Asante sana Mwalimu Jael...

Asante sana Mwalimu Jael...

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,802
Reaction score
43,205
Habari za usiku tulivu, poleni kwa majonzi ya msiba wa Morogoro, sote njia yetu moja kila mmoja kwa muda na wakati wake, ajuaye lini ni Maulana pekee. Pole za dhati ziwafikie walioguswa na msiba huu, ndugu jamaa na marafiki.

Rejea kwenye lengo la uzi, Kasie mie siishi vijaruba..... Sijui nianzie wapi....

Mwalimu Jael, tumekuwa marafiki kitambo sana twasemeshana na kusimuliana yanayotusonga na tunatiana moyo. Wajua naongea sanaa hata siku ile ukaniuliza hujui ni mawili yepi kati ya niliyotaka kukwambia.

Okay, kwanza asante kwa kunipa ushawishi na uthubutu wa kushiriki mashindano ya swimming. Siku nyingi nilikuwa natamani kushiriki mashindano ila, tangu ile siku tumeongea ana kwa ana kwenye motokaa, ukanisimulia jinsi ulivyokusanya medali za swimming wakati uko masomoni (PhD) basi nikajikuta napata hamasa ya kuongeza mazoezi ya swimming na kila bonanza iliyotangazwa tangu pale nikawa nashiriki. Medali yangu ya kwanza ilinipa furaha sana nikajikuta nakufurahia wewe, hadi leo nina heng'a imejaa medali. Asante sana mwalimu Jael.
images (4).jpeg


Pili kuna bonanza moja tulienda wote, hili lilifanyika mji tofauti na tunaoishi hivyo ilitulazimu kuondoka alfajiri laah tulale huko. Nakumbuka sote hatukuridhia kulala kule hivyo tuliamka alfajiri na kuwahi bonanza. Kwa ukarimu na upendo, uliendesha maili zote zile pamoja na uchovu na kurudi pia uliendesha. Kasie nikawa kama chiriku naongea stories hii ikiisha naweka stori ingine.... Wala hukuchoka kunisikiliza wala hukuboreka....

Aiseeh, ulinifikirisha kwa upya, muda mwingi huwa naendesha mwenyewe nikiwa kwenye mishughuliko yangu, ila kwa ule mwendo mrefu akili yangu iliwaza mengi sana...

Mkeo atakuja kukufurahia sana iwapo ataona nilichokiona mimi... Mwanaume anayejali na kutekeleza ya kiume, hata akisema meno moja tuu natekeleza bila ubishi aahahahhaaa

Nakumbuka bonanza moja ulinihangaisha kukufanyia usajili hatimaye asubuhi tutakutana kwenye swimming pool yaani....
Ngoja nikunukuu, " nimeshakutumia hela unifanyie usajili, taarifa zangu ntazikuta asubuhi kwenye swimming pool... Daaah. Najaribu kukwambia mie mwenyewe nimebanwa sina namna ya kukufanyia usajili je nikikwama.... Unaniambia see you at the pool.... Daah Mwalimu Jael....

Leo sasa, aahahahahhaaa kweli wewe ni zaidi ya profesa, umenionesha kazi uliyoifanya nikakwambia naomba niletee sample ukajifanya kama hujanisoma heheheheh, akili ya Kasie ikasema, subiri nami naingia maabara. Nikakujibu mapigo kifaa kikatoka sawia sema kingine kiligoma ila nikafurahi sababu bila wewe nisingeingia maabara kufanya makaratee.

Mwalimu Jael, natumai utapita hapa. Nikisema umegusa maisha yangu na umeshiriki kubadilisha muonekano wangu natumai unanielewa. Isingekuwa kuongea na wewe, nisingefanya ambayo nimeyafanya....

Najua ratiba yako imekubana sana na unavipindi vingi sana hapo chuoni na project nyingi zinakusubiri wewe uandae proposal.

Sina cha kulipa wema wako, ukipata wasaa laah ukiwa likizo , nakupa ofa ya kushinda na bibi Kasinde siku nzima kuanzia asubuhi hadi baada ya mlo wa jioni ukiwa unarudi nyumbani kupumzika mie naenda kuyaruka majina... nisikuchoshe sana maana majukumu yako ni mengi. Utapokuwa tayari, nipo tayari (kwa gharama zangu).



When you are ready, am ready....

Alamsiki ticha Jael.

Kasie Matata.
 
Aisee katika vitu nimenyimwa sijui kuogelea nataman hata nijue tu


Ukitia nia na bidii na kuondoa woga wa maji, kuogelea ni rahisi kuliko hata kuendesha gari.

Tafuta mwalimu mzuri akufundishe, sio wale wa coco beach tafuta mwalimu professional.
 
Muazime mwalimu Jael...

Cc: @demiss
Ukitia nia na bidii na kuondoa woga wa maji, kuogelea ni rahisi kuliko hata kuendesha gari.

Tafuta mwalimu mzuri akufundishe, sio wale wa coco beach tafuta mwalimu professional.
 
Muazime mwalimu Jael...

Cc: @demiss


Hahahahahaa mie sio mchoyo huwa nashiriki vizuri na wenzangu, akiridhia ntampeleka kwa Ticha Jael amtichi kuogelea. shurti tuu aoneshe nia (kuna ile wanasema Mwalimu anakupa ujuzi wa asilimia 25, zilizobaki asilimia 75 ni wewe bidii yako kujisomea vitabu mbalimbali, mitandaoni na kufanya majaribio. Hivo ukitegemea mwalimu tuu bila bidii yako umefeli...) na awe mvumilivu maana ratiba ya Ticha Jael imebana mnoo.

Akiwa wa kukata tamaa mapema hatopata ujuzi anaoutaka.

Sitoacha kusema asante Mwalimu Jael
 
Mwalimu Jael kaanzisha njia, sasa mwingine anaendesha vizuuuuri bila kuuliza mjenzi wa njia nani


Hahahahahhaaaaa hata sivyo hivyo, hujaelewa kabisa.

Mwalimu Jael ona huyu kaingia chaka kabisa....

Mara nyingi huwa natizama tabasamu la mwalimu Jael sichoki wala sishibi....
 
Kasie mi ntakufundisha ku bet karbu


Looh mambo ya probability mie siyawezi na hesabu zake zilinishinda tangu skuli, wee beti ukipata tule wote ukiliwa utalala njaa hehehheeeee.
 
Ndio nimepata wivu

Usihofu, japo Ticha Jael yupo humu ndani, ila anayenimiliki fikra zangu, mawazo, hisia pamoja na kunikaza humu JF ni Dadii pekee.

To clear your doubt and answer your question; Hapana, Ticha Jael hajanikaza wala hanikazi.

Dadii is my one and only. I deeply love him, adores him, respect him and gave him space whenever he feels like he need one.

Bado una wivu au umekuisha!!?
 
Usihofu, japo Ticha Jael yupo humu ndani, ila anayenimiliki fikra zangu, mawazo, hisia pamoja na kunikaza humu JF ni Dadii pekee.

To clear your doubt and answer your question; Hapana, Ticha Jael hajanikaza wala hanikazi.

Dadii is my one and only. I deeply love him, adores him, respect him and gave him space whenever he feels like he need one.

Bado una wivu au umekuisha!!?
Umeniisha...ila nakutamani wewe sasa
 
Back
Top Bottom