Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 76,662
- 161,660
Wewe ndiye asali wangu wa moyo
Kwa dhiki na faraja mpenzi kaza roho
Ingawa watasema mengi midomoni mwao
Usiwajali hao!!
Verse 1
Hizi tenzi madhubi kalili thabiti mahususi
Kwako mpenzi swali liko wazi toka enzi
Sio siri tena sibabaiki 'aeiou' hapana
Sina kigugumizi tena domo sio gundi tena
kinywa chepesi murua laini
maridadi kabisa maneno natema
uuhfh!! haaah nashusha pumzi na hema
Mwana wa kahena nimekufa kimahaba
Unanichanganya kimahaba
unanichanganya kwa mambo mengi kisura
kiumbo mshobo kama mpaka uroda
Najua wanakutazama kwa jicho la husda dada
Mtoto kichugwa kipoda tena bombaa
Ni wao tu roho zao za choyo wewe ndio asali wa moyo
Sintojali waniite zoba nimerogwa ama poyoyo
Wanataka kuzua mkumumba na jakamoyo
Hutu tuneno tudogodogo tusikupe
shaka sana twende bega kwa bega
Kama samaki na maji
Mizizi na ardhi tuzidi kuwachanganya.
kiitikio
Verse 2
Ewe ndiwe asali wa moyo wangu
Wanyuma yako wote nawaona machangu
Kwangu kwangu nakupa shahada yauvumilivu
Kwa wako utulivu sogea na utulize zetu mbivu
Woow! honey crazy! i cant bealive
Nilipoanza kukutokea kukufukuzia
Wanaa walianza kupaka tena kukandia
aaah! hawezi kung'oa mtoto high class
Yaani mgumu kama kisiki hang'oleki hata kwa leki
kwanza hali yangu duni halafu nikijicheki
sina 'Usponi town' kwetu
chai rangi vitumbu andazi
Nyumba mbavu za mbwa aliye nje anatuona waziwazi
Wakati shori kwao mambo ya mshiko , midikodiko
Chai ziwa juice passion,embe miwa 'rost' maini
tambi,kolonya, laini laini shata shata
nini shaka na vyapati vyapati
Aaaaha eti ningempata wapi?
Mh!! iwe bojo kaisii nikwenda muno
Akanana kange ninkashaha engozi
wanga wameuwawa mtaani
ngebe zimezimwa mchuchu
Kuvinjari nami
Kila tozi atakae mtokea anamuona kama Osami
Unajua wengi hawajui maana ya kupenda
Unajuwa wengine wanaona uchafu hata kulamba denda
Unajua wengine wanaona hofu kukashifiwa kwa kuwatokea watoto
wa matajiri au uwoga wa kupigwa kalenda
Na wangejua mapenzi hayachagui fukara wala
mtawala,dini, kabila desturi mila mradi
mmependana kama na B wangu tumeshibana
Rudia Kiitikio