Ingekuwaje KIFO cha mwanadamu kisingekuwepo?:-...
Hivi tu KIFO kipo, siku ya mazishi imekuwa kama sherehe, maselfie na pretenses kibao...
Hivi tu KIFO kipo, lakini kuna wanaokodishwa kulia ilihali wafiwa wanagonga whisky na Mvinyo.....
Utashangaa watu kujifanya tunamjali sana mtu akiwa marehemu kuliko akiwa hai,
Watu watagharamia mno kuwazika marehemu kuliko kuokoa maisha walipokuwa wahitaji....
Utastaajabu, watu hatusafiri kwenda kusalimia ndugu wanaoumwa, bali twasafiri wengi kwenda kuzika...
Kumbuka, ni nadra sana watu kukupa heshima ungali hai, lakini watapenda sana kukupa heshima za mwisho eti ukiwa kwenye jeneza..., PUMBAVU.
Halafu WEWE hujawahi kupewa ua na mtu yeyote tangu uzaliwe, lakini watalundika maua mengi mno juu ya kaburi lako... USHENZI!
Ukifa, watu watakupeleka msikitini au kanisani kwa lazima hata kama mwenyewe ulikuwa hapendi ibada kabisa.ulipokuwa hai..... Mmh, WANGEJUA!
Hatimae watasoma Historia FUPI" ya marehemu iliyoandikwa kwa uangalifu mno hata kama aliwahi kufungwa jela miaka kadhaa alipokuwa hai,haitaandikwa maana hiyo si historia, ila kama alienda semina ya siku 3 Ulaya, hiyo lazima iandikwe..
Halafu unaambiwa kuna watu wenye hadhi na watu wa kawaida!
MUNGU TAUSAIDIE.
Cha muhimu: Kila mtu atakufa, unaetembea kwenye kapeti nyekundu au udongo mwekundu, Utakufa. Utakayelazwa kwenye marumaru au udogo wa mboji, sote Tutakufa. Ahimidiwe Maulana.