CCM bado inaongozwa na Kizazi cha kwanza cha kisiasa na CHADEMA inaongozwa na Kizazi cha Tatu, lakini wanashindwa kuitumia Hiyo faida

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,891
141,824
Kizazi cha kwanza cha kisiasa kilihusisha Wanasiasa waliopigania Uhuru wa Nchi zetu mbili Tanganyika na Zanzibar na baadae kutuunganisha kuwa Nchi Moja

Kizazi cha pili kinahusisha Wanasiasa waliohudumu katika Mfumo wa CCM kikiwa Chama Pekee 1977 - 1992

Kizazi cha Tatu ndio hawa akina J J Mnyika, Zitto Kabwe, Dr Kigwangala, Halima Mdee, Dr Tulia nk....nk ambao wameanza Siasa ndani ya Mfumo wa vyama vingi

Sasa ukiiangalia CCM katika Uongozi wake bado inao Viongozi wa TANU na ukiwaangalia ACT Wazalendo bado wanao Viongozi wa ASP ndio hawa akina Steven Wassira, Lukuvi, Mkuchika, Mzee Duni Haji nk....nk

Chadema imekuwa na bahati ya kuwa na Viongozi wa Kizazi cha Tatu Hata Shujaa Magufuli ndio aliowapenda na kuwachukua kwa sababu Wana vibes za kileo

Hii ni faida kubwa sana kwa Chadema kwa sababu Vijana wao hawajarithi mivuto ya kisiasa kutoka kwa walezi wao wa Kizazi cha kwanza bali ni damu Mpya kwenye Siasa na Wapiga kura wa Chaguzi zijazo ni damu Mpya kwenye Siasa

CCM ina hazina ya Wazee lakini kwenye Dunia ya sasa mambo yanabadilika kwa kasi sana tunakoelekea uzee kwenye Siasa utakuwa siyo deal tena

Hili ni angalizo muhimu kwa CCM ili isibweteke, Sisi Wazee tuwaache Vijana watembee kwa miguu yao Wenyewe

J4 Ubarikiwe Sana!
 
Sahihi

Mana ninawatoto 7 hatahuyu mdogo wa mwisho Avodius hataki kusikia habari ya ccm na wote nimejitahidi wakoserikalini lakini Wap mama yao mwenyewe washampanga sikuhizi kilanikisema kuhusu ccm amekua akiguna tu ,ninahisi kunasumu tayari kapewa
 
Ccm ni chama cha kihafidhina..ni chama kisichokubali mabadiliko yawe ya ndani au ya nje..ndio mana ilichobakiza sasa ni kuiba kura kwa nguvu..na kupambana kuua upinzani.

Zama zimebadilika sana vijana wa sasa wanaiona ccm kama adui wao wa kwanza..siku wakiamua basi na iwe basi hakika ccm na viongozi wake watatafuta pakujificha.


#MaendeleoHayanaChama
 
Basi beba dumu la petrol nendanalo karikoo jimwagie Kisha jiwashe moto huku umeshika kilaza sauti ukielezea jinsi ulivyoguswa na lisu kushindwa uchaguzi 2020
 
Back
Top Bottom