CCM hatuna tena sababu za kupinga kurudi kwa Tanganyika. CCM hatuna haja tena ya kupinga Serikali tatu. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Mwita Werema amenena.Amenena kwa ufupi lakini katika ujumbe mkubwa sana. Ya kwamba, Dodoma ni Tanganyika na si Zanzibar. Tumemsikia akimwambia Mbunge Habib Mnyaa "kaulize huko huko kwenu Zanzibar.....hapa kwetu".
Haya si maneno ya mzaha. Haya si maneno ya kuyapuuza. Aliyeyasema;alipoyasemea;na alichomaanisha ni vitu 'serious' sana. Mwanasheria Mkuu wa nchi amesema...mnataka aseme nani tena kurudi wka Tanganyika? Ni huyu huyu Werema ndiye aliyedai mwanzoni kabisa kuwa Tanzania haihitaji Katiba mpya. Sasa anaitaka na Tanganyika.Yuko kinyume na CCM yetu.Yuko kinyume na Serikali mbili.
Jaji Werema lakini ni mbaguzi na aliyejaa kiburi cha madaraka. Hata kama kutakuwa na Serikali tatu kama anavyotaka,bado Wazanzibari wataendelea kuwa ndugu zetu. Halafu, ina maan Jaji Werema hajui kuwa Dodoma kuna Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Mambo ya kwenu na kwetu yanatoka wapi? Asante A-G Werema kwa kuirejesha Tanganyika lakini ubaguzi haufai.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam