Asili ya binadamu ni ipi hasa

kichakaa man

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
5,487
5,111
kwa muda mrefu nimekuwa najaribu kujiuliza asili ya binadamu dunian hasa ni ipi kuna binadamu wa aina tofaut kwa maana ya rangi, muonekano na sifa zao na hata maumbile na nimejaribu kutafakar sana kuhusu asili ya binadamu lakin huwa sipati jibu la kuridhisha kabisa.

Ukisoma vitabu vya dini vinasema binadamu tuliumbwa na mwenyezi mungu na mtu wa kwanza ni Adamu then Eva lakin ukifuatilia baada ya hapo wakafanya maasi na mungu alipo watoa kwenye bustan yake wakaja kuzaliana huku nje hapa huwa najiuliza hapa je adamu na hawa walikuwa ni wazungu,wahind, wachina , au waafrika kwa sababu baada ya hapo naona jamii NYINGI zilikuja kutokea . kama walikuwa ngozi nyeupe je sisi waafrika asili yetu halisi ni ipi had tupo hiv au mungu kulikuwa na watu wengine mbali na adamu na hawa yaani walikuja kuwakuta baada ya kufukuzwa kwenye bustan na hao walio wakuta je nani aliwaumba hao watu(bible huwa inasema watu wa mataifa huwa sielewi hao watu wa mataifa hasa je hawakuwa wameumbwa na mungu na kama wali umbwa na mungu kipi hasa kilifanya awe kama kawatenga na kuwapendelea wa Israel )

Upande wa Pili ukisoma vitabu kisayansi wanasema asili ya binadamu ni nyani/sokwe hapa kuna maswal kwanini hatuendelei kubadilika yaani kutoka KUWA nyani had una binadamu nin hasa kilifanya hii process kusimama na kwanin had leo kuna nyani/sokwe lakin hawabadilik kuwa binadamu.

Na je asili ya hao sokwe wa zamani ambao wanasema walikuwa ni binadamu walitokana na nin kipi hasa asili ya hao sokwe(binadamu wa sasa) na je kulikuwa na sokwe wa aina gan kwa sababu Leo hii wapo weusi,wazungu, wachina, n.k

Naomben mnisadie majibu wataalamu wa mambo

Asanteni
 
Nani kasema kuwa binadamu tulikuwa nyani na kwanini wazungu wanasema binadamu tulianza kuwa nyani
Ni nadhani wana lao jambo... Na ukisoma historia wanasema fuvu la binadamu wa kwanza alietoka kwa nyani lilivumbuliwa olduvai gorge Tanzania...
Wao wametuletea dini na kusema binadamu wa kwanza alikua mweupe, wametulitea sayansi zao na kusema binadamu wa kwanza alikua sokwe... Kuna sokwe mweupe???
Wanatung'ong'a bila sisi kujua. Ko binadamu mweupe aliumbwa na Mungu na sisi weusi tumetokea kwa sokwe?
 
Kuna muda sayansi inakuwa ni zaidi ya dini,maana kuna mambo unaona kabisa hayaingii akilini ila kwa kuwa wanasayansi wamesema basi unalazimika kukubali tu maana ukibisha utaonekana huna elimu.

Najua hapa watakuja watu kulitolea maelezo hili jambo ila hakuna jipya zaidi ya kuaminishana tu kuhusu hili jambo,maana kama ingewezekana kuthibitishika hili suala la kwamba binadamu tulikuwa minyani basi watu wasingekuwa wakiendelea kulitilia shaka hili suala.
 
Pamoja na nadhalia mbalimbali zinazoeleza chanzo cha binadamu ukweli unabaki palepale kuwa binadamu aliumbwa kwani inaonyesha wazi kuwa umbo lake ni kazi iliyohitaji ujuzi wa hali ya juu. Mfano, macho yapo juu kwenye fuvu la kichwa ili kumwezesha kuona mbali. Hilo linathibutisha kuwa kuna Nguvu ya uumbaji iliwezesha uumbaji huo. Asili ya pili inaonyesha mahitaji ya uumbaji huo, hapa asili inaonyesha mazingira yaliandaliwa ili kumfanya binadamu aweze kuishi, aliwekwa sehemu yenye hewa safi, maji yanayofaa, vyakula vya kumwezesha kukua, dawa za kumtibu nk. Jambo hili haliwezi kutokea kwa bahati mbaya. Dhana ya unyani wa binadamu ni kuwa binadamu anabadilika kutokana na mazingira anayoishi, jambo hili linachangia katika rangi yake, kimo, unene na hata umri yaani idadi ya miaka anayoishi. Hitimisho lenye mashiko ni kuwa binadamu aliumbwa na Muumbaji nguli, mwenye uwezo ulio juu sana ukilinganisha na jinsi binadamu anavyoweza kufikiri. Muumbaji huyo bado yupo hadi hivi leo kwani maisha yake bila shaka ni marefu kiliko ya binadamu. Fanyeni bidii kumtambua na kugundua kwanini alituumba. Nawasilisha
 
