Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,494
- 57,869
Leo kwenye pitapita zangu Mtandao wa X nimekutana na post aliyotuma Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema Bi. Brenda Rupia Jonas yenye clip ya maneno yaliyowqhi kusemwa na Viongozi mbalimbali (wa Vyombo vya Dola, Chama cha Mapinduzi na Serikali) kuhusiana na kukipendelea Chama cha Mapinduzi dhidi ya maamuzi ya Wananchi kupitia sanduku la kura na maneno ya Mwenyekiti wa Chadema akisisitiza kwa nini Wanataka Marekebisho ya Sheria za Uchaguzi na Katiba kabla ya Uchaguzi wa mwaka huu.
Kusema kweli napenda kuupongeza sana Uongozi wa Chadema kwa huu ubunifu. Kutengeneza short clips/ videos za namna hii ndo namna bora zaidi ya kufikisha ujumbe kwa watu wengi zaidi kwa wakati mmoja.
Dunia ya leo ni ya Sayansi na teknolojia. Watanzania wengi sasa Wanatumia Mitandao ya Kijamii kama njia ya kupata habari na kuhabarishana (Takwimu za TCRA zinasema wanaweza fikia Milioni 17 na zaidi). Clips hizi kusema kweli zinasambaza ujumbe wenu kwa haraka sana. Zinawafanya Watanzania wawaelewe kirahisi zaidi na kufanya Maamuzi sahihi.
Napenda kuwashauri pia tengenezeni clips za namna hii kuonesha mauaji ya Watanzania na Makada wenu yaliyofanywa na CCM na vyombo vyake vya dola kuwaeleza kwa nini ni muhimu Watanzania kuki support Chadema kwa hali na Mali ili kuongoza Mapambano ya Ukombozi.
Napenda kumaliza kwa kusema, Mungu yupo nanyi CHADEMA. Msirudi nyuma.