Asasi za kiraia nchini , (azaki) zapongezwa na kupewa changamoto!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,711
114,034
Wanabodi,

17/06/2014 AZAKI ZAPONGEZWA NA KUPEWA CHANGAMOTO

Asasi za Kiraia nchini AZAKI, zimepongezwa kwa kazi nzuri ya utoaji elimu kwa umma wa Watanzania kuhusu masuala mbalimbali ya ya muhimu kwa jamii ikiwemo mchakato wa katiba mpya, lakini pia zimepewa changamoto kutafuta namna bora zaidi ya kuendesha kampeni zake mbalimbali kwa mtindo wa ushirikishwaji wa na kuheshimiana na mihimili mikuu ya dola ya Bunge, Serikali na Mahakama na sio kwa kunyoosheana vidole, kulaumiana, kulumbana au kushutumiana baina ya AZAKI na mihimili hiyo.

Pongezo na changamoto hiyo imetolewa na Naibu Spika wa Bunge la JMT, Mhe. Job Ndugai, wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Saba ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaliyoanza jana katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Naubu Spika Ndugai, amepongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na AZAKI kupitia The Foundation for Civil Societies, katika kuhamasisha shughuli mbalimbali za kimaendeleo kupitia maonyesho ya ZAKI Bungeni, kwa kuwawezesha wadau mbalimbali kukutana, kubadilishana uzoefu, kujifunza na kutafakari mambo mbalimbali kwa lengo la kuboresha maisha na kuleta maendeleo.

Ametoa changamoto kwa AZASI, kazi yao isiwe ni kusema tuu na kunyooshea serikali vidole kana kwamba kila kitu ni jukumu la serikali, bali AZAKI kama sehemu ya jamii ya Watanzania, pia zina wajibu mkubwa wa kuchangia maendeleo ya taifa kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo likiwemo Bunge.

Naibu Spika amesema na hapa ninamnukuu
“Uwepo wa Asasi za Kiraia ni muhimu kwa ukuaji wa demokrasia na utawala bora katika nchi yetu, hivyo nawapa changamoto ya kujitafakari namna bora zaidi ya kufikisha ujumbe kwa walengwa kwa lengo la kuimarisha mahusiano kati ya Wabunge na AZAKI, badala ya migongano.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi kufugua maonyesho hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maonyesho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa TACOSODE, Bibi Theofrida Kapinga, amesema kauli mbiu ya Maonyesho hayo ni “Majadiliano Makini baina ya AZAKI na Bunge ni Msingi Imara wa Maendeleo.” Imejikita katika mtazamo kwamba, mijadala yenye tija baina ya wabunge na wana AZAKI, ni nguzo muhimu na imara katika kuharakisha michakato ya maendeleo nchini kwa kuhakikisha mahusiano na mashirikiano hayo yanazidi kuimarika kwa maendeleo ya taifa.

Bibi Kapinga amesema wana AZAKI, wanafarijika sana kuona Bunge limetambua umuhimu wa AZAKI kwa kuwashirikisha katika mijadala mbalimbali, wa utungaji sera mfano, UKIMWI, MKUKUTA, GESI ASILI, , na mapitio ya miswaada ya Kodi ya Ongezeko la Thamani VAT, Usimamizi wa Kodi, na Muswada wa Fedha.

Maonyesho haya ya 7 ya AZAKI Bungeni, yatamalizika kesho yameratibiwa na TACOSODE kwa kushirikiana kwa karibu na Policy Forum, SIKIKA na HAKI ELIMU, na kufadhiliwa na The Foundation for Civil Society (FCS).
 

Attachments

  • DSC_0656.JPG
    DSC_0656.JPG
    294.6 KB · Views: 78
  • DSC_0661.JPG
    DSC_0661.JPG
    407.3 KB · Views: 60
  • DSC_0650.JPG
    DSC_0650.JPG
    429.5 KB · Views: 61
  • DSC_0641.JPG
    DSC_0641.JPG
    401.2 KB · Views: 59
  • DSC_0632.JPG
    DSC_0632.JPG
    501.5 KB · Views: 60
  • DSC_0623.JPG
    DSC_0623.JPG
    559.9 KB · Views: 63
  • DSC_0597.JPG
    DSC_0597.JPG
    340.4 KB · Views: 59
  • DSC_0605 copy.JPG
    DSC_0605 copy.JPG
    324.7 KB · Views: 54
  • DSC_0615.JPG
    DSC_0615.JPG
    681.4 KB · Views: 47
  • DSC_0677.JPG
    DSC_0677.JPG
    413.9 KB · Views: 61
Back
Top Bottom