Tatizo watu hawajui wala kuielewa nadharia ya evolution lakini wanakomalia kusema eti evolution inasema binadamu alitokana na nyani.
Evolution inasema uhai ulianzia majini, kwahiyo watu nao wana asili ya majini.Msitumie nguvu kusema binadamu alitokana na nyani bali mfanye juhudi za kujua nyani walitoka wapi.

Evolution inasema evolution ya watu ina uhusiano wa karibu na ile ya primates wengine kama nyani na siyo kwamba nyani ndio waliobadilika kuwa watu.
Ingawa Evolution ina mapungufu yake[sababu ya info ambazo hazijapatikana] lakini ni bora kuliko creationism iliyojaa uongo na utapeli wa fikra.
Kabla mtu hajaanza kuichambua nadharia ya evolution ni bora awe na uelewa wa evolution na siyo kuzungumzia kitu asichokijua.
 
Halafu unaamini huo uongo?
 
Halafu unaamini huo uongo?
We hujaona watu ambao wanasema hawaamini dini wanaamini sayansi? hayo ndiyo matokeo ya kuweka imani yako kwenye sayansi,ukibisha unaonekana huna elimu ni sawa na kukufuru maana unawabishia wanasayansi.
 
Mwanadamu aliumbwa na Mungu. Asili ya mwanadamu scientifically and spiritually ni creative design
 
Tatizo watu hawajui wala kuielewa nadharia ya evolution lakini wanakomalia kusema eti evolution inasema binadamu alitokana na nyani.
Evolution inasema uhai ulianzia majini, kwahiyo watu nao wana asili ya majini.Msitumie nguvu kusema binadamu alitokana na nyani bali mfanye juhudi za kujua nyani walitoka wapi.

Evolution inasema evolution ya watu ina uhusiano wa karibu na ile ya primates wengine kama nyani na siyo kwamba nyani ndio waliobadilika kuwa watu.
Ingawa Evolution ina mapungufu yake[sababu ya info ambazo hazijapatikana] lakini ni bora kuliko creationism iliyojaa uongo na utapeli wa fikra.
Kabla mtu hajaanza kuichambua nadharia ya evolution ni bora awe na uelewa wa evolution na siyo kuzungumzia kitu asichokijua.
Huko usiende mkuu utafeli maana hujawahi kuwa na ujasiri wa kutosha kusimamia evolution. Sio tu nyani alitoka wapi tunaenda zaidi nini kilikuwepo kabla ya uwepo wa Chanzo cha nyani au evolution of organisms
 
Kwenye evolution Mimi siyo mbobezi.
Mapungufu au kutokuelezwa vzr kwa evolution hakuipi marks creationism.
 
Watu wengine shida tupu ......eti Mungu aliumba mtu miaka isiyozidi 10k iliyopita.......huo uongo mpeane huko makanisani mkija jf elezeni facts na siyo superstition.
 
Evolution ina majibu yote ya kwanini hawa wa huku wakabaki weusi na walioenda kule wakawa weupe na kuendelea, inaenda kufeli kwenye kuelezea ni nini hasa kilikuepo kabla ya nyani.

Hapa ndiyo credibility ya evolution inapopotea.
 
Mkuu ukiwaza sana unaweza kujikuta unatumia muda mwingi kujaribu kutatua fumbo ambalo halitatuliwi kwa akili ya kibinadamu.

Cha muhimu amini kuwa Mungu yupo, naamini Mungu yupo kutokana na baadhi ya vitu nilivyowahi kuviona na ninavyoendelea kuviona. Hivyo naamini pia sisi binadamu tumeumbwa na Mungu na yeye ndio anajua kwanini tumekuwa weusi wengine wakawa wazungu na wengine wakawa design tofauti.

Chamuhimu sana ninachowekaga mbele kwangu sio kutaka kujua nini asili yetu bali kuishi kwa amani duniani na kutenda yaliyomema kwa kuwa na imani kuwa Mungu yupo. Mengine yote namwachia yeye
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom