Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,259
- 79,826
"MTOTO WA NYOKA NI NYOKA"
Na, Robert Heriel
Panya huzaa panya
Paka huzaa paka
Mbwa huzaa mbwa.,.....n.k
Mtoto wa nyoka ni nyoka, wahenga walisema kisha wakaongezea, maji hufuata mkondo. Baadaye Yesu wa Nazareth akasema; huwezi chuma tini kwenye zabibu" Hii ni kusema, muembe huzaa maembe, Mzabibu huzaa zabibu n.k
Malaya huzaa Malaya
Mwizi huzaa mwizi
Muuaji huzaa muuaji
Mdhulumaji huzaa mdhalumaji.
Kabla sijafika Mbali, nitoe lengo la Makala hii.
LENGO: Vijana tuwe makini katika chaguzi za maisha hasa tunapoenda kuchagua wenzi wa maisha. Kwani kwa kutokufanya hivyo inaweza kuleta athari baadaye.
Tuendelee sasa.
Huwezi muambia malaya aache umalaya ikiwa yeye ndio asili yake. Huwezi mwambia mchoyo aache uchoyo wakati yeye ndio asili yake. Huwezi mwambie mdhulumaji aache dhuluma wakati yeye ndio asili yake. Huwezi mwambia mvivu aache uvivu wakati hiyo ndio asili yake. Viumbe wote tuliomo humu duniani tunaongozwa na silika. Kila mtu anasilika yake kulingana na asili yake aliyoirithi kutoka kwa wazazi wake.
Siku hizi watu wanahangaika katika ndoa, siku hizi ni kawaida kwa ndoa kuvunjika kutokana na kutokuelewana ndani ya ndoa. Vijana wa siku hizi tumekosea sehemu nyeti sana ambayo ndio msingi wa mahusiano.
Vijana wanahangaika kutafuta wanawake warembo wa sura na maumbile. Wanahangaika kutafuta wanawake wenye matako makubwa, na nyonga nene. Wakati huo huo wanawake nao wanahangaika kutafuta wanaume wenye pesa na utajiri mwingi, wakitafuta wanaume wenye kazi zenye vipato vizuri. Wanahangaika kutafuta wanaume wazuri wa sura na warefu wa maumbile
Wanasahau jambo moja muhimu, "Mtoto wa Nyoka ni Nyoka" Wanasahau kuangalia tabia au silika za wazazi wa mwezi anayemtafuta.
Wakati wa zamani haikuwa hivyo, ilikuwa lazima uchunguzi ufanyike. Mchumba alikuwa akichunguzwa, tabia na silika za jamii yao, magonjwa na maradhi ya kurithi yao, imani, mila, na desturi zao, uchapakazi, kisha mwisho kabisa maumbile. Wazee wa zamani walikuwa na sababu kubwa na muhimu ya kufanya hivyo. Moja wapo ni kutokuharibu kizazi chao
Wazee wa zamani walijua kabisa mtoto wa nyoka ni nyoka. Endapo mzazi ni mchoyo, mwizi, malaya, muuaji basi hata watoto wake watakuwa hivyo. Na ndivyo ilivyo.
Kikawaida, ukitaka kuoa mwanamke yeyote yule lazima umuangalie mama yake, kisha uangalie ukoo wao na jamii aliyotoka kwa ujumla. Pia ukitaka kuolewa na mwanaume, basi sharti umuangalie Baba ya huyo mume mtarajiwa, kisha angalia ukoo na jamii anayotoka. Hapo ndio utajua tabia halisi ya mke wako baadaye atakapofikisha umri kama wa Mkwe wako huyo
Ukiona mtu ni malaya basi jua wazazi wake au mmoja kati ya mzazi wake ni Malaya. Ukiona Mtu ni mwizi basi jua kabisa wazazi wake au mmoja wa wazazi wake ni mwizi. Asilimia zaidi ya 99% mtoto hurithi tabia kutoka kwa wazazi wake iwe mama au baba au ukoo, au jamii husika ya wazazi wake.
Kuna watu wataniambia kuwa mbona kuna wazazi wanatabia nzuri, wengine ni wachungaji au mashehe lakini watoto wao wanatabia mbaya?
Jibu ni kuwa, wazazi hao ni wanafiki, hakuna mzazi mwenye tabia nzuri alafu mtoto akawa na tabia mbaya hiyo haipo na haitokuja kutokea. Kinachofanyika ni kuwa baadhi ya wazazi hujifanya watakatifu mbele ya jamii lakini kwa kificho hufanya maovu. Na kama hafanyi kabisa basi kimwili hafanyi maovu lakini nafsi yake inafanya uovu kwa kutamani kuufanya sema mazingira hayaruhusu.
Upo ushahidi wa kutosha kuwa jinsi mzazi alivyo ndivyo mtoto wake atakavyokuwa kwa sehemu kubwa. Kama Baba yako alioa na akaacha wanawake zaidi ya mmoja kabla hajazeeka basi kunauwezekano mkubwa nawe ukafanya vivyo hivyo.
Hata hapo mtaani, au angalia kwenye ukoo wenu, au familia yenu, fanya utafiti mdogo, Watoto wengi ambao Baba zao walitia Mimba na kutelekeza mabinti waliowatia mimba utashangaa nao asilimia kubwa wamefanya hivyo hivyo. Alafu wale ambao Baba zao walizaa kwenye ndoa bila kuzaa nje ya ndoa basi kwa asilimia kubwa nao wamefanya kama baba zao.
