Asante Baba Askofu Mokiwa kwa kuanika unafiki wa sisi waumini

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,325
152,136
Nashukuru Askofu Mokiwa kwa kuanika unafiki wa sisi waumini tunaojidai kuguswa sana na imani zetu wakati ni wanafiki.

Nilileta mada inayofanana na anayoyasema Baba Askofu watu hapa wakanishambulia kwa kujifanya eti wamechukizwa sana na nilichokisema juu ya imani zao.

Ni ajabu sana tunaguswa na imani zetu kuliko matendo yetu.Naendelea kusisitiza ni bora wapagani kuliko sisi wenye dini tulioja unafiki wa kupitiliza mbele ya macho ya mwenyezi mungu.

Makonda nae kaja na yake!


Mokiwa-28Machi2016.png

Askofu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk. Valentino Mokiwa
Askofu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk. Valentino Mokiwa, ametaja majipu 10 yaliyoko makanisani na kuwataka Watanzania kujisafisha kwa kuacha mambo yasiyompendeza Mungu, ikiwamo migogoro ndani ya makanisa.


Askofu Mokiwa amesema ndani ya makanisa kuna mawe makubwa aliyoyafananisha na majipu ambayo hata Yesu Kristo anasononeshwa nayo.

Hayo aliyasema jana katika ibada ya Pasaka iliyoadhimishwa kitaifa katika Kanisa la Mtakatifu Albano, Upanga jijini Dar es Salaam.
Askofu Mokiwa alitaja jipu la kwanza kuwa ni uwapo wa mashindano makanisani, huku akisema siku hizi makanisa yanashindana kwa kuangalia kanisa lipi kubwa kuliko lingine na kanisa linamiliki shule ngapi.

Alisema: "Ushindani wa kanisa gani ni kubwa kuliko lingine, kanisa gani lina mali kuliko lingine, askofu anayeongoza kanisa fulani ni kabila fulani, na kanisa gani lina waumini wengi kuliko lingine na kanisa gani lina vituo vingi vya kulelea watoto yatima kuliko lingine.

“Imefika wakati sasa makanisa yajitathmini na kuanza kupunguza kuzungumza mambo ya nje ya kijamii na badala yake waelekezane uovu unaopatikana ndani ya makanisa,” alisema.

Jipu lingine alilitaja kuwa ni maaskofu kupigana vita. Alisema kuna tabia ya askofu mmoja kumchimba askofu mwingine, kupanga mapinduzi dhidi ya askofu mwenzake, pamoja kutukanana.

Alisema kuna tabia ya askofu kuacha eneo lake na kuingia katika eneo la askofu mwingine na kusababisha misuguano.

Jipu lingine alisema ni mapinduzi ndani ya makanisa, kuwa kuna ugumu wa moyo na kusalimiana kwa badhi ya waumini wa makanisa na kwamba waumini siku hizi wanasemana na kusingiziana, hivyo kumekuwapo kwa uongo ndani ya taasisi hizo ambazo dhima yake ni kuleta amani na furaha miongoni mwa waumuni.

Askofu Mokiwa alitaja tatizo lingine kuwa ni chuki baina ya waumini, huku watu wakiwa hawasalimiani na hawapendani, jambo ambalo hata askofu anapojaribu kuwaita na kuwapatanisha, wanakimbia kwa kutoa udhuru.

Alisema jipu lingine ni uwapo wa nguvu ya pesa kanisani au nguvu ya mtu ndani ya kanisa, ambayo inasababisha kuvurugika kwa kanisa.

Askofu Mokiwa alisema: "Kuna watu makanisani wanatumia pesa kwa manufaa yao wenyewe. Mbona hujitolei kusaidia watoto yatima? Mbona hujitolei kuwasaidi kikundi cha uinjilisti kwenda kuhubiri? Watu wa namna hiyo wana lengo la kuvunja amani."
Alitaja jipu lingine kuwa ni wizi na ulaghai na kwamba katika makanisa kuna ulaghai uliokithiri.

Jipu lingine alisema kuwa ni uwapo wa roho ya uchochezi kwa baadhi ya waumini makanisani, huku pia akitaja uwapo wa injili za kibiashara kwa baadhi ya makanisa kutumia injili kujiingizia kipato kwa kufanya miujiza.

Askofu Mokiwa alisema jipu lingine ni uwapo wa wivu na uzushi ndani ya makanisa.

“Siku hizi hayo mambo yanaitwa majipu ambayo yanasababisha kanisa kushindwa kuendelea, wakristo wanashindwa kumwona Mungu kwa sababu kuna watu waliotofauti ndani ya makanisa,” alisema Mokiwa.

MAKONDA: ATAKAYEOMBA ULINZI KANISANI KUSWEKWA NDANI
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika ibada hiyo aliliomba kanisa kumsaidia kutimiza wajibu wake kwa kunyoosha mienendo ya waumini wake, huku akitumia nafasi hiyo kusisitiza agizo lake la kuwataka wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhakiki silaha zao ndani ya siku 90.

“Kuanzia Julai Mosi, mwaka huu mimi mwenyewe nitaongoza msako wa kukagua silaha ambazo hazijahakikiwa. Sitakuwa na huruma, wala sitamwangalia mtu usoni,” alisema Makonda.

Makonda alisema kwa sasa jiji la Dar es Salaam haliko salama kutokana uwapo wa silaha ambazo hazieleweki.

Aliwaomba waumini wa Kikristo, ambao jana walikuwa wanaadhimisha Sikukuu ya Pasaka, kujitolea kuchangia maendeleo ya mkoa ikiwa ni pamoja na kumaliza tatizo la madawati.

“Juzi kuna mama mmoja Kimara, ni kiongozi wa kanisa, anasema kuna shughuli kanisani, anaomba ulinzi. Nikamuuliza wa nini, akasema unajua huku kuna rushwa. Nikashangaa kusikia eti kanisani napo kuna rushwa, hadi leo siamini. Sasa nasema yeyote atakayepiga simu kuomba ulinzi wa polisi kanisani namweka ndani,” alisema Makonda.

CHANZO: NIPASHE
 
Kuna wengine nimewahi kuwaambia maneno hayo, nilitukanwa sana nikajuta kwanini nimewaambia. Wadada waimba kwaya ambao wamenizoea wakanitolea maneno mabaya sana. Nikatulia moyoni, sasa wananiheshimu kwa ukimya wangu maana walijua nitawapiga na wala sikuwafanya lolote zaidi ya kuwaambia ukweli ndio huo.
WEWE MTOA MADA; mimi huwa sisomagi magazeti ya uhuru, nakuomba uniambie aliyoyasema huyo askofu ili na mimi nipone kwa kiwango changu. Waumini wengi wa kilokole ni wasikilizaji wa neno wala si watendaji wa neno!
 
Hahahaha.....

Leo umeliamini na kulisoma gazeti la UHURU?

Kweli wakati mwingine tuwe tunaweka akiba ya maneno jamani..
 
Ndiyo kwanza leo unajuwa kuwa mu wanafik?

Mbona mnajulikana enzi na enzi na wale walioukataa huo unafiki wa makanisani leo hii ndiyo waitwao Waislam.
Shida unarukia mazungumzo ya ndani. Hata masheikh kila siku wanakemea una afiki Kati ya waislam. Huwezi kosa kondoo wa sio wa kundi fulani. Its funny wewe ndio una tumia km sababu ya kuamini dini yako. Uta umia sana.
 
Unafiki mbaya.

Kuna watu hawanywi pombe lakini wazinzi kila siku hawakosekani kwenye nyumba za ibada na wao wanawaona walevi ndio kwenye dhambi.

Kuna wanasiasa wanaiba fedha za wananchi halafu wanafanya harambee kuchangia nyumba za ibada huo ni unafiki mkubwa.
Pia kuna unafiki wa Chadema kumuita Lowasa fisadi halafu akawa mtu safi baada ya kuwa mgombea wao wa urais.
Unafiki haufai .
 
Wale wote wenye kupuuza ndiyo leo wamebaki katika unafik wa kanisa.

Kwenye uislamu hakuna waumini ambao ni wanafiki wote mpo safi? Wote wanaoitwa waislamu wanatenda kwa asilimia 100 mafundisho ya uislamu?

Huo ndio unafiki wenyewe ,hapo utakuwa unajidanganya mwenyewe.
 
Nashukuru Askofu Mokiwa kwa kuanika unafiki wa sisi waumini tunaojidai kuguswa sana na imani zetu wakati ni wanafiki.

Nilileta mada inayofanana na anayoyasema Askofu watu hapa wakanishambulia kwa kujifanya eti wamechukizwa sana na nilichokisema juu ya matendo yetu.

Ni ajabu sana tunaguswa na imani zetu kuliko matendo yetu.Naendelea kusisitiza ni bora wapagani kuliko sisi wenye dini tulioja unafiki wa kupitiliza mbele ya mwenyezi mungu.

Makonda nae kaje na yake!

20160328_044834.jpg
==TULIOJA unafiki?
==Makonda naye KEJA na yake?
Naona umeishi sana somalia hivyo kusahau lugha ya kiswahili
 
Nashukuru Askofu Mokiwa kwa kuanika unafiki wa sisi waumini tunaojidai kuguswa sana na imani zetu wakati ni wanafiki.

Nilileta mada inayofanana na anayoyasema Askofu watu hapa wakanishambulia kwa kujifanya eti wamechukizwa sana na nilichokisema juu ya matendo yetu.

Ni ajabu sana tunaguswa na imani zetu kuliko matendo yetu.Naendelea kusisitiza ni bora wapagani kuliko sisi wenye dini tulioja unafiki wa kupitiliza mbele ya mwenyezi mungu.

Makonda nae kaje na yake!

20160328_044834.jpg
nakubaliana na baba askofu lakini nimekwazwa sana na chanzo cha habari hii , gazeti la uhuru linaendeshwa kwa ruzuku ( sijui ya serikali au ya ccm ) , ni gazeti ambalo linaendeshwa kwa hasara miaka yote , limechukua hela nyingi ambazo zingeweza kununua madawati kadhaa , nakiri hadharani kwamba silipendi na wala siliamini .
 
Back
Top Bottom