Asali ni zaidi ya utajiri

Nawasalimu wakubwa kwa wadogo ktk jukwaa hili,
Kuna kipindi nilileta uzi kuuliza mazingira ya Tabora yalivyo kwani mke wangu alipangiwa kazi mkoa huo,mwaka jana mwezi wa 12 nilienda kumtembelea kipenzi changu wilayani sikonge kijiji sitotaja kwa ajili ya kuficha uhalisia wangu,naweza kufahamika mapema kwa watu waliomo humu na wanaishi kule.

Nilipokua kule kuna watu waliniagiza ASALI mbichi kama 3 hivi,hivyo nilipokaribia kuondoka niliamua kutafuta kwa wenyeji wa pale,nilitaka kununua ambayo imechujwa lkn kuna mdau akanmbia ninunue ambayo haijachujwa kwani inauzwa shlingi 80000 kwa ndoo ya lita 20,ambayo ukiichuja inatoa asali lita 10 iliyochujwa na safi kwa matumi.

Nilinunua ndoo mbili kwa shilingi 160000,ili nikitegemea nichuje nipate lita 20 niwapelkee wadau walioniagiza,ajbu kwenye ndoo hizo mbili nilipata lita kama 28 hivi badala ya 20 ikawa faida kwangu,ktk zile ndoo mbili yale makapi(masega) nilipata kama ndoo moja iliyojaa ya lita 20,ambayo nayo ni dili make wanayauza kwa kilo moja shilingi 3000,lakini ukiyapika unapa NTA kama kilo 3 hivi,ambayo kwa kule kilo ya NTA ni 10000/12000 hivyo kwa kilo 3 ni 30000.

UTAJIRI ULIPPO-
Katika uchunguzi wangu ASALI kule inavunwa kwa wingi mwezi wa 6/7 ambapo ndoo ya lita 20 inauzwa mpaka 40000/35000 kwa ndoo moja,na inapanda bei kuanzia mwezi wa 10 nakuendelea mpaka wa 3/4/5 wanapoanza kuvuna tena, mimi nimenunua asali kipindi ambacho imepanda bei.

NAENDELEA HAPA..
Sasa kama unamtaji nenda tabora mwezi wa 6au 7 tafuta sehemu wanazovuna asali,kipindi hicho utanunua kwa 40000 mpaka 35000 kwa ndoo ya lita 20, na nzuri nunua ambayo haijachujwa kabisa ndio faida zaidi,tafuta sehemu au chumba cha kupanga chenye ukubwa wa kutosha kutegemea na kiasi unachohitaji,kule vyumba bado bei nafuu sana vya kupanga kwa mwezi haizidi 20000,lipia miezi mitano au sita then chukua ndoo zako za asali paki humo nenda kaendelee na shuguli zako.

Iikifika mwezi wa kumi mpaka kumi na moja nenda kauze pale pale asali yako ndoo moja kwa shilingi 80000 na zaidi,wala usihangaike kutafuta soko lilipo,miezi hiyo kule asali hakuna na inapatikana kwa shida kweli kweli,wanunuzi wapo wakutosha 24/7hrs,wanakutafuta wewe,sio wewe kuwatafuta.
Kama pia unaweza na unasoko tofauti na kuuza kule basi fatilia maliasili wakupe utaratibu wa nini cha kufanya kusafirisha asali.

Kwa maana ukiweka mtaji wa 2m baada ya miezi 4 unapata 4m,ukiweka 5m baada ya miezi hiyo ni 10m,kwa maana kua unanunua asali kwa 40000 kwa ndoo,then unakuja kuuza kwa 80000 kwa ndoo ni mara mbili ya ulichokiweka.
Ukiamua kuchuja mwenyewe kuna faida zaidi kwan yale makapi unatengeneza NTA kwa kuipika utauza 10000 kwa kilo moja.

