upinzani kwa serikali na middle class; Itambulike kwamba - kwa vijana ambao hawakuwa na elimu ya kutosha ya kupata ajira katika bureaucratic structures za nchi, uanachama wa TANU Youth League ulikuwa ni fursa pekee, pia tiketi kwa vijana kujipatia immediate wages/salaries katika nafasi mbalimbali za chama na pia daraja la kupata promotion na ajira za mishahara serikalini baadae;

Role ya Vijana kuelekea kipindi cha uhuru ilizidi kuongezeka kwa kasi kubwa both as a social category lakini pia kundi muhimu la political actors; Kwa mfano, mwaka 1958 ulifanyika mkutano mkuu wa TANU Tabora katika kipindi ambacho Mwalimu Nyerere alikuwa katika deep negotiations na serikali ya mkoloni kuhusiana na suala la uchaguzi mkuu; Awali, Wanachama wengi wa TANU walipinga pendekezo la serikali ya mkoloni ya kuwa na ‘a tri-racial election system’, and in anticipation, TANU ika organize a national civil disobedience campaign to be enforced na TANU Youth League (TYL); Kazi hii ilikuwa itekelezwa chini ya uongozi wa mdogo wa Mwalimu Nyerere – Joseph Butiku kama mwenyekiti wa TYL; Mkakati huu ulisitishwa baadae baada ya serikali ya mkoloni kufikia makubaliano na Nyerere kushirikia katika uchaguzi mkuu; Hali hii ikazaa dissenters ndani ya TYL ambao hawakuunga mkono makubaliano ya Nyerere na serikali ya mkoloni, hivyo wakaamua kuunda a new movement by the name of African National Congress (TANU) chini ya Rais wao Mzee Zuberi Mtemvu;

Pamoja na yote haya, TANU haikurudi nyuma bali maintained its original mission – to enforce party discipline in public areas and to attack formal opposition to TANU; Kuna wakati Katibu Mwenezi wa ANC mwaka 1961 alitoa malalamiko kwamba TANU Youth League ilikuwa ikijichukulia mamlaka na pia sheria mikononi na inakamata wananchi wanaounga mkono ANC, tried and convicted them; vile vile publicity secretary wa ANC alilalamika kwamba TYL have drilled like solders na silaha na kuvamia majumbani mwa watu, ejected wenye nyumba, pia wamekuwa wakisimamisha magari barabarani na kuyapekua n.k (chanzo cha taarifa hii ni “Omido to Kahama, 21 July 1961, TNA 540/20/69); Pia rejea press release ya Omido, 12 August 1960, TNA 561/17/21; Vile vile, kwa mujibu wa Rais wa ANC – Zuberi Mtemvu, poor performance ya chama chake ilitokana na vitisho vya TYL ambayo ilikuwa inakamata wananchi waliokuwa wanaunga mkono ANC, inawachapa viboko na kuwatia ndani bila ya authority from TANU’s government;

Pia mujibu wa mwanazuoni mmoja – Thomas Burgess (2001) anaelezea phenomenon hii kama ifuatavyo:
“The advent of TANU in urban areas like Dar-es-salaam offered youths opportunity to win the acceptance of more established residents’ by performing security work, maintaining discipline at nationalist rallies and assuming other physical tasks desired by party leaders”;

Kwa kuhitimisha, makala yangu haijalenga kuchukua upande wowote wa hoja, badala yake, inalenga kuhimiza juu ya umuhimu wa kuangalia domestic experiences tulizopitia na kufikia kuwa na hali ya militarization of political parties in Tanzania badala yaku focus kwenye experience za nchi za wenzetu, suala ambalo halina tija katika kuelewa tumetoka wapi, tupo wapi na twende wapi kama taifa; Njia sahihi ya sisi kujadiliana kwa hoja na kufikia muafaka ni kwa kurejea katika historia ya nchi yetu;

Cc nguruvi3, mzee mwanakijiji, kiranga, EMT, Jokakuu, kobello, Edwin mtei, mwigulu nchemba et al;
 
Uchambuzi wako ni mzuri sana!

