Asili ya binadamu

Asili ya binadamu

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Posts
3,811
Reaction score
1,607
Mtoto mdogo msichana alimwuliza mama yake:
"Mama, asili ya binadamu ilianza vipi?"

Mama akajibu,
"Mungu aliumba Adam na Hawa, baadaye wao wakawa wanazaa watoto mpaka tukafikia sisi binadamu wa leo"

Siku mbili baadaye msichana akamwuliza baba yake suali lile lile. Baba akajibu:
"Miaka mingi iliyopita, kulikuwa na masokwe wawili, mke na dume, hawa wakawa wanaendelea kubadilika hatua kwa hatua mpaka kufikia hatua hii tuliyonayo binadamu wa leo".

Jawabu ile ilimchanganya msichana, ikabidi arudi kwa mama yake kumwuliza:
"Mama, wewe uliniambia binadamu walianza na Adam na Hawa, baba kaniambia binadamu walianza na sokwe, ukweli ni upi?

Mama akajibu:
"Sikiliza mwanangu, yote ni sawa, isipokuwa baba yako anakuelezea jinsi familia yao ilivyoanza na mimi ninakuelezea familia yangu ilianza vipi"
 
Hahhaha Ntachinja mtuuuu hahahahahahahahahahahahahhhahaahahahaha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom