Asanteni Vodacom kwa kurejesha salio langu..

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,220
2,000
Tarehe 28.12.2013 saa 1244 nilikuwa na salio la maongezi tshs 30337.79 na kifurushi cha 600mb kufika saa 1730 kuangalia salio ilikuwa Tshs 0.0 bado 0. Baada ya kuwasiliana na wahudumu wa Vodacom waliniambia niwapigie saa nne ya usiku kuwa wangekuwa na details za matumizi yangu, niliwapigia kama walivyoniambia wakaniambia pesa hiyo imetumika kwenye internet yaani 600Mb + Tshs30337.79 niliwaambia kwa muda huo mfupi sikuwa na matumizi ya kumaliza hata hiyo 600MB wakasema ngoja wafatilie tarehe 29.12.2013 nilipigiwa na wahudu mara mbili wote walirudi kitu kile kile ilipofika saa kumi na moja asubuhi niliwapigia tena wakaniambia watanipigia saa mbili asubuhi mpaka saa tano walikuwa hawajanipigia nikaamua kuwapigia wakaniambia niende voda shop ya karibu nilipoenda voda shop nikaambiwa hawana uwezo wa kufatilia matumizi ya data/internet nikapiga simu huduma kwa wateja nikajibiwa tatizo langu limeripotiwa litashughulikiwa baada ya dakika kama 20 dada mmoja(Yunis) akanipigia kutoka vodacom alionyesha anahasira kaniambia yaleyale kuwa matumizi ya pesa zangu yameishiakwenye internet kama vipi niende dar akanionyeshe matumizi yangu nikamwambia sawa nikienda dar nitafika ofisini kwake akanionyeshe, leo 31.12. nilipigiwa simu na watu wawili kutoka voda wakijaribu kunielewesha kuwa kuna software ziko on hata kama huzitumii hivyo wakaniomba nizizime, nikawaambia najua faida na hasara ya kuacha software zina run muda wote na ninajua matumizi yangu kwa siku haizidi 20MB hata zikiwa zina run iweje ndani ya saa tatu 600MB + 30337 ziishe wakaniambia wana shughulikia tatizo langu..
Kwenye majira ya saa sita nilipokea pesa/salio la maongezi kutoka vodacom na baadae nikapigiwa simu kuwa wamerejesha kwasababu baada ya bado yangu kuisha sikutumiwa meseji ya kuonyesha kuwa bando langu limekwisha.
Nitakuwa sijawatendea haki nisipo washukru namna mlivyo lishughulikia tatizo langu kwani mmenipigia simu zaidi ya mara nane(8) hii kwenye mitandao mingine ni adimu sana kwanza kupata huduma kwa watenja unaweza maliza hata siku mbili unawatafuta tu...

ASANTENI VODACOM
 

zindouna

JF-Expert Member
Aug 12, 2011
249
225
mimi sina hamu nao hao vodacom....wameswap line yangu wakanilamba hela zote kwenye account yangu ya benki...kuweni waangalafu mkiona line zenu haziko hewani muda mrefu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom