ARUSHA: Rufaa ya Onesmo Ole Nangole yatupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Arusha. Mahakama ya Rufaa nchini imetupilia mbali rufaa ya kupinga hukumu ya kesi ya uchaguzi katika jimbo la Longido mkoani Arusha.

Uamuzi huo umesomwa leo (Alhamisi) na msajili wa Mahakama ya Rufaa nchini, Amir Msumi na kusema kwamba wakata rufaa waliwasilisha rufaa mpya badala ya kurekebisha baadhi ya vipengele kama walivyoagizwa na mahakama.

Msumi amesema badala ya kuwajumuisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na msimamizi wa uchaguzi kwenye rufaa hiyo, wakata rufaa walifanya kitu ambacho hawakuruhusiwa kukifanya na mahakama na hivyo rufaa hiyo imetupwa na wanapaswa kulipa gharama za uendeshaji wa kesi hiyo.
 
Hizi ni njama,Mtu kashinda mubashara halafu mnamnyanganya haki kwa kigezo cha mahakama.Mahakama zenyewe ndio hizi zipo mifukoni mwa serekali.Zina puuzwa na kina makonda.
Hata dada yangu bulaya,Hii round ya mwisho watampora ubunge wake na kumzawadia lile babu kibabe."Tushajua"Ila mwisho wa ubaya ni ubaya.Ipo siku.
 
Wassira bado anafurukuta huko Bunda hivyo Nangole naye ana haki ya kuendelea kufurukuta
 
Hizi ni njama,Mtu kashinda mubashara halafu mnamnyanganya haki kwa kigezo cha mahakama.Mahakama zenyewe ndio hizi zipo mifukoni mwa serekali.Zina puuzwa na kina makonda.
Hata dada yangu bulaya,Hii round ya mwisho watampora ubunge wake na kumzawadia lile babu kibabe."Tushajua"Ila mwisho wa ubaya ni ubaya.Ipo siku.

Hawawezi. Wale wanatumwa na Mzee wanachokosea CDM ni kuweka dau kubwa .Huyu Mzee atapinga mpaka 2020
 
Mahakama imetupilia mbali kesi na kuwataka wakata rufani kwenda kurekebisha makosa ambayo yamesababisha rufani yao kutupwa na kuleta upya
 
Back
Top Bottom