NJIA NYINGINGINE..
Tafuta pori kule kodi au nunua kwani bado kule ni bei nafuu,unaweza kupata pori hata kwa laki tatu mpaka tano kutegemea na ukubwa na mtu anaekuuzia,chonga mizinga yako ambayo unauwezo nayo,kule mizinga wanachonga kwa 2000 pamoja na kupandisha juu ya miti,hivyo ukichonga mizinga 1000 x kuchonga na kupandisha 2000=2,000,000 jumla kwa idadi ya mizinga 1000.
Ikumbukwe kua mzinga mmoja kwa miezi tajwa hapo juu unaweza kuta kila mzinga unatoa ndoo moja ya asali ambayo haijachujwa,hivyo kwa kipindi cha mwezi wa 3 mpaka 6 kuna maua ambayo nyuki hupendelea kuyatumia ndio msimu wake wa kustawi hivyo uzalishaji unakua mkubwa tofautisha na miezi mingine.

Basi tufanye umehangaika wee ukapata ndoo zako 400 badala ya ndoo 1000,na hii ni makadirio ya chini kabisa na haiwezi kua hivyo hata ukose vipi make nikipindi ambacho uzalishaji ni mkubwa sana kule, chukua hizo ndoo 400 tunza,njoo uza mwezi wa 10/11 kwa 80,000 kila ndoo.hivyo ndoo 400 x 80,000=32,000,000m.

Ukisafirisha unaweza kupata zaidi ya hapo,mimi ndio nimeanza kufanya hivyo sio mjuzi sana bado najifunza,nikivuna ntaleta mlejesho nini kimetokea.

SIKU NJEMA KWENU WOTE.
Mkuu uko sahihi.
Mimi nimeoa Tabora mke wangu pia alinipa maelezo Kama yako kuhusu asali.
Kwa hyo huu mwaka nataka kujikita kwenye biashara ya asali ila bado sijapata muda wa kufanya research Zaid.
Yaani itakuwa nikipata hela naziingiza kwenye asali tu,sipendi biashara za mahindi na mpunga.
 
Ubarikiwe kiongoxi
 
hapana soko lipo sana tu hasa dar...tena ya sumbawanga ndo dili sana .kuna mchiz ana hela balaa yy anauza asali tu anaitoa sumbawanga...
Habari kiongozi,kwa Hapo dar soko la asali naweza kulipata wapi?hata mimi asali ninayo ya kutoka karagwe na Bukoba.Please Nahitaji kupata contact za mnunuzi direct.Tuwasiliane 0767440210.
 
Natamani Sana kuleta asali SA lakini vigezo na masharti ya export hapo Tanzania kwa mjasiriamali mdogo ni kama tu vya kwenda mbinguni.

Ni kwweli hata huyo dogo anaefanya export nya asali membe bdo alimshika mkono.hv hv ngumj sana..
 
Mheshimiwa mm sijaelewa hapa kwenye

-Kutengeneza mizinga ni 2000. Je hii ni mizinga ya aina gani aisee na material ni nini?isijekuwa mizinga ya mabua.
-Huku kuchuja asali ni kazi nyepesi kiasi hiki unachotuaminisha na uweze kupata asali safi laini kabisa?

Mengine nimeyaelewa.
 
Kule mizinga ya kisasa bado haijafika Lkn wanasema nibora zaid sababu baadhi ya sehem ipo,kuchuja asali kule wanachuja kienyeji na ni asali nzuri na bora kabisa,iyo laini unayosema inakua imechakachuliwa (imepikwa),asali og ni nzito
 
Nashukuru kwa kuniunga mkono kwa hili nilsemalo,mimi nilienda na nikajionea na hapa najipanga kurudi[/QUOTE]
 
[/]Mkuu vp ushawahi kufundishwa namna ya kuitambua asali og na iliyokwisha chakachuliwa?

Hebu tuelimishe hapa
Chukua glass ya maji weka maji kiasi then chukua asali mimina kidogo kwenye glass,kama haijachakachuliwa itashuka chini bila kujichanganya na maji na itajitenga kabisa,kama imechakachuliwa inajichanganya na maji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom