KERO Arusha tumekuwa tunakatiwa maji pasipo utaratibu na mamlaka za maji

KERO Arusha tumekuwa tunakatiwa maji pasipo utaratibu na mamlaka za maji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

tamuuuuu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2014
Posts
22,189
Reaction score
29,748
Ndugu waziri wa maji Juma Aweso pole kwa majukumu. Kwa masikitiko makubwa baadhi ya wananchi huku Arusha tumekuwa tunakatiwa maji pasipo utaratibu na mamlaka za maji.Ukataji umekuwa ni wa kibabe na hakuna makubaliano wala maridhiano.Watu wa maji wanafungua mageti ya watu bila taarifa kwa wahusika na wanakata maji wakati tayari malipo ya Ankara tena nusu yameshalipwa kutokana na deni lililokuwepo
Watendaji wamekuwa ni watu wa lugha chafu,dharau na jeuri.Ukienda ofisini hawakusikilizi wapo bisy na simu zao.Sasa tunajiuliza maswali yafuatayo;
1.Je wanapata wapi mamlaka ya kufungua mageti ya watu bila wenyeji kuwepo?
2.Ikiwa mtu ameanza kulipa maji tena nusu,inakuwaje tena anakatiwa maji?
3.Sera ya serikali ni kuwapatia maji watanzania,Je huku ndiyo kuwapatia huduma ya maji watanzania?

RAI:
Mheshimiwa Rais kasema maji ni UTU, mheshimiwa waziri na katibu mkuu wa wizara fuatilieni hili na toeni mwongozo kwa watendaji wenu wa mamlaka za maji dhidi ya huu unyanyasaji wanaofanya kwa wananchi.Kwani huu utaratibu si sawa.

Serikali ina lengo la kutoa huduma za kijamii kwa watanzania ikiwa ni pamoja na maji na kuweka unafuu.
Zuieni huu ukandamizaji,kwani Mheshimiwa Rais amekuwa anasisitiza maji ni huduma na ni UTU.Ondoa hawa watendaji wanyanyasaji.Chini ni gari inayozunguka na hao waruka ukuta na wafungua mageti ya watu kisa kukata maji wakati maji ni HUDUMA.
Ninawajibika kwa serikali yangu lakini haya ni manyanyaso na ukandamizaji. Wachukuliwe hatua hawa.
Ikufikie Mheshimiwa Juma Aweso.View attachment 3281691
 
Attachments

  • Screenshot 2025-03-24 145413.png
    Screenshot 2025-03-24 145413.png
    497.4 KB · Views: 15
Ndugu waziri wa maji Juma Aweso pole kwa majukumu. Kwa masikitiko makubwa baadhi ya wananchi huku Arusha tumekuwa tunakatiwa maji pasipo utaratibu na mamlaka za maji.Ukataji umekuwa ni wa kibabe na hakuna makubaliano wala maridhiano.Watu wa maji wanafungua mageti ya watu bila taarifa kwa wahusika na wanakata maji wakati tayari malipo ya Ankara tena nusu yameshalipwa kutokana na deni lililokuwepo.Sasa tunajiuliza maswali yafuatayo;
1.Je wanapata wapi mamlaka ya kufungua mageti ya watu bila wenyeji kuwepo?
2.Ikiwa mtu ameanza kulipa maji tena nusu,inakuwaje tena anakatiwa maji?
3.Sera ya serikali ni kuwapatia maji watanzania,Je huku ndiyo kuwapatia huduma ya maji watanzania?

RAI:
Mheshimiwa Rais kasema maji ni UTU, mheshimiwa waziri na katibu mkuu wa wizara fuatilieni hili na toeni mwongozo kwa watendaji wenu wa mamlaka za maji dhidi ya huu unyanyasaji wanaofanya kwa wananchi.Kwani huu utaratibu si sawa.

Serikali ina lengo la kutoa huduma za kijamii kwa watanzania ikiwa ni pamoja na maji na kuweka unafuu.
Zuieni huu ukandamizaji,kwani Mheshimiwa Rais amekuwa anasisitiza maji ni huduma na ni UTU.Ondoa hawa watendaji wanyanyasaji.Chini ni gari inayozunguka na hao waruka ukuta na wafungua mageti ya watu kisa kukata maji wakati maji ni HUDUMA.
Ikufikie Mheshimiwa Juma Aweso.View attachment 3281691
Duuh Noma!
 
Back
Top Bottom