ARUSHA: Watu wawili wafariki kwa kuchomwa moto bila nyumba kuungua

Watu wawili wamefariki dunia Leo hii asubuhi katika nyumba ya marehemu bilionea Msuya baada ya moja ya chumba walichokuwa kuungua Moto huku mwanaume hiyo akiwa amefungwa kamba mikononi.

Tayari polisi wamechukua miili sasa hivi baada ya kuchukua maelezo kutoka kwa wapangaji wengine.

Hili tukio limetokea katika moja ya nyumba yake iliyopo Sakina Arusha.

----------
Eng Mose, said

Watu 2 wa jinsia ya kike na Kiume ambao bado majina yao hayajatambulika wamekutwa wamepoteza maisha katika Kitongoji cha Elkiurei Kata ya Kiranyi wilayani Arumeru kwa kile kinachosemekana kuwa ni ajali ya moto.

Akithibitisha tukio hilo mwenyekiti wa kitongoji hicho Bwana Enesphori Chami amesema kuwa tukio hilo ni la kushangaza kwasababu wamekuta marehemu hao katika mazingira ya ya kujiuliza maswali mengi kwa kuwa mwanaume alikuwa amefungwa kamba mikononi jambo lonaloleta utata kuelewa nini kilikuwa kinaendelea.

Bwana Chamia amesema marehemu hao walikuwa mwanaume na mwanamke wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka kata ya 30 na 35 lakini kinachoshangaza wameungua wao pamoja na Godoro jambo ambalo linatia wasiwasi majirani waliokuwa eneo hilo.

Naye shuhuda aliyejionea tukio hilo amesema kuwa walilazimika kuvunja mlango kwa kuwa ulikuwa umefungwa kwa ndani lakini dirisha lilikuwa limefunguliwa jambo ambalo hawajaelewa kwasababu marehemu hao mwanaume alikuwa amefungwa kamba.

Shuhuda huyo amesema kuwa Mwanamke huyo anajulikana kwasababu wako naye siku zote lakini mwanaume anaonekana kuwa ni mgeni kwasababu hawajawahi kumuona na mwanamke alikuwa anaishi peke yake.

Naye Diwani wa kata ya Kiranyi Bwan John Seneu amesema kuwa tukio hilo ni la kushangaza kwasababu kama ni nyumba kuungua ingeteketea yote lakini kilichoungua ni godoro peke yake kitu kinachoendelea kuwafanya wananchi kuwa na maswali mengi.

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa makini Na matukio kama haya na kutambua wageni wanaowatembeleakatika maeneo yao

Pamoja na hayo jeshi la polisi linaendelea na upelelezi ili kubaini chanzi cha tukio hilo la kusikitisha.
d1856a31425093e81dc5686c434a7389.jpg
 
: Breaking News

Watu wawili , mwanume na mwanamke wanadaiwa wamekutwa wamekufa kwa kuchomwa na moto mitaa ya Whiterose, Sakina Arusha.

Mtoa taarifa anasema ni wamefungwa mikono na miguu wote wawili na kuchomwa juu ya Godoro, nyumba haijapata madhara makubwa.

Taarifa zaidi zitafuata...!
: Ni ya kutisha ila inasikitisha aisee,,,,,inasemekana binti kapangishiwa chumba na jamaa,,,jamaa kamfumania na jibaba,,,,jamaa akampiga kamba jibaba akawafungia kisha akapiga kibiriti,,,,,So sad aisee
 
12102b8f63be15ca2d43b1ac38f0b913.jpg
Watu wawili wanaodhaniwa ni wapenzi, wameuawa kwa kuchomwa moto baada ya kufungwa kamba wakiwa kitandani, katika tukio lililotokea eneo la Whiterose lililoko kata ya Kiranyi wilayani Arumeru mkoani Arusha.


Mamia ya watu wamejitokeza kuzunguka nyumba lilipotokea tukio hilo baada ya kuona moshi ukitoka katika moja ya chumba na kuonekana miili ikiwa imeteketea kwa moto.



Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo amesema tuki hilo limetoke jana, Jumanne saa 3.00 asubuhi


Amesema aliyekutwa amefariki ni Maurine Urio (32) pamoja na rafiki yake huyo ambaye hajaweza kutambulika kutokana na kuungua sana.


“Tumepata taarifa asubuhi hii kuwa kuna nyumba inaungua na polisi pamoja na zimamoto walifika eneo la tukio na kukuta watu hao wameshapoteza maisha wakiwa juu ya godoro ambako mwanaume alionekana kabla ya kuchomwa alifungwa kamba miguu na mikono ili kuzibitiwa,”amesema.


Mkumbo amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa Mount Meru huku wahusika wa tukio hilo wakiwa wanatafutwa.


Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa mtaa wa Ilkiurei iliyoko kata ya Kiranyi, Onesphory Chami amedai kuwa tukio hilo linahusishwa na wivu wa mapenzi.
 
12102b8f63be15ca2d43b1ac38f0b913.jpg
Watu wawili wanaodhaniwa ni wapenzi, wameuawa kwa kuchomwa moto baada ya kufungwa kamba wakiwa kitandani, katika tukio lililotokea eneo la Whiterose lililoko kata ya Kiranyi wilayani Arumeru mkoani Arusha.


Mamia ya watu wamejitokeza kuzunguka nyumba lilipotokea tukio hilo baada ya kuona moshi ukitoka katika moja ya chumba na kuonekana miili ikiwa imeteketea kwa moto.



Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo amesema tuki hilo limetoke jana, Jumanne saa 3.00 asubuhi


Amesema aliyekutwa amefariki ni Maurine Urio (32) pamoja na rafiki yake huyo ambaye hajaweza kutambulika kutokana na kuungua sana.


“Tumepata taarifa asubuhi hii kuwa kuna nyumba inaungua na polisi pamoja na zimamoto walifika eneo la tukio na kukuta watu hao wameshapoteza maisha wakiwa juu ya godoro ambako mwanaume alionekana kabla ya kuchomwa alifungwa kamba miguu na mikono ili kuzibitiwa,”amesema.


Mkumbo amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa Mount Meru huku wahusika wa tukio hilo wakiwa wanatafutwa.


Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa mtaa wa Ilkiurei iliyoko kata ya Kiranyi, Onesphory Chami amedai kuwa tukio hilo linahusishwa na wivu wa mapenzi.
e1d75e3cd6140950f33a8c3b2c8f9508.jpg
 
aiseee inasikitisha sana.RIP ndugu zetu mlokufa kifo cha mateso makali na pia MWENYE MUNGU AWAREHEMU.Ameeen!
 
Pesa makaratasi hasara roho.....sasa unaua mtu unaishia kufungwa unaenda kuolewa jela huko unacha wanawake wengine wazuri zaidi ya huyo aliekutoa utu.
Hakuna kesi hapo wewe... uliza utaambiwa.. ugomvi wa mapenzi hakuna kifungo cha maisha na hivyo aliwafumania ndio kabisaaaa...
 
Bosi, Ngolilo,
Bosi, Ngolilo.
Ivi ukimfumania mkeo ndo umuue ndugu.
Na wewe ukifumaniwa uuawe au mwenzetu hujawahi kufanya mapenzi na msichana asiyekuwa mkeo ?
Kosa la kufumania linauma kweli lakini halilingani na adhabu ya kumwua mfumaniwa.
Mwanamke ni binadamu huwa anaweza kushawishiwa na kujikuta akichepuka, kama wewe unavyoshawishiwa na wadada wa kisasa.
Pia huyo msichana hakuwa mke wake wa ndoa maana alipanga chumba na kuishi kibachela
Unajua katika mapenzi usimwamini mwenza wako saana hadi ukadhani unapendwa wewe pekee.
Kumbuka hata wewe hukuwa wa kwanza kuwa mpezi wake, hata kama ulikuwa wa kwanza, ujue kama wewe unavyowapenda wanawake wa mtaani naye pia kuna wanaume wanao mvutia zaidi yako.
Zaidi wewe huna haki ya kutoa uhai wa mtu yoyote kwani huyo si mali yako na mmekutana ukubwani tu.
Kama umemfumania unaweza kumsamehe au kumwacha, kwani dunia bado inamuhitaji ujue.
Usiwe unapenda saaana kiasi ukifumania unashindwa kuiendesha akili yako, yaani unageuka kichaa.
Penda kidogokidogo ndugu, kwani ktk mapenzi kuna kuchokana, kuogopana, kushwawishika nje ya ndoa nk.
Huyu aliyeuwa lazima alaumiwe, siyo binadamu ana kichaa cha mapenzi.
Vijana mjifuze kuhimili kukataliwa, kufumania, kuachwa nk. Kwani hamna hati miliki ya mapenzi kwa wadada mlionao.
Ona, wazazi na ndugu wamlee msichana,
wamtunze,wamsomeshe, unajua ghalama walizotumia halafu unakuja kumwua kirahisi tu.
Yaani hizi hela ulizomhonga kwani ulilazimishwa uumpe mpaka uwe na uchungu kuliko ndugu na wazazi wake walio mghalimia katika maisha yake hadi unamwona mzuri.
Jifunze kuhimili mapenzi, kuua kwa kufumaniwa ni ulimbukeni mbaya.
Ujue hakuna msichana anaye kupenda wewe tu, wewe ni kwamba umejitokeza kumshawishi na anakukubalia kwani anahitaji mtu wa kumliwaza au wa kuishi naye tu.
Kuna watu anawapenda kuliko wewe.

Bosi, Ngolilo
Unaongea hivyo kwakuwa hayajakukuta kijana... lkn yakikukuta either ujiue ww au uwaue wao.. always hakuna anayependa kuua mwenzake bt mazingira na kikubwa hapo ni udhalilishwaji wa huyo anayehumia... hujui hayo subiri yakukute afu uje hapa na utueleze.. mm nimeshudui mtu anajiua kwa hali kama hiyo... so huyo akili imemtuma aue tu..
 
Wakuu naomba namimi nichangie hii thread kama hivi.

Mi nadhani kama mlango ulifungwa kwa ndani japo hatukuambiwa kwanba unakufuli,kitasa au komeo.
Mwanaume amefungwa kamba.
Dirisha liko wazi.
Hawakupiga kelele.
Ukisoma hiyo picha ya tukio vzr inaonyesha huyo mwanaume kabla ya kufungwa kama aidha alileweshwa kwa dawa kali,pombe binafsi sikubali kwamba aliuwawa kabla ya tukio nadhani alileweshwa kabla ya kuuwawa maana inahaja gani ya kumfunga kamba marehemu?
Afu mtuhumiwa wa mauaji nadhani ni huyo dada mwenyewe,kwanini yeye hakufungwa kamba pia kwenye picha unaona kwamba alifurukuta kidogo kwa maana kwamba alikua na fahamu wakati wa kuungua.
Yawezekana pengine walikua na visa vyao vya kimapenzi na bi dada akaona akihitimishe kisa hicho kwa njia hiyo.
Habari ya kumuhusisha marehemu bilionea Msuya sioni kama ina uzito ni bahati mbaya tu kwamba tukio limetokea katika moja ya nyumba zake.
Hayo ni maoni yangu mimi kama mimi baada ya kuzisoma picha za tukio na maelezo yake.
R.i.p them .
 
Back
Top Bottom