Akiwa mgumu kwa kuota "ngaka" na makenya na sugu mikononi kitandani usilalamike ukaja kuanzisha thread hapa hawa viumbe Mungu hakuwaambia kuwa "mtakula kwa jasho"jasho ndio "suna" la kiume mke ni msaidizi tu na si zaidi sasa mke unakuta anafanya kazi za sulubu kama kugonga kokoto kufyatua matofali hawezi kuwa mke huyo!
Nimekupata vizuri sana, na wala sina cha kukupinga hata kidogo.
Ujue kuna kitu kimoja, ngoja nikuambie, ni hivi:-
Ujue kutokana na Mfumo/Mifumo ya Maisha tunayoishi imefanya baadhi ya Kazi zionekane kama si za Wanawake, au naweza sema Haziwafahi Wanawake.
Kwahiyo Mtu kama Mimi nikiona Mlimbwende anafanya Kazi zile ambazo tunazoziona kama hazifai kwa MALAIKA kuzifanya, ndicho kinachinifanya nijisikie raha zaidi/sana, ninapoona Mrembo anazifanya, anafanya.
Lakini mambo haya ni kwa Tamaduni zetu.
Nchi za Wenzetu zilizoendelea kuna Wanawake wanafanya Kazi za Kitaalam halafu za Shurba.
Unakuta Mtoto MTAMU yumo ndani ya nguo za Kazi, labda kapiga BAMBA juu na Chini, au yumo ndani ya Overall, halafu Mtoto ana Vitendea Kazi vyote, anakupigia Kazi kiustadi zaidi, halafu inakwenda na Muda, yaani habahatishi.
Sasa Sisi hizi Nchi zetu, Mwanamke akiendesha Basi la Abiria tunaona ni kitu cha ajabu sana