Asante Papii Kocha kwa wimbo huu!

Asante Papii Kocha kwa wimbo huu!

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
15,015
Reaction score
35,165
Wakuu,

Nakiri huu wimbo nimeanza kuusikia kwa Mara ya kwanza Jana,lakini kumbe una zaida ya mwaka mmoja ila sikuwahi kuusikia,labda kwakua hua si mfuatiliaji sana wa bongo fleva,kumbe aliimba msanii Papii Kocha baada ya kutoka gerezani ambako alikaa kwa muda wa miaka 13.

Ni moja ya nyimbo nzuri na yenye ujumbe wa kufika rohoni na kufariji sana.

Katika maisha tunapitia mengi magumu ambayo unaweza kudhani hakuna tumaini au Mungu amekuacha...hapana Mungu yupo na ameshaitika subiri kupata majibu yako.

Najua Papii Kocha alikata tamaa akajua labda Mungu hasikii kilio chake lakini Kumbe Mungu alishasikia kilio chake na alikua anasubiri muda ufike.

Usikate tamaa,Mungu daima hayupo mbali,anasikia kilio chako,endelea kumshukuru kwa kuwa chenye thamani zaidi ni uhai.

Baadhi ya mashairi;

"Mungu waambie ni wewe tu, ni wewe tu uliyesababisha Leo imefika

Waambie kila Siku ni zawadi,hakuna heshima inayozidi uhai

Hawapaswi kukata tamaa sababu daima haupo mbali"

Daima usikate tamaa,Kumbuka Papii Kocha na Baba yake walihukumiwa kifungo cha maisha na wanadamu lakini walipomlilia Mungu aliitika na hatimaye muda ulipowadia aliwafuta machozi.

Asante Papii Kocha,Mungu azidi kukulinda na kukufariji.

Mungu waambie
 
Nimeshindwa Ku-attach audio kutoka kwenye simu,anayeweza anisaidie kuuweka hapa.
 
Back
Top Bottom