Asante A-G Werema kwa kuturejeshea Tanganyika yetu

Asante A-G Werema kwa kuturejeshea Tanganyika yetu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,006
CCM hatuna tena sababu za kupinga kurudi kwa Tanganyika. CCM hatuna haja tena ya kupinga Serikali tatu. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Mwita Werema amenena.Amenena kwa ufupi lakini katika ujumbe mkubwa sana. Ya kwamba, Dodoma ni Tanganyika na si Zanzibar. Tumemsikia akimwambia Mbunge Habib Mnyaa "kaulize huko huko kwenu Zanzibar.....hapa kwetu".

Haya si maneno ya mzaha. Haya si maneno ya kuyapuuza. Aliyeyasema;alipoyasemea;na alichomaanisha ni vitu 'serious' sana. Mwanasheria Mkuu wa nchi amesema...mnataka aseme nani tena kurudi wka Tanganyika? Ni huyu huyu Werema ndiye aliyedai mwanzoni kabisa kuwa Tanzania haihitaji Katiba mpya. Sasa anaitaka na Tanganyika.Yuko kinyume na CCM yetu.Yuko kinyume na Serikali mbili.

Jaji Werema lakini ni mbaguzi na aliyejaa kiburi cha madaraka. Hata kama kutakuwa na Serikali tatu kama anavyotaka,bado Wazanzibari wataendelea kuwa ndugu zetu. Halafu, ina maan Jaji Werema hajui kuwa Dodoma kuna Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Mambo ya kwenu na kwetu yanatoka wapi? Asante A-G Werema kwa kuirejesha Tanganyika lakini ubaguzi haufai.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Huyu WEREMA sijui ni ushamba au ndo Cheo kimemlevya... Yuko arrogant sana... Kwa kweli jinsi anavyojibu maswali huwa anakera maana dharau na kiburi imemjaa..

Nitashangaa Sana Wazanzibar wengine wakizidi kumkumbatia... Huu Muungano ulishakufa na kama walivyosema Jini lake limeshatoka kwenye chupa haliwezi kurudi
 
Hoja aliyokuwa anaiwasilisha Mnyaa ilikuwa mahsusi kwa Zanzibar na ndo maana akaambiwa akaulize huko kwao
 
Safi sana CCM wnyw wanajua muungano hauna manufaa siku wakiwa wapinzani nao watataka serikali tatu sababu kiukweli ndo mfumo unaofaa ila sahv wanajitoa sense kwa uroho wao wa kutaka posho mbili mbili
 
lazma hapa Werema atakua amesema lililo mioyoni mwa wanaccm wengi,maana jambo likiwa moyoni na akilini,kuna wakati unajikuta ukilisema au kulitenda bila wewe kujijua
 
Hata kama mtu ataomba radhi moyoni ukweli ni kwamba Tanganyika Yupo Mlangoni Anakuja
 
yule kula kulala mtoto wa malechela le totoz mbona hujamtag uzi huu?

Le Mutuz ni mpiganaji jamani acheni kumsingizia eti kula kulala, ametafuta maisha miaka karibia 30 nje huko na hapa bongo si anaishi kwake sio kwa mzee Tinga tinga.
 
kati ya watu ambao huwa siwakubali ni huyu werema maana anajibu watu kama vile wengine ni choo aisee yaani full majigambo na dharau nadhani cheo kimemlewesha sana aisee
 
Tanganyika tulishaizika kitambo. Mnataka kufufua marehemu?

Hata Eritrea ilizikwa ikafufuka, na pia si unakumbuka USSR?? Ni mataifa mangali yalizikwa na bado yakafufuka?? Ndugu, hatuhitaji sana kutumia nguvu kwa jambo hili. Hatuijui kesho, na hapo ndipo Mwenyezi Mungu ametufumba!.]

Hujui vizazi vinavyokuja vitakuwa na akili gani na maono gani!

ccUfisadi Sipendi
 
Back
Top Bottom