Arusha wamvua nguo MIzengo Pinda!!

Arusha wamvua nguo MIzengo Pinda!!

reandle

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Posts
11,166
Reaction score
8,152
Kama kuna kipindi nilipata kumdharau na kumchukia kupita kiasi Mheshimiwa Pinda ni pale alipoingilia maamuzi ya John Pombe Magufuri kuhusu suala zima la mizani! Wafanyabiashara wa malori wakacheza na akili ya Watanzania na Watanzania nao bila kujitambua wakawa upande wao na kuona alichofanya Magufuri sio sahihi! Watu wa malori wakafikia hadi kusema eti Tanzania ndiyo nchi pekee inayoruhusu uzito mdogo wakati ukweli ni kwamba Tanzania ndio miongoni mwa nchi zinazoruhusu uzito mkubwa zaidi wa Tani 56. Kenya labda wabadilishe sasa, wao ilikuwa maximum load ni 48 tonnes…..na ikiwa inazidi upande mmoja tu; unakula bonge la faini! Wafabiashara wa Tanzania wakawahadaa Watanzania kiasi cha kutuonesha as if suala la mzigo ku-move na kuegemea kwenye axle moja ni suala la Tanzania peke yake! Upumbavu mwingine ambao Wafanyabiashara waliwadanganya Watanzania na sisi kama mazuzu tukawaunga mkono ni suala la ubovu wa mizani!

Mungu hamfichi mnafiki. Kwa mujibu wa ITV saa 2 usiku huu; Wakala wa Vipimo Arusha ilifanya ukaguzi wa kushitukiza! Magari kibao yamejaza kupita kiasi. Aidha kuna gari limezidisha 30 tonnes, na baada ya kuona kimeo dereva ameingia mitini. Lakini madereva wengine kama kawaida yao; eti mizani mbovu! Upumbavu mtupu.

Habari hii ni aibu kwa Pinda, tena ni aibu iliyopitiliza aibu ambayo anapaswa kuwa nayo PM. Magufuri hakukosea hata chembe kuondoa nafuu ya 5% ambayo kimsingi ilikuwa ni favor na wafanyabiashara wakaibadilisha na kuiona ni right yao. Kwa upande mwingine, Magufuri sasa wakati umefika ukafahamu tafsiri sahihi ya kujihudhuru! Ikiwa mara kwa mara maamuzi unayofanya huwa yanatenguliwa na wakubwa wako; tafsiri yake ni kwamba wana mashaka na uwezo wako wa maamuzi….wanakuona unamudu sana kazi ya u-foreman kuliko kufanya maamuzi. Hiyo peke yake ni sababu tosha kabisa kukufanya kujihudhuru si kwa sababu umeshindwa kazi au umefanya makosa bali umeshindwa kufanya kazi na wakubwa wako ambao hawaamini katika maamuzi yako!
 
Hili si swala la Magufuri wala la Pinda, hilo ni suala la wananchi wenyewe wajiuzuru. Kama wananchi wangeliona hoja ya magufuri kuwa na mantiki basi wangelim-support, kinyume chake walianza kumshutumu mh. pombe, ndipo Pinda akatumia huo mwanya kuamua barabara zetu ziendelee kupigwa tu.
 
:A S 2152::A S 2152::help:who is Pinda in this world? Acha tu barabara zife wajukuu wa mkulima ni watoto wa Waziri mkulu kwa sasa .... nani anajali zikiharibika hizo barabara na wakulima kushindwa kusafirisha mazao yao!!
 
Hili si swala la Magufuri wala la Pinda, hilo ni suala la wananchi wenyewe wajiuzuru. Kama wananchi wangeliona hoja ya magufuri kuwa na mantiki basi wangelim-support, kinyume chake walianza kumshutumu mh. pombe, ndipo Pinda akatumia huo mwanya kuamua barabara zetu ziendelee kupigwa tu.
SIO siri, kama kuna jambo ambalo lilini-disappoint kweli kweli ni vile Magufuri alivyokuwa anashambuliwa kila kona na wananchi! Lakini hata hivyo, siwalaumu sana coz' wafanyabiashara wa malori walicheza sana na media, hususani Power Breakfast ya Clouds; waka-manipulate watu na bila kujijua raia tukaingia kichwa kichwa kuwaunga mkono bila kufahamu kwamba tunachezewa akili! Niseme wazi kwamba, huwa namkubali sana GERALD HANDO wa CLouds lakini katika sakata hili nae alitumika vilivyo, ama kwa kujua au kutojua! Huyu Gerald alinikera sana kwenye vipindi vyake!!

Msema hovyo Kibonde ndie pekee aliyekuwa amegundua ghiriba hii ya wafanyabiashara; lakini kwa bahati mbaya nae alishambuliwa kwenye kipindi chake hadi akafunga mdomo na siku zilizofuata ikawa ni nafasi ya POWER BREAKFAST peke yake kueneza propaganda za wafanyabiashara!
 
wananchi wengi hutazamishwa na vyombo vya habari vyenye waandishi wa kusujudia bahasha za kaki. kwenye luninga unakutana na host kilaza au mnafiki au vyote viwili, anaruhusu gest kuendesha mjadala. utazamishaji huwa ndio silaha ya upotoshaji. ukichanganya na elimu yetu ya uraia ni ndogo ndo basi tena
 
Nadhukuru mmejua upu..mb..a..vuu wenu upo wapi na ubadilishe heading sioni pinda kosa liko wapi
 
watu melogwa na maghufuli? kwa hiyo hata maamuzi ya kuvunja nyumba za watu kwa kisingizio cha kufuata sheria nazo zilikuwa ghiliba za wafanyibiashara?
 
Mkuu NasDaz umeandika ukweli mtupu lakini nataka nikuhakikishie jambo moja tu kwamba weigh bridges zetu zina matatizo makubwa sana. Niliwahi kupata fursa ya kuwa karibu na hao jamaa wa Tanroads kwahiyo ninafahamu matatizo ya mizani zao,Zina variations kubwa sana Kati ya mzani mmoja na mwingine ukipima mzigo huo huo.

KUna siku ilitokea transporter mmoja aligoma kulipa faini mzani wa Kibaha na akawaambia Yuko tayari kujaza gari mafuta aondoke na mtu wa Tanroads Kibaha warudi na gari waipime upya katika mizani zote kuanzia Kibaha,Chalinze,Msata na Himo.
Jamaa wakakubali na zoezi likaanzia Kibaha,baada ya hapo wakaenda Chalinze wakapata vipimo tofauti na walivyopata Kibaha,Kisha wakaenda Msata napo wakapata vipimo tofauti na walivyopata Kibaha na Chalinze ( Gross Vehicle Mass-GVM),na zoezi la kurudia vipimo likaishia hapo Msata.

Kwa uzoefu wangu na mizani za Tanroads Kuna variations kubwa sana baina ya mzani mmoja na mwingine. Kwahiyo provision ya 5% ilikuwa ni fair kabisa kwa wafamyabiashara kwakuwa hata kiutaalamu unapotengeneza machine au mtambo lazima unaweka hiyo provision either plus or minus.
 
Last edited by a moderator:
Pinda amenusuru loss kiuchumi. Magufuli hakuangalia hilo, yeye katoa maamuzi kirobot robot bila kuangalia pande zote, kisha atoe uamuzi ambao ni balanced ili mambo yaendelee. Unavyoropoka eti mkapaki malori yenu upenuni kwenu hakujua anazungumzia loss kwenye sekta ya uchukuzi asilimia ngapi? Au alifikiri ni vilori viwili vitatu? je Mgufuli alikuwa waziri wa barabara miaka mingapi? Mbona hakuliona hilo ? Na hata baada ya kutoliona haoni ingekuwa busara kukaa nao na kuondoa mapungufu hayo? Hiyo asimilia 5 sio issue. Issue ni hilo lilioonekana Arusha. Huko mezani ndio kuna rushwa kubwa pengine kuliko sehemu nyingine zote nchini maana ni kila siku na kila mizani jamaa wanapokea mlungula ili uzito usioruhusiwa upite. Magufuli ni robot type maana hajui kama waendesha mizani ni janga.
 
SIO siri, kama kuna jambo ambalo lilini-disappoint kweli kweli ni vile Magufuri alivyokuwa anashambuliwa kila kona na wananchi! Lakini hata hivyo, siwalaumu sana coz' wafanyabiashara wa malori walicheza sana na media, hususani Power Breakfast ya Clouds; waka-manipulate watu na bila kujijua raia tukaingia kichwa kichwa kuwaunga mkono bila kufahamu kwamba tunachezewa akili! Niseme wazi kwamba, huwa namkubali sana GERALD HANDO wa CLouds lakini katika sakata hili nae alitumika vilivyo, ama kwa kujua au kutojua! Huyu Gerald alinikera sana kwenye vipindi vyake!!

Msema hovyo Kibonde ndie pekee aliyekuwa amegundua ghiriba hii ya wafanyabiashara; lakini kwa bahati mbaya nae alishambuliwa kwenye kipindi chake hadi akafunga mdomo na siku zilizofuata ikawa ni nafasi ya POWER BREAKFAST peke yake kueneza propaganda za wafanyabiashara!

Ndugu yangu nakubaliana na wewe Kimsingi .Lakini jambo la kujiuliza ni Kwanini ASerikali haitaki kuboresha miundombinu ya RELI ilikuondokana na karaha hii....Hii mitandao ya Barabara zinazojengwa kwa mkopo ni mzigo mkubwa sana kwa wananchi wa tanzania.Pia udhibiti wake ni Mgumu. Mawaziri hawa kwa makusudi wanashiriki kuuwa usafiri wa RELI ambo kimataifa ndiyo usafiri unaotarajiwa kuwa more economic. Tungewekeza kwenye Reli kasheshe zote hizi zisingekuwepo.

Kwa makusudi hata hizi reli mbili (TAZARA na RELI YA KATI) zilizopo zinahujumiwa (YA TANGA ARUSHA NDO HIVYO TENA) nI KWA NINI wafanyakazi wa vitengo vy mizigo hulazimika kuchaji Bei kubwa kusafirisha mzigo kuliko Bei inayochajiwa kwa Gari kwa mzigo wa Uzito husika. Shida kubwa kwa hapa Tanzania ni namna tunavyopanga mipango ya maendeleo utafikiri wote tutakufa kesho...mipango yetu yote ni ya CHEKECHEA TU... Hakunaanayeangali maslhi mapana ya Taifa.
 
CLOUDS wapigwe tu, tumechoka.
 
watu melogwa na maghufuli? kwa hiyo hata maamuzi ya kuvunja nyumba za watu kwa kisingizio cha kufuata sheria nazo zilikuwa ghiliba za wafanyibiashara?
Inawezekana wewe ni muathirika katika hilo, so I can understand it! Lakini kama sheria inasema nyumba inatakiwa kujengwa kutoka umbali fulani na mtu akaenda kinyume chake basi ni sahihi kubomolewa! Kama itaonekana si sahihi basi njia muafaka ni kubadilisha sheria husika na sio kumlaumu anayesimamia sheria. Watanzania tumezoea kutotii sheria!
 
Ndugu yangu nakubaliana na wewe Kimsingi .Lakini jambo la kujiuliza ni Kwanini ASerikali haitaki kuboresha miundombinu ya RELI ilikuondokana na karaha hii....Hii mitandao ya Barabara zinazojengwa kwa mkopo ni mzigo mkubwa sana kwa wananchi wa tanzania.Pia udhibiti wake ni Mgumu. Mawaziri hawa kwa makusudi wanashiriki kuuwa usafiri wa RELI ambo kimataifa ndiyo usafiri unaotarajiwa kuwa more economic. Tungewekeza kwenye Reli kasheshe zote hizi zisingekuwepo.

Kwa makusudi hata hizi reli mbili (TAZARA na RELI YA KATI) zilizopo zinahujumiwa (YA TANGA ARUSHA NDO HIVYO TENA) nI KWA NINI wafanyakazi wa vitengo vy mizigo hulazimika kuchaji Bei kubwa kusafirisha mzigo kuliko Bei inayochajiwa kwa Gari kwa mzigo wa Uzito husika. Shida kubwa kwa hapa Tanzania ni namna tunavyopanga mipango ya maendeleo utafikiri wote tutakufa kesho...mipango yetu yote ni ya CHEKECHEA TU... Hakunaanayeangali maslhi mapana ya Taifa.

Baadhi ya big fish ndo wamiliki wa magari ya mizigo, na uwepo wa reli bora utawapunguzia ulaji.
Kuna jamaa kwenye daladala nilimsikia akisema ujenzi wa barabara kilomita 1 gharama yake ni sawa na ya utengenezaji wa reli kilometa 6 (wataalamu wanisaidie). reli zingeungania mikoa inayozalisha mazao ya chakula na biashara na mikoa mingine, mfumko wa bei za vyakula ungepungua kwani mizengwe na gharama za usafirishaji vingepungua.
 
Mkuu NasDaz umeandika ukweli mtupu lakini nataka nikuhakikishie jambo moja tu kwamba weigh bridges zetu zina matatizo makubwa sana. Niliwahi kupata fursa ya kuwa karibu na hao jamaa wa Tanroads kwahiyo ninafahamu matatizo ya mizani zao,Zina variations kubwa sana Kati ya mzani mmoja na mwingine ukipima mzigo huo huo.

KUna siku ilitokea transporter mmoja aligoma kulipa faini mzani wa Kibaha na akawaambia Yuko tayari kujaza gari mafuta aondoke na mtu wa Tanroads Kibaha warudi na gari waipime upya katika mizani zote kuanzia Kibaha,Chalinze,Msata na Himo.
Jamaa wakakubali na zoezi likaanzia Kibaha,baada ya hapo wakaenda Chalinze wakapata vipimo tofauti na walivyopata Kibaha,Kisha wakaenda Msata napo wakapata vipimo tofauti na walivyopata Kibaha na Chalinze ( Gross Vehicle Mass-GVM),na zoezi la kurudia vipimo likaishia hapo Msata.

Kwa uzoefu wangu na mizani za Tanroads Kuna variations kubwa sana baina ya mzani mmoja na mwingine. Kwahiyo provision ya 5% ilikuwa ni fair kabisa kwa wafamyabiashara kwakuwa hata kiutaalamu unapotengeneza machine au mtambo lazima unaweka hiyo provision either plus or minus.

Mungu wangu! hawakuwekeana dau au makubaliano kwa atakashindwa katika hilo? "taifa linajengwa na wenye moyo linaliwa na wenye meno" Anonymous
 
Back
Top Bottom