Ashikwa Pabaya na Mwanamke Aliyezaa Naye

Ashikwa Pabaya na Mwanamke Aliyezaa Naye

JF2050

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Posts
2,085
Reaction score
45
Kuna Jamaa mmoja alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na msichana fulani ambaye walikuwa wakisoma pamoja O-level, form I-Iv. Katika uhusiano wao jamaa akawa amempa mimba yule dada.

Mwaka 2001 kuendea kufanya mtihani wa form IV, yule dada mimba ikawa imekua, kutokana na kelele za walimu kwamba ana mimba na sheria za wakati huo, binti ikabidi aache shule. Mwaka 2002 Dada wa watu akazaa.

Shule ilikuwa day. Baada ya mtihani wa form IV, jamaa akawa amerudi kwao (mbali kidogo na shule) kusubiria matokeo. Dada kwao ilikuwa karibu na shule waliyokuwa wakisoma. Dada akafanya juhudi ya kumtafuta jamaa kwa kumwandikia barua na kutumia watu kumjulisha kwamba amezaa mtoto na ni wake. Jamaa alipata ujumbe, lakini "aliruka mita mia" na kusema sijazaa naye, kwanza alikuwa na mahusiano na watu wengine, hiyo mimba sio yangu!

Dada wa watu kuona hivyo, akaamua kutulia akaanza kulea mtoto. Baadaye, jamaa akaenda shule form V. Dada akawaza, huyu jamaa alimkataa mtoto, huenda ilikuwa ni woga au mawazo ya kitoto, ngoja nimwandikie tena barua kumwambia ukweli ni kivipi mtoto ni wake, akamwandikia. Jamaa aliipata barua na aliijibu (Dada anadai anayo hiyo barua). Kitu kimojawapo alichoandika katika barua hiyo ni kwamba mtoto sio wake na asitajwe wala kuhusishwa mahali popote na swala la mtoto. Dada akasema basi, akaendelea kulea.

Mtoto akakua. Baadaye, alianza shule (Sasa yupo darasa la nne). Watu waliomwona mtoto wakawa wanamweleza jamaa, aisee mtoto ni wako wala haina ubishi kwani anafanana na wewe!

Jamaa akaanza kujishuku, dah anafanyaje sasa! Sijui aliwaza nini, akaanza kumtafuta huyo dada, anamwambia "ulisema mtoto ni wangu twende tukapime DNA ili nithibitishe". Dada akamwambia unaumwa! Usinisumbue wala sitaki kukuona, ukinifuata au kukaribia kwa namna yoyote kwa mtoto nakushtaki! Mtoto sio wako, mimba nilipewa na mpita njia, usinisumbue! (Dada anakuambia mtoto ni wake, alizaa na mtu hamjui, one 9t stand).

Jamaa kichwa kikastick! Lol!

Habari kwamba huyo mtoto ni wa jamaa zimeenea katika idadi kubwa ya watu na eneo na inajulikana kwamba alimtelekeza! Ngoma nzito zaidi ni hii:

Jamaa akaamua kuachana na dada ingawa moyo unamuuma sana, akatafuta mchumba - graduate amwoe. Yeye ana MS.

Mchumba: Haya background yako tafadhali,mahusiano yako ya nyuma, ulizaa, ulioa, una mtoto, blah blah?

Jamaa: Sijawahi kuoa sina mtoto.

Mchumba: Vilevile sijawahi kuolewa sijawahi kuzaa.

Namba 1.

Muda si muda mchumba katonywa, jamaa yako amezaa na mwanamke 2002 lakini alimktaa mtoto, yule wala huhitaji ushahidi anafanana naye - yaani ni carbon copy, kama vipi tukusaidie ukamwone kisirisiri! Baada ya mchumba kuhakiki, kamwambia jamaa bazazi mkubwa, kumbe umezaa, na mtoto umemkana, achana na mimi! Mchumba PTtuuuuuuuh huyo kwao.

Katafuta mchumba mwingine, yakajirudia yaleyale ya number 1. Wa tatu hivyohivyo!

Sasa jamaa akamuwakia yule dada aliyezaa naye: Inakuwaje unawaambia wachumba zangu mie nimezaa na wewe? Dada aliyezaa naye kamtukana, na kumwambia wachumba zako ndio kitu gani? Mie nawajua? Wananihusu? ------- kwenda zako bazazi mkubwa wee! Allah!

Jamaa nilisoma naye O-level hata mimi (hii sasa ni siri kwenu msimwambie). Dada aliyezaa naye ni jirani yangu! Tuna urafiki mzuri na familia yao, nikiwa nafanya kazi zangu nikichoka na kutaka kupiga story naenda kwao. Pia ikiwa nitapata shida yoyote bila shaka familia yao itahusika kwa kiasi kikubwa kunisaidia.

Jamaa kawaza, pia kapewa mawazo na watu mbalimbali kwamba tuma mtu anayefahamiana na kuelewana vizuri na huyo dada akasettle mambo! Akasema eeenhh, nimesikia Simplicity. ndio swahiba wake/wao mkubwa, ngoja nimwombe.

Akanipigia simu, ndugu yangu janga linalonihusu unalijua, naomba uongee na lara 1 (sio jina halisi) unisaidie kumaliza hii kesi (Hapa natumwa kama diplomat). Lengo langu ni akubali tukapime DNA ili kama mtoto ni wangu nilee na gharama zote nitamrudishia! Hata akisema m 30 mkuu nitampa! Lol!

Jamaa anashindwa kusema moja kwa moja mtoto ni wake ingawa ana uhakika kwa sababu si alimkataa! Kwa hiyo anataka kutumia gia ya kupima DNA kama ndio njia ya kujihalalishia.

Attempt one:

(Nimepewa kazi ujue): Nikamtoa dada kiwanja kikali, tukawa tunakunywa (sio pombe), tunakula, tunacheka tunagonga, kichwa kinaniambia anzisha mada. Baadaye, nikamwambia, dada yangu sikiliza: E bwana eehh Mshinga (sio jina halisi) amenituma anataka myamalize haya mambo! Kusikia hivyo alibadilika ghafla, akazoza, yaani wewe kunitoa kote huko hili ndio lilikuwa lengo lako! Kama huna kitu cha kuongea ni heri tunyamaze mpaka tutakaporudi nyumbani!

Nikadhani anatania, nikajaribu kurudia nilichomwambia kwa namna nyingine, akaniambia, naona hunijui, kama unataka uache kukanyaga kwetu, kwa maudhi utakayoyapata endelea! Huyu mtu alinitesa na kuniumiza sana. Sitaki kusikia chochote kinachohusiana na yeye! "Sitaki sitaki sitaki".

Nikajaribu kumbembeleza akaniambia kwa heri, nikadhani mchezo, dada huyooooooooooooooooooooooo, katembea.

Kiwanja kilikuwa kizuri pametulia washikaji fulani walikuwa wamekaa pembeni, duh walijua kwamba nilikuwa namtongoza, na binti amenichomoa live! Niliona aibu nikajilaumu nini hii sasa imenitokea! Washikaji wakawa wananipa pole. Ila nikasema hawa inabidi niwaeleze kisa, sio siku nyingine tunakutakana, wanaanza kuninyoshea kidole, kwamba jamaa alichomolewa na demu live bila chenga!

Ndugu zangu wana Jf, janga ndio hilo. Sijaenda kwao, nilimpigia simu mara 2 hakupokea, nimeona ngoja nimpe muda. Feedback kwa aliyenituma bado sijarudisha, namwambia tu subiri nipate muda nitamtafuta!

Mawazo yenu ndugu zangu ni muhimu ili kuokoa jahazi!
 
Last edited by a moderator:
Simplicity unatoa threads kama singles za Diamond.

Nimekuvulia kofia, ndugu/rafiki zako wana visa. khaa!!!!

Nami kuanzia kesho naanza kumwaga visa vya majirani. threads 10 kwa siku si mbaya sana.
 
Alimtenda jeuri mbaya sana, mwache akomage...manaume ya hivo yanaboa sana, mwache dada yangu arejeshe heshima yake
 
''Bwana kama wewe ungehesabu makosa nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha ili uogopwe''. Kuna mambo yanaudhi, yanakera na hayana uungwana ndani yake. Jamaa alifanya kosa kubwa. Lakini mtoto anastahiri haki ya kumjua baba yake na pengine malezi(upendo wa baba upo?). Namshauri mama wa mototo arudishe moyo nyuma. Leo ana uwezo wa kumzuia mtoto kesho atakuwa na maamuzi yake.
 
Haya na ukome na kiherehere cha kujitia u kofi anani. na dada aweke tu akili vizuri siku atakuta mtoto kajibeba kaenda kwa babae ni heri apoke mshiko aongezee mtaji au arudi class.
 
Da hizi mada nyingine ngumu aisee, yaani huwezi amini na kurudia kuisoma mara mbili wala hata hata sijajua hapa ushauri apewe nani kati yako, huyo bi dada, au huyo baba asiyejua nafasi yake.

Ila hata kama ni story ya kutunga ina ukweli mwingi sana ndani yake. Bro wangu mwenyewe ashawahi kukutana na inshu kama hii.
 
utakubali vp kibwegebwege?ebo! demu mwenyewe alikua anadandiwa na masela kibao ndio mana akamjb amepewa na mpitanjia.dna lazima hapo
 
utakubali vp kibwegebwege?ebo! demu mwenyewe alikua anadandiwa na masela kibao ndio mana akamjb amepewa na mpitanjia.dna lazima hapo

Kama roho yako inakwambia mtoto si wako DNA ya nini? Umemkataa mtoto, mama kaishakubaliana na hiyo hali kwa nini uendelee kusokola yasiyohusu.

Lara 1 U-LIBERAL ni mzuri jamani, unapata mimba unakaa kimya mpaka unajifungua mtu hajui, wala humuulizi maziwa nepi, nguo. Kimya kimya.
 
Hahahahahaaa!
Mwanaume umbea umekuzidi! Eti"... Itabidi niwape mchapo wale jamaa ili wasininyoshee vidole, kisa nimepigwa chini..!"
Wiki hii kunani? Wanaume kujivisha mapigo ya kike kile!!!!!
...
Sometimes Ukofi Anan haufai kabisaaa!
Sasa huyo ke kwa sasa anakuona SHANKUPE tu!!!!
 
yeah! pole kofi anani wakitaa, hapo bwana kwa hali iliyofikia sio suala la kutuma mtu ni issue ya wazee wa jamaa waende kuonana na wazee wa binti ndio muafaka unaweza kupatikana. ikiwa vipi ikiwa mshikajia anajiamini atie timu mwenyewe home kwa madingi wa bidada... mbona inawezekana!

mimi nina ushuhuda wa kwangu mwenyewe kama hivyo, lakini sikuwa na nyodo kama jamaa....
 
safi sana

Huyo dada aendelee hivyo hivyo

Dawa kwa mibazazi yote
 
Hapo inategemea na msimamo wa mtoto hapo baadae, lakini huyo mama angechukua tu hizo M30 afanye mambo yake sababu mtoto anaweza asiwe na msimamo ukubwani akamfuata baba yake. ila ninahistoria ya kweli baba mmoja alimkutaa mtoto hivyohivyo mtoto akakuwa akasomeshwa na wajomba baadae mama akafariki, yule baba alioa hakubahatika kupata mtoto na huyo mke wake. huyo kijana akapata kazi kubwa tu serikarini, yule baba kafilisika pia kazeeka hana mtoto ikabidi aanze kumuuomba msamaha mtoto wake na walikuwa wanafanana utafikiri photocopy yake, lakini mtoto alikuwa anakataa mimi sina baba, mama aliniambia sina baba na hata kama wewe ni baba angu labda kamuombe msamaha mama angu kaburini kwa kumtelekeza na kumuumiza, then waombe msamaha wajomba zangu walionisomesha, wao ndo wataniambia kuwa wewe ni baba yangu. alikuwa anatoa misaada sana pale kijijini kwao anampa na huyo baba ake halafu anamwambia nakusaidia kama mzee wa kijijini kwetu na sio baba.
 
' Lakini mtoto anastahiri haki ya kumjua baba yake na pengine malezi(upendo wa baba upo?).
je kama huyo baba ni marehemu ingekuwa ni lazima sana ,kama 2002 mpaka sasa hajamwona wala kumsaidia je huyo mtu anaumuhimu? sidhani kama ni muhimu kwa baba kama huyo to hell kabisa
 
Sasa yeye anamtaka mtoto tu mama hapana na wakat alimharibia mwenzake uschana anapenda vya kunyonga eeh!
 
Back
Top Bottom