Arusha: Wafanyabiashara maduka madogo wawekewa makufuli kwenye biashara zao

more88

JF-Expert Member
Apr 9, 2016
447
412
Kama kichwa kinavyojieleza, leo hii katika kata ya Sakina Arusha tumeona wafanya biashara wadogo wenye mitaji ambayo wengi wao ni kuanzia laki 5 hadi milion 2 wakifungiwa biashara zao na maafisa waliojitambulisha kuwa wanatokea Manispaa ya Arusha

Kuna baadhi walipewa vitambulisho vipya vya wajasiriamali vile vya elfu 20 lakini cha ajabu maafisa hao wamevikataa na kuwataka wakakate leseni ya biashara. nakumbuka Rais Magufuli amekuwa akisisitiza vitambulisho vitagawiwa kwa wafanya biashara ambao mitaji yao ni chini ya MILION 4 (NNE) sasa kwa nn hawa maafisa wa manispaa wanapingana na kauli ya RAIS

Kwa sasa hata sisi wafanyakazi tunaona hali ilivyo mbaya kibiashara huku mtaani, kwa nini wasingesubiri hata hili janga la korona lipite maana limeathiri biashara nyingi sana na kufa kwa mitaji? Badala yake wanakuja kufunga viduka vidogo huku mitaani hadi watu leo tumekosa huduma, maana hata dawa tumeshindwa kununua

Ombi langu ni kwamba tunaomba maafisa biashara wazingatie maelekezo aliyotoa rais kuhusu wajasiriamali wadogo pasipo kuwaonea na kuwawekea makufuli katika biashara zao, na je ni sahihi kumfungia mtu biashara bila kumpa elimu na muda wa kwenda kulipa?

Kuna harufu ya rushwa katika hili zoezi tunaomba mamlaka husika ziingilie kati kuzuia wananchi kuonewa.
 
Hakuna kupoteza nguvu wakati wa maombi Chief.....

Unaonekana kana kwamba umekataa tamaa na maisha....!!!

Haya yote ni Mapito tu,lazima tuyapitie

Tatizo linakuja kwenu
Mnataka kila siku barabara iwe imenyooka,bila ya kuwa na miinuko au matuta au ubovu wa barabara

Chief
Maisha hayako hivyo
Yafunge maisha yako na kuridhika juu ya hali uliyokuwa nayo sasa,huku ukitafuta ufumbuzi sahihi
Na usipende mara nyingi kutumia ulimi wako katika kutatua matatizo yako,jifunze kutenda zaidi kuliko kusema

Mola Ibariki Dunia
Mola Ibariki Afrika
Mola Ibariki Tanzania
Mola Mbariki Rais wetu
Mola Wabariki Watanzania wote
utapoteza nguvu bure mkuu
 
HUKO TABATA NIMEZISIKIA WAMEKUJA NA KODI ZUIO AIISEE KAZI MNAYO MWAKAHUU
UKIPANGISHA AKIKISHA UNAMWONGEZEA. MTU KALE KA TEN PERCENT CHAKE ILI AKIKULIPA UNAMWONDOLEA UNAMWAMBIE KALIPIE TRA... SOWAKIJAKUKIMBIZANA NAE UMEJITTA
 
Back
Top Bottom