Ashukuru "mungu" wake kizazi cha viongozi wa dunia kimebadilika sana, enzi za akina Obama tungezungumza mengine.

CreativityCode

Senior Member
Aug 8, 2020
158
653
Ni ukweli usiopingika kizazi cha viongozi wa kidunia na marais wa nchi kubwa duniani kimebadilika sana.

Tukianza na Katibu Mkuu wa UN ni kama amepoa sana na taasisi yake imekosa mashiko.

Tukija kwa Taifa la Marekani nalo sera zake za nje zimekosa meno kabisa kutokana na Rais wao Trump kuangalia zaidi mambo yake ya ndani kuliko ya nchi nyingine za dunia. Afrika ndiyo imeachwa kabisa ijiendee yenyewe.

Hali imekuwa tofauti kabisa na kizazi cha uongozi cha akina Obama, Ban Ki-Moon, Tony Blair ama Gordon Brown. Kizazi hiki cha viongozi wa dunia kilikuwa ni moto wa kuotea mbali kwani hakikumvumilia kiongozi yeyote duniani aliyekuwa na chembechembe za udikteta na kunyima watu haki ya kuishi na uhuru wa kujieleza.

Nawaambia ukweli kabisa Obama angekuwa madarakani Tanzania tungezungumza mengine.

Pia ashukuru sana coronavirus kwani imewafanya viongozi wa kidunia kushughulikia mambo yao zaidi kuliko ya nchi nyingine na ni nadra sana na wala tusitegemee kuona waangalizi wa uchaguzi kuja Tanzania hivyo huyu bwana na tume yake wanaweza kufanya lolote lile kuhakikisha wanakuwa madarakani.

Pengine tuishukuru teknolojia ya mawasiliano maana dunia inaweza kufuatilia chochote kile watakachokuwa wanakifanya hasa kwenye kujumlisha kura labda wasitumie computer maana zinaweka na kutuma records kwa mabeberu hivyo wataona kila gumashi litakalokuwa linafanywa.

SIKU NJEMA
 
Kuna haja gani ya kuongoza chama kisichokubalika na wananchi?
Chama ambacho hakishindi bila kuiba kura.
Chama ambacho viongozi wake wanakiri hadharani kuwa ushindi wait unatokana na kuwatumia polisi na TISS.
Chama ambacho kinaitumia NEC kuwaengua wapinzani wake.
Hiki chama hakika Ni CHAMA CHA MASHETANI
 
[SUB]Kuna mambo huyafahamu vizuri,[/SUB]
[SUB]Wote hao uliowataja walimkuta Museveni na walimwacha.[/SUB]
 
Mtaongea mengi huu mwaka eti mnaibiwa ?? Mtaibiwa mara ngapi mpaka mjifunze kuweka ulinzi wa kura zenu......hivi nyomi ya mbagala na ya dodoma kweli inautata kuhusu kuibiwa....vyama vya upinzani tanzania mmepoteza mvuto
 
Wanadai kuwa wale watu waliojaa pale Jamhuri Dodoma walipelekwa na mafuso. Wanasahau kuwa bwana mkubwa huwa anasimama na kuongea na watu njiani, hawaelewi maana ya ukaribu wa kiongozi na anaowaongoza.
 
Africa Kwa sasa inaongozwa na nguvu ya Mungu pekee, Na nchi za Africa zilizochagua kuongozwa na nguvu ya Mungu, ndio hazitatishika na Marekani Wala Umoja wa mataifa Kwa Sera zake za kukandamiza nji ndogondogo! Mungu kaamua kuingilia Kati, Yatosha kuonewa, Mungu ameskia kilio cha Watu wake Africa

Na wakileta mchezo kazi yetu ni kuwashitaki Kwa Mungu, watapigwa wachakae, Korona haitakwisha, Vimbunga vitadidimiza Aridhi zao

Matetemeko ya Aridhi hayatapoa,

Na sasa tumejipanga,Kila anayeonekana kuwa na seara za kibeberu, hawezi kupewa nchi aongoze, Atapuuzwa kama anavyopuuzwa huyu wetu!

Mungu Akiwa upande wetu ni Nani wa kutushitaki?

Mataifayote yenye mwelekeo wa Sera za kibeberu yatapigwa Kwa laana ya kibeberu

Tanzania haitapigwa Bani na mtu yeyote, na atakayejaribu, mapigo ya Mungu yaipiga nchi yake
 
HAKUNA CHA BEBERU WALA MTOTO WAKE NA BEBERU, KIBARAKA WALA MTOTO WAKE NA KIBARAKA ATAIGUSA NCHI YETU. AMSTERDAM AMEKUAJE KWANI? MNAANZA KUKATA TAMAA KABLA YA WAKATI? IACHENI TANZANIA IITWE TANZANIA NA MSHINDWE WOTE WENYE NIA OVU NA TANZANIA, UWE MZAWA AU WA KUJA KATIKA JINA LA YESU, WATANZANIA WENYE NIANJEMA NA NCHI YETU TUSEME WOTE AMEN KUBWA.
 
Africa Kwa sasa inaongozwa na nguvu ya Mungu pekee, Na nchi za Africa zilizochagua kuongozwa na nguvu ya Mungu, ndio hazitatishika na Marekani Wala Umoja wa mataifa Kwa Sera zake za kukandamiza nji ndogondogo! Mungu kaamua kuingilia Kati, Yatosha kuonewa, Mungu ameskia kilio cha Watu wake Africa

Na wakileta mchezo kazi yetu ni kuwashitaki Kwa Mungu, watapigwa wachakae, Korona haitakwisha, Vimbunga vitadidimiza Aridhi zao

Matetemeko ya Aridhi hayatapoa,

Na sasa tumejipanga,Kila anayeonekana kuwa na seara za kibeberu, hawezi kupewa nchi aongoze, Atapuuzwa kama anavyopuuzwa huyu wetu!

Mungu Akiwa upande wetu ni Nani wa kutushitaki?

Mataifayote yenye mwelekeo wa Sera za kibeberu yatapigwa Kwa laana ya kibeberu

Tanzania haitapigwa Bani na mtu yeyote, na atakayejaribu, mapigo ya Mungu yaipiga nchi yake
MTU WA MUNGU, UBARIKIWE SANA MKUU. KUNA WATU HUMU LENGO NIKUONA NCHI INAINGIA KWENYE MATESO NA SHIDA ILI BEBERU ATIE MKONO WAKE, HAWATAFANIKIWA MILELE
 
Na Na Kagame na Mugabe hata yule wa Sudan akaondolewa juzi tu.
Kuna sehemu wapinzani wanakwama, kudhani hao jamaa huko ng'ambo wanajali Afrika kizalendo kweli. Wanancho angalia ni maslai yao, kama dikteta hahatarishi mishe zao hata atawale miaka 40 hawana shida naye.
 
Back
Top Bottom