Asanteni Sana Maaskofu, Mmeishi Kwenye Ukweli Wa Neno la Mungu. Tunashukuru Kuusambaza Waraka Mpaka Ngazi ya Familia.

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,566
41,084
Tangu kale Mungu alipoumba Ulimwengu, na kisha mwanadamu, wanadamu walipewa haki yao ya kumiliki rasilimali zilizopo kwenye nchi z6ao. Kwenda kuvamia au kuiba kisicho kwenye ardhi yako, kulizaa mapigano.

Mungu alipomwumba mwanadamu, aliifanya ardhi kuwa ni urithi wake na vizazi vyake, na mgeni akija lazima afahamike ni mgeni, na kamwe hawezi kuwa juu ya warithi wa haki.

Tamko la Maaskofu limejaa upendo kwa wanadamu wa leo na wazao wetu. Maaskofu hawaombi kupewa bandari wala umiliki wowote. Kwa upande wa pili, wanaopigania urithi wetu uporwe na wageni, japo rushwa mara nyingi haina ushahidi, wamesukumwa na mapato yasiyo haki, mapato ya rushwa. Mapato yenye kuleta upofu wa akili, kifo cha dhamira na unafiki wa nafsi.

Maaskofu wamekuwa kama mfalme Sulemani, ambaye alipopewa na Mungu, nafasi ya kuomba chochote, hakuomba utajiri, hakuomba maisha marefu, bali aliomba hekima ya kuwahukumu watu kwa haki. Maaskofu hawajachagua lolote la kuwafaidisha wao binafsi, bali kuwanufaisha wananchi wa leo na watoto wetu, ilihali wao hawana watoto.

Watawala wamezuia vyombo vya habari kuandika habari zozote za waraka wa maaskofu, ikiwa ni pamoja na waraka wenyewe. Lakini haitapunguza chochote katika kuwafikia wananchi. Kama ujumbe wa Mungu ulienea Dunia nzima bila ya kuwepo magazeti, internet, mitandao, simu, TV wala redio, leo itashindikana nini ujumbe wa maaskofu kuwafikia watu wote wenye dhamira njema, wakati ambao tekinolojia za mawasiliano zimetapakaa?

Leo nimeenda ibadani, nimefurahi kuusikia waraka wa Maaskofu ukisomwa mbele ya waumini wote, na kila kila mwenyekiti wa jumuia ndogo ndogo akipewa nakala ya mkataba ili kila jumamosi wakati wa ibada, waumini wapate nafasi ya kutafakari ujumbe wa maaskofu, na juu ya hatima ya urithi wa Taifa letu.

Mungu aliye Baba wa hekima lakini hakimu mkuu, tunaomba akatoe hukumu dhidi ya wasioutakia mema urithi wa Taifa letu, sawasawa na uasi wao kwa nchi, kwa kadiri ya mapenzi yake.
 
Hakuna kitachobadilika, ndo kwanza wanasababisha ionekane ni chuki kati ya Waislamu na TEC

Sisi SDA ngoja tukae pembeni na popcorn
 
Hao ni wapinzani wa TEC hawataongea kotu
Usilete uwongo wako hapa. Hakuna upinzani wowote wala chuki. Wote wanamwabudu Yehova na Kristo Masiha wake Yesu Kristo.

Tena kila mwaka, maeneo mengi kuna ibada za pamoja, chini ya Umoja wa Makanisa.
 
Hakuna kitachobadilika, ndo kwanza wanasababisha ionekane ni chuki kati ya Waislamu na TEC

Sisi SDA ngoja tukae pembeni na popcorn
Unarukia kwenye vitu ambavyo huna uelewa navyo. Ni utaratibu wa kawaida, nyaraka zote za maaskofu, ni nyaraka za kichungaji. Nyaraka zote za kichungaji, iwe zimetolewa na maaskofu au Mama Kanisa, yaani Papa, ni lazima zisomwe mbele ya waumini wote wakati wa ibada
 
Unarukia kwenye vitu ambavyo huna uelewa navyo. Ni utaratibu wa kawaida, nyaraka zote za maaskofu, ni nyaraka za kichungaji. Nyaraka zote za kichungaji, iwe zimetolewa na maaskofu au Mama Kanisa, yaani Papa, ni lazima zisomwe mbele ya waumini wote wakati wa ibada
Ikiuma chomoa
 
Tec imekua taasisi ya ajabu kabisa badala ya kuhimiza maendeleo imekuwa msitari wa mbele kupinga maendeleo
 
Baada ya padre kiongozi wa ibada ya leo kumaliza kusoma waraka ule, umati wote wa waumini wamepiga makofi kwa kiwango ambacho sijawahi kushuhudia hapo kabla.

Tafsiri yake ni kwa kwamba wengi wa watanzania hawaipendi huu mkataba au makubaliano.
Hatukuwa tumearifiwa kwamba ratiba za leo kwenye ibada kutakuwepo na kusomwa kwa tamko kiasi cha watu kujiandaa, ilikua ni mshtukizo kwa wengi wetu ila taarifa imepokelewa kwa kwa shangwe na vigelegele vingi mno!
 
Back
Top Bottom