Ashtakiwa kutakatisha Dola 898,000

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
MFANYABIASHARA Salum Rajabu (51), mkazi wa Maili Moja Kibaha, mkoani Pwani, amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka mawili ikiwamo kujipatia fedha na kutakatisha Dola za Marekani 898,000.

Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka yake jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashidi Chaungu.
Wakili wa Serikali Esther Martin, alidai kuwa katika shtaka la kwanza kati ya Aprili 1 na 20, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, Mvomero mkoani Morogoro, na Lubumbashi nchini Congo, mshtakiwa akiwa raia wa Tanzania alijipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alijipatia Dola za Marekani kutoka kwa Segere Bushiri, Rocky Kungala na Paty Lufumada Dola za Marekani 898,000, baada ya kutakiwa kuziwasilisha nchini Tanzania kwa Albert Makendi Mayombo.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa tarehe na mahali pa tukio la kwanza, mshtakiwa alitakatisha Dola za Marekani 898,000 wakati akijua ni zao la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Martin alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu Chaungu alisema kesi hiyo itatajwa Julai 6, mwaka huu na mshtakiwa apelekwe mahabusu.

NIPASHE
 
Dola 898,000!!

"Kwenye kesi yako tukijumlisha na hakimu tupo sita. Tunakuachia dola 100,000 iliyobaki tunagawana sisi ili kuua hii kesi, unaonaje?"

"Haina shida mzee we nisaidie tu"

No wonder TAKUKURU wako loaded.
 
Kisha potea kaishi kijijini kwenu kabisa....
 
Katakatisha!

Ivi hizi thamani za dola tunazobambikiwa nchini ndiyo thamani halisi ya wanakozitumia?

Maana niliona kwenye soko la samaki China bei ya samaki kamba ama konokono m1 wanauzwa $8 ama 10 ambapo tunavyobambikwa hapa ni lakimbili unusu, bei ya ng'ombe, yaani konokono anathanishwa na ng'ombe!

Maduka ya nguo Marekani shati la kawaida dola 15 hadi 20 yaani laki tatu shati la kuchomekea!

Je laki 9 hizo ukienda nazo Usa unaweza kutanua kinyama hadi kuheshimika kama hapa bongo?

Nani mjuzi wa kuthaminisha anitoe tongo tongo?

Ninaona kumtakatisha mtu kwa laki 9 haiingii akilini kutokana na kiwango hicho cha 'pesa ya mboga'
 
Dola 15 ni laki tatu? Ama kweli unabonge ta tongotongo unahitaji Mafuta taa kunawia uso
 
  • Thanks
Reactions: amu
Katakatisha!

Ivi hizi thamani za dola tunazobambikiwa nchini ndiyo thamani halisi ya wanakozitumia?

Maana niliona kwenye soko la samaki China bei ya samaki kamba ama konokono m1 wanauzwa $8 ama 10 ambapo tunavyobambikwa hapa ni lakimbili unusu, bei ya ng'ombe, yaani konokono anathanishwa na ng'ombe!

Maduka ya nguo Marekani shati la kawaida dola 15 hadi 20 yaani laki tatu shati la kuchomekea!

Je laki 9 hizo ukienda nazo Usa unaweza kutanua kinyama hadi kuheshimika kama hapa bongo?

Nani mjuzi wa kuthaminisha anitoe tongo tongo?

Ninaona kumtakatisha mtu kwa laki 9 haiingii akilini kutokana na kiwango hicho cha 'pesa ya mboga'
Duh.......ulienda hata USA kweli wewe??
 
Hebu nikufundishe hesabu mkuu, kubadili dola kuwa tsh ni hivi;
Mfano 1USD rate yake ni around 2300 Tsh.
Je, 15USD=?

Mpaka hapo hujaelewa tu mkuu?
Katakatisha!

Ivi hizi thamani za dola tunazobambikiwa nchini ndiyo thamani halisi ya wanakozitumia?

Maana niliona kwenye soko la samaki China bei ya samaki kamba ama konokono m1 wanauzwa $8 ama 10 ambapo tunavyobambikwa hapa ni lakimbili unusu, bei ya ng'ombe, yaani konokono anathanishwa na ng'ombe!

Maduka ya nguo Marekani shati la kawaida dola 15 hadi 20 yaani laki tatu shati la kuchomekea!

Je laki 9 hizo ukienda nazo Usa unaweza kutanua kinyama hadi kuheshimika kama hapa bongo?

Nani mjuzi wa kuthaminisha anitoe tongo tongo?

Ninaona kumtakatisha mtu kwa laki 9 haiingii akilini kutokana na kiwango hicho cha 'pesa ya mboga'
 
Umeona? Ndio maana wabeba boksi siku tunarudi huko, miji huchafuka.

Back
Top Bottom