Lakini naona mkuu kama vile ni bahati mbaya zaidi umeitaja asili ya Green Gurd kati katika siasa za kijani lakini ndani unaitaja asili ya UVCCM ya leo jambo ambalo ni tofauti kabisa na uhalisia wake!

Unapoitaja Green Gurd kiasili ni lazima uanzie na kuundwa kwa Jeshi la Polisi baada ya Uhuru na kuingia kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa 1992!

Hapo ndipo mahali pa chimbuko,

Lakini huko kwingine ni kuangalia UVCCM na BAVICHA tu!
 
Bahati mbaya zaidi umeitaja asili ya Green Gurd kati katika siasa za kijani lakini ndani unaitaja asili ya UVCCM ya leo jambo ambalo ni tofauti kabisa na uhalisia wake!

Unapoitaja Green Gurd kiasili ni lazima uanzie na kuundwa kwa Jeshi la Polisi baada ya Uhuru na kuingia kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa 1992!

Hapo ndipo mahali pa chimbuko,

Lakini huko kwingine ni kuangalia UVCCM na BAVICHA tu!

Jeshi la Polisi awali halikuwa na mamlaka kuliko TYL; nitarudi kujadili zaidi baadae;


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Uamuzi wa Chadema
kuanzisha ulinzi wake binafsi kama chama cha siasa umepokewa kwa hisia
tofauti miongoni mwa jamii ya watanzania; Suala hili limezua two major
schools of thought; Upande wa kwanza napenda kuuita the Mwigulu
Nchemba’s school of thought kutokana na ukweli kwamba yeye ndiye
kiongozi wa juu zaidi katika CCM aliyetoa maoni yake juu ya uamuzi huu
wa Chadema; Kwa kundi hili, hoja ya msingi ni kwamba uamuzi huu wa
Chadema ni kinyume cha Katiba ya nchi, lakini muhimu zaidi ni kwamba
kitendo hiki sio tu kina historia ya ugaidi bali pia kinajenga mazingira
ya fujo, ugaidi na nchi kutotawalika, among other things; Upande wa
pili wa hoja napenda niuite Edwin Mtei’s School of thought kutokana na
ukweli kwamba kama muasisi wa Chadema, Mzee Mtei ametoa msimamo wake
rasmi kuunga mkono uamuzi wa Chadema kuunda ulinzi wake kamili kama
taasisi; Kwa kundi hili, hoja ya msingi ya ni kwamba udhaifu wa serikali
chini ya CCM umepelekea kuibuka kwa serious gap katika suala la ulinzi
wa umma; Ni katika mazingira haya ambayo yanatawaliwa na
de-professionalization and politicization of the country’s security
system, Chadema wamebaini kwamba, wao kama chama pamoja na wafuasi wao
hawawezi tena kuwa salama katika ushindani wa siasa ndani ya demokrasia
yetu bila ya kwanza kujiundia mfumo wa ulinzi na salama wao binafsi kama
taasisi;

Katika mjadala wangu wa leo, nia yangu sio kujadili ni upande upi upo
sahihi na upande pi haupo sahihi, badala yake its just an attempt
kujadili asili ya militarization of politics katika muktadha wa nchi
yetu, hasa kwa kurejea kidogo kwenye historia ya nchi yetu; Nimechukua
uamuzi huu baada ya kuona serious gaps katika mjadala unaoendelea hivi
sasa ambao kwa bahati mbaya upo zaidi outward looking kuliko inward
looking; Kwa maana nyingine, mjadala uliopo una ‘import’ experiences za
nje ya nchi kuhusiana na suala husika badala ya kuangalia experience ya
ndani ya nchi yetu ya Tanzania ambazo zipo wazi kwa wale wanaojali
kutumia muda wao kuelewa historia yetu kama taifa; Kama tutakavyobaini,
suala husika has always and will always remain to be the “Youth
Question”;

TANU ilizaliwa July 7, 1954 as a reorganization ya TAA, mchakato ambao
uliongozwa na young “ACTION GROUP”; Vijana hawa walikuwa western
educated & exposed na walikuwa wana lead comfortable urban lives;
Kazi ya awali ya kundi hili la vijana hawa wa kizazi kipya ilikuwa ni
kutoa ahadi kwa wananchi (weusi) kwamba TANU itasimimia vyema masuala
yote muhimu kwa manufaa ya wengi (tofauti na mkoloni), hasa
Political, Social and Economic Empowerment
; Kwa mfano, kwa kuanzia,
TANU ilifuata nyayo za makundi kama vile “The Wazaramo Union” by
appealing to African racial sentiments against wafanyabiashara wa kiasia
(wahindi) na kuahidi kwamba wata short circuit hawa middle men
(wahindi) kwa kuanzisha maduka na vyama vya ushirika ambavyo ni African
based n.k;

Wananchi wengi walianza kujawa na matumaini juu ya malengo na ahadi hizi
za TANU: Pamoja na mafanikio haya ya TANU, changamoto kuu mbili
zikaanza kujitokeza kuelekea miaka ya mwisho ya 1950s: Kwanza ilikuwa ni
suala la je – ni kwa kiasi gani TANU ingefanikisha welfare kwa umma na
pia kujijengea uhalali wa Kisiasa (political legitimacy) ndani ya
Tanganyika? Na pili ambayo ni muhimu zaidi kwa mjadala wetu wa leo ni je
– role ya Vijana katika chama (TANU) ingekuwa nini, ndani ya chama
ambacho kilikuwa katika mapambano ya ndani kwa ndani kuhusiana na
generational conflicts (wazee na vijana) kuhusiana na nafasi za uongozi
katika chama na jamii kwa ujumla? Kufuatia changamoto hii, muda sio
mrefu, TANU ikagundua kwamba ili ifanikiwe, strategy muhimu ilikuwa sio
nyingine bali udhibiti wa fujo/civil disorder ambayo ilikuwa imminent
kutokana na ukubwa wa matumaini ya wananchi (hasa vijana) juu ya matunda
ya uhuru per TANU’s promises wakati wa harakati za uhuru; Ni katika
reorientation hii ya kiitikadi i.e. transformation kutokea ahadi ya
maisha bora kwa wananchi to prevention of fujo ya umma (vijana),
taratibu TANU nationalists wakajikuta wakianza kuwa na “a shared
concern”
na Serikali ya mkoloni, kwani kwa Mwalimu na washauri wake,
ikaanza kuwa obvious kwamba ikulu ya TANU faced changamoto kubwa kwani
isingeweza kufanya mastaajabu yoyote ya maana kwa wananchi per ahadi za
TANU in the 1950s;

Kufuatia hali hii, kuanzia miaka ya mwisho ya 1950s, mikutano ya hadhara
ya TANU kwa ujumla ikaanza kuwa ya Amani na Utulivu ingawa kuna nyakati
kulitokea vurugu kidogo hasa pale baadhi ya viongozi wa TANU walipokuwa
wanaichingea serikali ya mkoloni kwa wananchi na kupelekea umma
kuhamasika kutaka mabadiliko ya haraka; Muda sio mrefu, serikali ya
mkoloni ikaanza kuhofia kwamba kitendo cha viongozi wa TANU kuichongea
serikali kwa wananchi kungepelekea umma kubeba the same rhetoric kwa
kasi kubwa na kulazimisha mapinduzi nchini; Hivyo, serikali ya mkoloni
well said!
 
Mchambuzi kuna vitu vingi ambavo labda wewe huvijui juu ya TYL na mtililiko wa mambo katika nchi yetu! Kwanza grooming ya UWT in relation TYL na baadaye UVCCM! Kimsingi kuna watu waliokuwa grromed kuchukua posti TISS wakati simply walikuwa wanachama waaminifu wa TYL and UVCCM, lakini jambo hili kwa siku za usoni linaweza kuleta matatizo kwakuwa TISS hao fautishi majukumu accordingly! Yeah umefanya literature review vizuri, lakini realities zinakuwa concealed sijui ni kwa kuprotect interesti za nani!

Ajira za the then TYL ambao wakawa groomed to vyombo vya usalama ndio wanaosababisha kero hawajui wamtumikie master yupi, je wamtumikie aliewasababishia ajira yaani CCM? au wawatumikie wananchi!
 
Uchambuzi wako ni mzuri sana!

Lakini naona mkuu kama vile ni bahati mbaya zaidi umeitaja asili ya Green Gurd kati katika siasa za kijani lakini ndani unaitaja asili ya UVCCM ya leo jambo ambalo ni tofauti kabisa na uhalisia wake!

Unapoitaja Green Gurd kiasili ni lazima uanzie na kuundwa kwa Jeshi la Polisi baada ya Uhuru na kuingia kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa 1992!

Hapo ndipo mahali pa chimbuko,

Lakini huko kwingine ni kuangalia UVCCM na BAVICHA tu!
Green guards, Blue guards, Red Brigade..... ni makundi ambayo hayaeleweki na yapo chini ya vyama husika.

Sipingi uwepo wao as long as viwe regulated na jeshi la Polisi, pamoja na jeshi la wananchi kwa kupitia wizara ya Mambo ya ndani, kama makampuni ya usalama yanavyodhibitiwa.

Washike bakora, mapanga, visu, marungu, mawe, bunduki etc ... ili mradi wafuate sheria.
Hayo mambo ya kudhani kuwa kwa kuanzisha paramilitary entities as a security apparatus ndani ya vyama vya siasa, yatawatokea puani msipoangalia.
 
Mchambuzi kuna vitu vingi ambavo labda wewe huvijui juu ya TYL na mtililiko wa mambo katika nchi yetu! Kwanza grooming ya UWT in relation TYL na baadaye UVCCM! Kimsingi kuna watu waliokuwa grromed kuchukua posti TISS wakati simply walikuwa wanachama waaminifu wa TYL and UVCCM, lakini jambo hili kwa siku za usoni linaweza kuleta matatizo kwakuwa TISS hao fautishi majukumu accordingly! Yeah umefanya literature review vizuri, lakini realities zinakuwa concealed sijui ni kwa kuprotect interesti za nani!

Ajira za the then TYL ambao wakawa groomed to vyombo vya usalama ndio wanaosababisha kero hawajui wamtumikie master yupi, je wamtumikie aliewasababishia ajira yaani CCM? au wawatumikie wananchi!
TYL ... wala haipo siku hizi, especially baada ya trade liberalization in mid to late 80s.
Hata Zanzibar walikuwa na pioneers ... Mao, Hitler, Castro, Sankara walikuwana youth leagues ambazo zilikuwa na mandates za kipolisi depending on the local government.
Miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na kambi za vijana especially CCM ambazo uwazi wake unatatanisha, ila according to them ni kama kambi ambazo zipo nchi nyingi tu ... hata yale mauaji ya Norway ni katika kambi kama hizi, ambazo nia yake ni kukuza vijana kisiasa....

Hotuba aliyotoa Kagame kumkashifu JK nayo ilitolewa kwenye kambi za vijana.
Putin naye hutumia kambi za vijana wa chama chake, hata republicans wa States especially wale walio extremely right.

Kuanzisha kambi ni kawaida, ila ziwe regulated.
 
