Asante Kikwete, hata bibi yangu anajua Ikulu yako imemsafisha Jairo!

KAMBOTA

Senior Member
Mar 21, 2011
176
103
IMG_1634.jpg

Na Nova Kambota,
Niliwahi kusema kuwa ingawaje ngwara na mtama husababisha mtu kudondoka chini bado ni ukweli ulio wazi kuwa ngwara na mtama ni tofauti anayebisha na abishe! Kuna tofauti kati ya mchafu na msafi, kwani kuna mpuuzi gani ulimwenguni humu ambaye ananunua sabuni ili aoshe nguo safi? HAKIKA MCHAFU ANAHITAJI KUSAFISHWA!
Ndiyo Ikulu yako mpendwa rais wangu Jakaya Kikwete imetumbukia kwenye “sifa kashfa” ya kumsafisha David Jairo eti magazeti yamepambwa na kichwa hiki “Ikulu Yamsafisha Jairo” . Pengine wewe mheshimiwa Kikwete unajisikiaje labda baada ya Ikulu yako kumsafisha Jairo? au Luhanjo anasema nini sasa?
“Silence means Yes” au? kama siyo kwanini basi Ikulu yako ipo kimya? Mpendwa rais wangu umeshiriki kumsafisha Jairo! mmmh! HONGERA SANA NASEMA TENA HONGERA SANA!
Msafi haitaji kusafishwa bali mchafu anahitaji……………………………kama Ikulu yako ilivyofanya! SAFI SANA RAIS WANGU! Tanzania itakukumbuka kwa mengi lakini la Ikulu Yako kumsafisha Jairo HAKIKA BIG UP RAIS WANGU.
Haya twende tu kwani mbona nimekuzoea hata jamaa zangu pale kijiweni eti wanakutania kuwa “umeshindwa kujivua gamba eti limeishia kiunoni” teh teh teh! mmh kazi sasa ipo kwa makamu wako kwenye chama “The Annointed Comrade Pius Msekwa ” duuh kwa yaliyovumbuliwa huko Ngorongoro kumbe na yeye ni gamba aisee! POLE SANA RAIS WANGU UMEZUNGUKWA NA MAGAMBA, what about you my prezda?
Nasema haya ooh tusije kulaumiana tu nakwambia rais wangu NARUDIA TENA usije kusema sijakupa pongezi kwa KUMSAFISHA JAIRO, ooh! nasema HONGERA SANA MJOMBA , lakini najaribu kuwaza juu ya uwezo wako wa kupambanua mambo rais wangu Kikwete, NAULIZA HIVIIII….Je unafahamu tofauti ya ngwara na mtama? je wewe kwa kumsafisha Jairo umejipiga nini? mtama au ngwara?…. SORRY RAIS WANGU NAWAZA TU KWA SAUTI LEO!

Nova Kambota Mwanaharakati,
Nipigie +255717 709618
Niandikie novakambota@gmail.com
Nitembelee
www.novakambota.com
27
August 2011, Saturday.
 
Kikwete Ameshindwa kuisoma jamii anaiongoza kuwa sasa imechange sio ile ya NYERERE, kwa hili anazidi kupoteza hako kajisifa kadogo alikokuwa amebaki nako,
SOMA MCHEZO
 
unajua kuna aina nyingi za kuongoza.
kama umewahi kufuga hawa wafuatao unaweza elewa ninachomaanisha. na mojawapo ni hizi
--------------------kuku huwatangulia vifaranga wake
--------------------Bata hutanguliza vifaranga wake
kwa hiyo kila mmoja anaweza tumia aina mojawapo ya uongozi anaoupendelea na kama unafaa kwa wakati husika, sehemu husika na jamii husika.
 
Back
Top Bottom