Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,017
- 9,885
MFANYABIASHARA Salum Rajabu (51), mkazi wa Maili Moja Kibaha, mkoani Pwani, amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka mawili ikiwamo kujipatia fedha na kutakatisha Dola za Marekani 898,000.
Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka yake jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashidi Chaungu.
Wakili wa Serikali Esther Martin, alidai kuwa katika shtaka la kwanza kati ya Aprili 1 na 20, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, Mvomero mkoani Morogoro, na Lubumbashi nchini Congo, mshtakiwa akiwa raia wa Tanzania alijipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alijipatia Dola za Marekani kutoka kwa Segere Bushiri, Rocky Kungala na Paty Lufumada Dola za Marekani 898,000, baada ya kutakiwa kuziwasilisha nchini Tanzania kwa Albert Makendi Mayombo.
Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa tarehe na mahali pa tukio la kwanza, mshtakiwa alitakatisha Dola za Marekani 898,000 wakati akijua ni zao la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.
Martin alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu Chaungu alisema kesi hiyo itatajwa Julai 6, mwaka huu na mshtakiwa apelekwe mahabusu.
NIPASHE