Mchambuzi pamoja na uchambuzi wako mzuri ambao angalau umetukumbusha historia ya TANU na UVCCM, naona bado hujagusa evolution ya green guard ambayo kimsingi ni tofauti kabisa na UVCCM au hiyo TYL ya wakati wa TANU. Kwa tafsiri nyingine, naona hapa umejadili foundation ya UVCCM na BAVICHA, lakini hujagusia kabisa green guard ambayo kwa mjibu wa nyaraka mbalimbali, ilianza kufanya kazi rasmi mwaka 2007 kwenye uchaguzi wa kiteto. Na ndiko ambako kwa mara ya kwanza watu waliexperience matendo yake ya kikatili. Na ukiangalia, malengo ya uanzishaji wake, yaani green guard na red brigade ya sasa, ni tofauti kabisa na yale ya TYL au UVCCM ya sasa na BAVICHA.

Tunasubiri uchambuzi wako zaidi wenye kuelezea nafasi ya green guard ndani ya CCM.
 
Mchambuzi pamoja na uchambuzi wako mzuri ambao angalau umetukumbusha historia ya TANU na UVCCM, naona bado hujagusa revolution ya green guard ambayo kimsingi ni tofauti kabisa na UVCCM au hiyo TYL ya wakati wa TANU. Kwa tafsiri nyingine, naona hapa umejadili foundation ya UVCCM na BAVICHA, lakini hujagusia kabisa green guard ambayo kwa mjibu wa nyaraka mbalimbali, ilianza kufanya kazi rasmi mwaka 2007 kwenye uchaguzi wa kiteto. Na ndiko ambako kwa mara ya kwanza watu waliexperience matendo yake ya kikatili. Na ukiangalia, malengo ya uanzishaji wake, yaani green guard na red brigade ya sasa, ni tofauti kabisa na yale ya TYL au UVCCM ya sasa na BAVICHA.

Tunasubiri uchambuzi wako zaidi wenye kuelezea nafasi ya green guard ndani ya CCM.

Mkuu Lukolo, karibu katika mjadala; Kama umenisoma vizuri, mada yangu hailengi kuelezea nani yupo sahihi bhaina ya CCM na Chadema, badala yake kuhimiza juu ya umuhimu wa kurejea katika historia ya nchi yetu, hasa siasa za TANU kuelekea uhuru wa Tanganyika; Kwa kufanya hivyo ndio kutatusaidia kuelewa chanzo cha militarization of political parties, hasa katika muktadha wetu Tanzania; Hoja yangu ya msingi kama haujaipata vizuri ni kuonyesha militarization of political parties asili yake ni nini; Sasa kwa kuangalia historia ya nchi yetu, it all began with the formation of TYL ambayo amongst others, ilikuwa na majukumu niliyoyaainisha katika bandiko namba moja, majukumu ambayo yana uhusiano wa moja kwa moja na majukumu ya green guard; Pia hata uamuzi wa Chadema kuja na chombo chake binafsi, majukumu yake yanakuwa na orientation zinazofanana na za CCM; kwa maana nyingine, green guard ni matokeo ya vision na mission of TANU kupitia TYL, na kwa Chadema pia, utekelezaji wa brigade yake hautakuwa wa maana bila ya kuiweka Bavicha in the front seat;
 
Mchambuzi pamoja na uchambuzi wako mzuri ambao angalau umetukumbusha historia ya TANU na UVCCM, naona bado hujagusa evolution ya green guard ambayo kimsingi ni tofauti kabisa na UVCCM au hiyo TYL ya wakati wa TANU. Kwa tafsiri nyingine, naona hapa umejadili foundation ya UVCCM na BAVICHA, lakini hujagusia kabisa green guard ambayo kwa mjibu wa nyaraka mbalimbali, ilianza kufanya kazi rasmi mwaka 2007 kwenye uchaguzi wa kiteto. Na ndiko ambako kwa mara ya kwanza watu waliexperience matendo yake ya kikatili. Na ukiangalia, malengo ya uanzishaji wake, yaani green guard na red brigade ya sasa, ni tofauti kabisa na yale ya TYL au UVCCM ya sasa na BAVICHA.

Tunasubiri uchambuzi wako zaidi wenye kuelezea nafasi ya green guard ndani ya CCM.

Nikweli ndiomana namelazimika kuuliza kama ni bahati mbaya vile, kile kilichoelezwa katika kichwa cha uchambuzi sio kile kilicho ndani ya uchambuzi huo!
 
Kwa mujibu wa maelezo haya ni historia tu inajirudia. lakini kwa sasa kwa vile hatuna mkoloni tunayepigana naye na vyombo vya ulinzi na usalama ni vya kwetu tuna wajibu wa kufanya tofauti, kuhakikisha hatuundi vikundi ndani ya vyama vyetu vinavyofanana na vikosi hivyo. Hii itawezekana tu kwa kuvisuka vikosi vyetu ili kuviondolea - de-professionalization and politicization - kwa mujibu wa maelezo yako. Otherwise thank you for the historical background.
 
Habari ndeeeeefu, maudhui kiduchuuuu!
 
At least you have cooled my nerves, as for a couple of past days Mwigulu has been spoiling my mood.

Yes. At least we can read the logical and factual literature about past Political parties militarization in our country.
Mchambuzi we are waiting anxiously your comments about what Yericko Nyerere has raised in post #3 of this thread.
 
Last edited by a moderator:
Nikweli ndiomana namelazimika kuuliza kama ni bahati mbaya vile, kile kilichoelezwa katika kichwa cha uchambuzi sio kile kilicho ndani ya uchambuzi huo!

Hoja ya msingi hapa ni je, nini ni chimbuko la militarization of party politics in Tanzania? Jibu ni TANU kupitia TYL, na ni katika muktadha huo, green guard ndiyo ikazaliwa, na kwa vile historia inajirudia (rejea historia juu ya majukumu ya TYL late 1950s), chombo cha chadema kinazaliwa nyakati hizi na at the fore front kutekeleza shughuli hii itakuwa sio chombo kingine ndani ya chadema bali bavicha, kwa sababu zile zile za enzi za TANU na TYL;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hizi nguvu zingelikuea zinaelekezwa kwenye kutatua matatizo yetu ya kiuchumi ninasmini tungekuwa mbali sana. Ma-green, while, yellow, red and black guard or brigade hayana masilahi kwa taifa letu.
Mfumo wa ulinzi ulipo unajitosheleza. JWTZ, TISS, Police, mgambo...JKU na KMKM Huko Zanzibar, Auxilary police from security companies. Kama kuna gap.... Bunge litunge sheria nyingine and not otherwise. Vyama Vinne vina wabunge so a private bill motion can be passed.
 
Hizi nguvu zingelikuea zinaelekezwa kwenye kutatua matatizo yetu ya kiuchumi ninasmini tungekuwa mbali sana. Ma-green, while, yellow, red and black guard or brigade hayana masilahi kwa taifa letu.
Mfumo wa ulinzi ulipo unajitosheleza. JWTZ, TISS, Police, mgambo... Auxilary police from security companies. Kama kuna gap.... Bunge litunge sheria nyingine and not otherwise. Vyama Vinne vina wabunge so a private bill motion can be passed.
Mkuu big up, nakubaliana na wewe 100%.
 
Mkuu Lukolo, karibu katika mjadala; Kama umenisoma vizuri, mada yangu hailengi kuelezea nani yupo sahihi bhaina ya CCM na Chadema, badala yake kuhimiza juu ya umuhimu wa kurejea katika historia ya nchi yetu, hasa siasa za TANU kuelekea uhuru wa Tanganyika; Kwa kufanya hivyo ndio kutatusaidia kuelewa chanzo cha militarization of political parties, hasa katika muktadha wetu Tanzania; Hoja yangu ya msingi kama haujaipata vizuri ni kuonyesha militarization of political parties asili yake ni nini; Sasa kwa kuangalia historia ya nchi yetu, it all began with the formation of TYL ambayo amongst others, ilikuwa na majukumu niliyoyaainisha katika bandiko namba moja, majukumu ambayo yana uhusiano wa moja kwa moja na majukumu ya green guard; Pia hata uamuzi wa Chadema kuja na chombo chake binafsi, majukumu yake yanakuwa na orientation zinazofanana na za CCM; kwa maana nyingine, green guard ni matokeo ya vision na mission of TANU kupitia TYL, na kwa Chadema pia, utekelezaji wa brigade yake hautakuwa wa maana bila ya kuiweka Bavicha in the front seat;
Nimekuelewa vizuri sana Mchambuzi, na actually ninaelewa vema namna ambavyo UVCCM imekuwa kwa muda mrefu ikitumika kama sehemu ya military force ya CCM. I was once a UVCCM member na ninajua ni namna gani tuliplay role mbalimbali zikiwemo za ulinzi na usimamizi wa mambo mbalimbali ya chama. Lakini ukiangalia hali ya sasa, ni kama UVCCM na BAVICHA vimekuwa ni vyombo vya propaganda, huku vikiacha kazi ya ulinzi na usimamizi wa shughuli za chama mikononi mwa green guard na red brigade.

Lakini nikirejea pia kwenye post yako ni kama TYL walikuwa ni wanaharakati zaidi kuliko militia forces za chama kama ambavyo green guard na red brigade zinavyotumika hivi sasa. In so saying, vyama vya sasa, vimewaacha UVCCM kuendelea kuwa wanaharakati, huku militarization ikipelekwa kwa kikundi kingine. In this regard we can consider a formulation of one extra body of these parties in addition to jumuia ya wazazi, umoja wa wanawake, and UVCCM or BAVICHA; which I think its not bad, given the ever expanding population and the diminishing abilities of our police forces.

Lakini pia turudi nyuma kwenye post yako, una conclusion gani kuhusu haya? Is this how we need to go? Turudishe mamlaka yale ya ulinzi kwa UVCCM na BAVICHA au ni sahihi kuendelea na hizi harakati za kuunda vikundi maalumu vya kiulinz? Na ni yapi yanaweza kuwa madhara yake? Na zaidi ya yote hivi vikundi viwezeshwe kiasi gani/viwe na nguvu kiasi gani? Kama ya polisi au kama ya jeshi?
 
Mchambuzi
Ni kwa bahati mbaya sana analysis yako haijakamika... Mfano inashindwa kuonyesha kwamba kuna vyombo halali vilivyoanzishwa kisheria na kikatiba kuziba mapengo ambayo yalikuwepo kabla ya Uhuru. Vyombo hivi vimeanzishwa miaka ya 60/70 etc Nimeshavitaja hivyo vyombo. Hivyo basi nadhani iwe CCM au CDM au mwingine kuanzidha chombo rasmi cha ulinzi lazima viwe registered kwa sheria za sasa... Maana hata Vikundi kama NGO zina-be registered na kama chama au vyama vitaweka baysna vikundi vya ulinzi kwenye katiba zao lazima vyombo husika viridhie.

Lakini nchi hii si ina Bunge na vyama husika ndio vinara kwenye hilo Bunge? Kama ni muhimu kila taasisi iwe na jeshi lake basi sheria itungwe labda iwe taasisi yoyote kwanini vyama tu?

Mwisho
Acha kuwasemea CDM; categorically they said wanataka ulinzi mbadala na sio under BAVICHA bali under CDM hayo mengine ya kwako mkuu...

It extremly wrong kulinganisha mazingira ya before uhuru yaani chini ya serikali ya kikoloni na wakati nchi ikiwa chini ya serikali iliyo chaguliwa kimokrasia... These are two different environments.
 
Back
Top Bottom