NTEGEYE Jr
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 322
- 286
Leo katika kipindi cha dakika 45 kilichoongozwa na Sam Mahela kwa ugeni wa Prof. Janabi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, nimejifunza mengi. Kwa dokezo la uchache wa niliyojifunza ni haya.
1. Kunywa Pombe nyingi kwa wakati mmoja, ni hatari kwa afya yako kwani husababisha Moyo kutanuka, Kumbuka Moyo ni Elastic kiasi ambacho siku moja utafikia UKOMO wa kutanuka zaidi ya size yake. Hapo ndio unasikia kifo cha ghafla.
2. Kitaalam, kama wewe ni Mnywaji wa pombe unatakiwa kunywa Pombe wastani wa chupa 2 tu kwa siku. Hata hivyo kila chupa, ichukue muda wa SAA 1. Mfano, kama unakaa KONA PUB au SAI SAI PUB masaa 2 basi unywe 2 tu.
LAKINI: Kwa wale wanaopenda kunywa pombe Kali kama Value, Whisk, Konyagi au GONGO ni hatari zaidi kwani ile inaenda kutanua moyo kwa nguvu. Kwa taarifa fupi tu ni kwamba, ukiona unakunywa pombe kwenye glass kidogo halafu unakunja SURA, basi ujue mwili unajaribu kukwambia kuwa "Kitu hicho hatari"
Kipindi cha Dk 45 kwa Prof. Janabi ni sehemu ya kwanza. Jumatatu wiki ijayo sehemu ya pili itaendelea.
MY TAKE: usiposikia kauli za wataalam, ukijiona wewe ni jeuri sana, mjanja sana na Jasiri zaidi utaisumbua familia yako itakukosa ghafla.
Natangulia JELA maana najua huo ni UCHOCHEZI