muzi
JF-Expert Member
- Jun 17, 2016
- 1,048
- 1,479
TUFANYAYO KWA JINA LA UTAMADUNI.
1. Tunajali sana mtu akiwa marehemu kuliko akiwa hai.
2. Tunagharamia mno kuwazika marehemu kuliko kuokoa maisha yao walipokuwa wanaumwa.
3. Hatusafiri kwenda kumsalimia ndugu anayeumwa, bali twasafari wengi kwenda kumzika.
4. Ni nadra sana watu kukupa heshima ukiwa hai, lakini watapenda sana kukupa heshima za mwisho ukiwa kwenye Jeneza.
5. Wewe hujawahi kupewa ua na mtu, tangu uzaliwe, lakini ukifa watarundika maua mengi mno juu ya kaburi lako.
6. Utakesha msibani kwa jirani yako, kwa kuwa amefariki, ila hukuwahi kufika ndani kwake hata siku moja akiwa hai.
7. Ukiwa hai hakuna anayetaka kujua kijiji unachotokea, ila ukifa, watajaa kwenye magari wasindikize jeneza lenye mwili wa marehemu kuona kijiji hicho.
8. Tunamchukua marehemu kumpeleka Kanisani au msikitini kwa lazima hata kama mwenyewe alikuwa hapendi Ibada kabisa.
9. Ijapokuwa hamjaweka marumaru popote kwenye nyumba zenu, mnajichanga familia ili kujenga hilo kaburi la Marehemu.
10. Historia fupi ya marehemu huandikwa kwa uangalifu mno hata kama aliwahi kufungwa jela miaka kadhaa alipokuwa hai, haitaandikwa maana siyo historia, ila kama alienda semina ya siku 3 ulaya, hiyo lazima iandikwe.
Ndugu zangu, nawasihi tuwajali watu wakiwa hai kwanza, Mwili ndio ubebao Roho, na Roho ndiyo ibebayo uhai, Kumuacha mtu anateseka akiwa hai, akifa ndipo misaada ya mazishi sio vizur, mtu pengine hakuwahi kuona laki moja akiwa hai, lakini akifa inatolewa million 5 za kugharamikia mazishi, je kwanini hakupewa akiwa hai?
Ndugu zangu, je, mwili wafaa zaidi ya Roho?
Mwili haufai kitu, maneno hayo niliyowaambia ni Roho tena ni uzima.
*WENU KATIKA KRISTO.AHSANTENI.