Kupitia ukurasa wa LHRC wamechapisha taarifa hii;
Asasi za kiraia na watetezi wa haki za binadamu tuna jukumu kubwa katika jamii la kulinda na kutetea haki za binadamu, pamoja na kufuatilia masuala ya uwajibikaji na utawala bora.
Baada ya Tume iliyoundwa na Rais Samia Suluhu kuchunguza matukio yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 kutoa taarifa yake hadharani tarehe 23/04/2026, tumeona tuna wajibu wa kuichambua na kutoa taarifa fupi kwa umma juu ya uchambuzi wa awali wa taarifa hiyo.
Taarifa hii inalenga kuonesha mapungufu yaliyojitokeza katika ripoti hiyo, pamoja na kutoa mapendekezo ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa.
Pamoja na kwamba tangu awali hatukukubaliana na muundo wa Tume hii ambao haukuzingatia ushirikishwaji wa makundi yote ya kijamii na wataalamu wa kimataifa wenye uzoefu wa uchunguzi wa matukio ya aina hii bado tuna wajibu wa kuchambua taarifa hiyo, kubainisha mapungufu yake, na kutoa mapendekezo yetu.