Pia chunguza, wamama wengi ambao wamezaa na mwanaume zaidi ya mmoja basi hata watoto wao nao kwa asilimia kubwa hufuata mtindo huo huo. Au Wamama ambao hawaishi na waume zao utashangaa hata watoto wao hawaishi na waume zao kwa asilimia kubwa. Lakini wamama ambao wameolewa na wamedumu kwenye ndoa mpaka uzee au mpaka mmoja wa wanandao amefariki basi watoto wao kwa sehemu kubwa huolewa na kudumu kwenye ndoa.
Unapooa au kuolewa lazima uzingatie kitu inaitwa Tabia ta mtu unayeenda kuoa au kuoelewa naye. Usiishie kwenye kutafuta uzuri au pesa, ukasababisha maafa kwenye kizazi chako.
Kuna watu wanasema tabia mtu anaweza kubadilishwa. Ni uongo. Tabia haibadiliki, tabia ni asili ya mtu. Inatoka ndani ya mtu sio nje. Tabia ni kama ngozi tu, ukiichubua kwa mafuta ya kemikali ili ngozi iwe nyeupe, itakuwa nyeupe lakini ndani ni nyeusi tuu. Ndio maana mtu hata ajichubue vipi awe mweupe kama mzungu lakini lazima azae mtoto mweusi.
Vivyo hivyo kwa tabia, unaweza ukajitahidi kuibadilisha tabia kwa sehemu kubwa, yaani kuichubua mpaka ukaonekana kweli umebadilika lakini kwa ndani hujabadilika. Utakuwa umeacha kwa nje tuu lakini kwa ndani tabia ile inaendelea. Tabia ukiizima inajificha kwenye unconscious mind. Yaani inakuwa kama haipo kumbe ipo. Tabia hiyo unairithisha kwa watoto na kama watoto hutowachubua basi itadhihirika.
Ndio maana unakuta mchungaji au sheikhe unawezamkuta swala tano na mtu mwema kwa nje, lakini watoto wake wakawa wahuni na waovu. Hiyo ni kutokana na tabia halisi ya wazazi au mmoja wa mzazi kuwa ni muovu au mhuni.
Hii pia unaweza ikuta kwa Watoto waliozaliwa na wazazi waovu au wahuni. Unaweza kuta mtoto amezungukwa na wahuni, lakini asiwe mhuni, asivute bangi, asiwe malaya licha ya kuzungukwa na malaya. Hii inatokana na kuwa, mzazi wake mmoja sio mhuni kiasili au sio malaya.
Na kama wazazi wote kiasili ni wahuni, malaya, wachawi, wachoyo piga ua garagaza huyo mtoto lazima awe na tabia hizo hizo.
Huwezi oa mwanamke malaya alafu ukamfanya aache umalaya, never ever. Utahangaika wee! Ukifanikiwa sana atafanya kwa siri kubwa. Na kama hatafanya basi, atawarithisha watoto wako uliowazaa. Yaani utazaa vitoto malaya, au vichoyo, au viizi, viuaji na maovu mengine.
Unaweza ukahangaika kumlea mtoto wee, pigia kelele wee! Chapa bakora wee! Lakini nakuhakikishia kama amerithi kwako au kwa mwenza wako utakuwa unajihangaisha tuu.
Kwa wale wanasaikolojia wataungana na mimi hasa waliomsoma mwanasaikolojia Nguli aitwaye Sigmund Freud.
Huyo ameelezea kinagaubaga jambo hili katika nadharia yake "Freudian Psychoanalytic Theory of Personality"
Pia kwa wale wasomaji wa vitabu vya teolojia hasa Biblia wataungana na mimi kuwa Kwenye ishu za Kiroho, Mtoto wa Nyoka ni nyoka siku zote wala hataweza kubadilika.
Na ndio maana Yesu anakuambia, "usifungwe nira na wasio amini" Mungu aliwaambia waisrael wasioane wala kuolewa na mataifa mengine bali wachukuane wao kwa wao.
Huwezi ukazaliana na malaya alafu ukamuomba Mungu watoto wako wasiwe malaya. Huwezi na haiwezi kutokeo.
Huwezi taka kuzaa na mzungu au muarabu alafu ukataka kizazi chako kibaki kuwa cha Kiafrika, ni lazima mtoto atatoka chotara.
Huwezi kufunga ndoa na kuzaa na muuaji alafu ndani ya nyumba ukaomba asiwepo muuaji wakati unafahamu fika kwenye kizazi chako lazima atoke muuaji kwani mama/baba ni muuaji.
Kama unataka watoto warefu, basi chukua mtu mrefu
Kama unataka watoto weupe, chukua mtu mweupe
Lazima kwenye kizazi chako atatako mtoto mweupe iwe watoto au wajukuu.
WITO:
Lazima tuwe makini tunapoenda kuanzisha mahusiano ya kindoa. Tuzingatie mahitaji yetu.
Kama hutaki malaya, basi usioe malaya kwa maana huna uatakachokifanya akabadilika, zaidi sana unaenda kuzalisha malaya zaidi duniani.
Kama hutaki mchoyo basi usioe mwanamke mchoyo.
Utajuaje tabia za mwenzi unayetaka kumuoa, fanya tafiti kwa wazazi wake, ukoo wao, ndani ya miezi sita utajua mbivu na mbichi.
Kumbuka: Tabia hujificha kwenye unconscious mind pale super- ego inapokuwa na nguvu zaidi ya Ego. Kumbuka tabia ya Mtu(Human Behaviour) inajengwa na mambo matatu yaliyopo kwenye fikra(Mind) mambo hayo ni Id, Ego, na Super ego
Id - Instincts (Silika) Hii haibadiliki) Mtu huirithi kutoka kwa wazazi.
Ego - Reality (Uhalisia)
Super-ego _ Morality (Maadili) Hutokana na jamii
Nipumzike sasa!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300