Arusha Stadium kufurika 30/5/2015, Ni mkutano wa hadhara wa Lowassa

Status
Not open for further replies.
Manaake hadi Ilala imeitwa Mkoa ilhali ni Wilaya. Tutaheshimiana tu!

Mkuu, ilala kuitwa wilaya au mkoa inategemea unaiongelea katika muktadha gani, ki polisi inaitwa ni mkoa, tmk na kinondoni yote ni mikoa ndio maana ina ma RPC'S vile vile hata kwa Tanesco hiyo ni mikoa ndio maana ina ma mameneja wa mikoa, ki utawala ndio wilaya.
 
Radio zitafanya kazi kubwa. Huku kwetu hata wakikata haituumizi sana zaidi heshima inarudi mtaani mafuta yatatumika
 
Mkoani Kagera ukiwa na wilaya 8 TANESCO wameata umeme tangu juzi jumatano na kwamba utarejeshwa jumatatu au jumapili.Tutaheshimiana tu

Mkoa wa Kagera unapata umeme wake kutoka UGANDA.

Je, una maana hata Yoweri Museveni ameanza kumshughulikia Edward Lowassa?
 
Mkuu, ilala kuitwa wilaya au mkoa inategemea unaiongelea katika muktadha gani, ki polisi inaitwa ni mkoa, tmk na kinondoni yote ni mikoa ndio maana ina ma RPC'S vile vile hata kwa Tanesco hiyo ni mikoa ndio maana ina ma mameneja wa mikoa, ki utawala ndio wilaya.

Basi mngesemaga 'mkoa wa kitanesko wa ilala' kama mnavyosemaga 'mkoa wa kipolisi wa ilala' fikiri vizuri! Tutaheshimiana nasema
 
Radio zitafanya kazi kubwa. Huku kwetu hata wakikata haituumizi sana zaidi heshima inarudi mtaani mafuta yatatumika

Simpo tu, tutawasha kamtambo ketu pale tisiaraei tuvuruge mawasiliano kwa baadhi ya maeneo! Tutaheshimiana tu
 
Haaaa haaa nasikia wanafunzi wa chuo cha ualimu Patandi wamekataza kuhudhuria sherehe hizo na jumamosi wamepangiwa kufanya mtihani kuanzia saa 8 mchana hadi 12 jioni tutaheshimiana tu.

Pengine hiki chuo kinaweza kutoa maprofesa wenye uwezo wa kuhoji bila KUABUDU pesa za akina lowasa
 
Manaake hadi Ilala imeitwa Mkoa ilhali ni Wilaya. Tutaheshimiana tu!

No.
Baadhi ya taasisi kama Tanesco na TRA wana 'MIKOA' ya kiutendaji, ambayo ni tofauti kabisa na mikoa ya kisiasa tu nayoifahamu. Tanesco wana 'Mikoa' kadhaa ya kiutendaji hapa Dar kama ilivyo kwa TRA
 
CCM inaelekea kubaya zaidi na zaidi kila kukicha. Hapa Dodoma,Waziri Sophia Simba anahaha kukusanya na kusafirisha makada na wananchi wa kawaida kwenda Arusha. Wasafirishwa wanapewa sh.30000 na watakapofika Arusha malipo mengine yatafanyika.

Kesho,Ndugu Edward Lowassa anatangaza nia ya Urais huko Arusha. Sophia Simba anawasafirisha watu mchana wa leo kwenda Arusha,kutoka hapa Dodoma kwenda kwa Lowassa. Pesa inamwagwa vilivyo.

Hivi ndivyo uungwaji mkono unavyopaswa kuwa? Lowassa anaendelea kujidhihirisha jinsi asivyofaa kwa kutaka kuununua Urais. Fisadi aogopwe kama acid!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kanda ya Kati)
 
Huyu mama si ndo aliyewaagiza wanawake wasilale na wanaume km waume zao wanasapoti upinzani? SORRY KM NIMESAHAU NIMECHANGANYA....


Mwalimu Nyerere alisema 'Hapa hatumchagui mtu maarufu ,tunamchagua mtu safi na huyu si safi ambaye hapo alimlenga Lowasa.Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe naye chai.Wengine wanasema aah ni tuhuma tu.

Samueli Sitta]Yusufu Makamba ]mnasisima hapa mnasema ni tuhuma ,tuhuma tu.Lakini mtakumbuka mke wa kaisari alipotuhumiwa kwa ugoni Kaisari akaagiza uchunguzi ufanyike .Uchunguzi ukafanyika ikabainika kwamba sio kweli.Lakini Kaisari bado akamuacha ,akasema mke wa kaisari hapaswi hata kutuhumiwa .

Na sisi hapa mgombea wetu hapaswi hata kutuhumiwa .wakati wapo wengine safi ambao hawana tuhuma.

Kama mkimteua huyo mimi sitapiga kampeni .Siko tayari kumsafisha mtu matope ndio nimuombee kura Hapana kabisa.

Huyu mimi namjua si msafi na nchi nzima inajua siyo msafi.hafai kuwa mgombea wetu'Mwl.Juliasi Nyerere NEC dodoma ,Juni 1995.
Nimeona niandike hayo maneno hapa kwani yana faida kubwa sana kwa watanzania wanaiotakia mema nchi yetu .Nyerere hayupo duniani tena lakini maneno yake na wosia wake utaendelea kudumu daima.

CCM lazima mtambue IKULU SIYO PANGO LA MAFISADI .

CCM lazima mtambue IKULU SIYO WODI YA WAGONJWA.

CCM lazima mtambue Mwalimu Nyerere aliwahi kusema watanzania wanataka mabadiliko wakiyakosa ndani ya ccm watayatafuta nje ya ccm sasa ni wakati muafaka kwa watanzania kutafuta mabadiliko nje ya ccm.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom