Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Rais Samia Suluhu amezindua kiwanda kikubwa nchini cha kuchakata nyama cha Eliya Food Overseas Ltd, kilichopo wilayani Longido Mkoa Arusha chenye thamani ya Sh bilioni17 na kuahidi kumaliza changamoto ya Maji inayokikabili ifikapo desemba 5, mwaka huu .
Akiongea katika uzinduzi huo rais Samia amepongeza uwekezaji huo mkubwa nchini na kusema ni fursa Kwa wafugaji wa Wilaya ya Longido na Mkoa wa Arusha kuuza mifugo yao .
Rais Samia aliahidi kutatua changamoto zingine katika kiwanda hicho ,ikiwemo upatikanaji wa malighafi ya Nyama,Masoko ya Ngozi ,pamoja na kuwapatia elimu wananchi kuacha kuweka alama kwa kuchoma ngozi jambo linalopunguza thamani ya ngozi.
"Tumezichukua changamoto hizo ila suala la maji nataka pindi ifikapo desemba 5 mwaka huu yawe yanapatikana kiwandani hapo kwa uhakika viongozi wa mkoa na wilaya simamieni hilo " alisema
Rais Samia aliongeza kuwa kiwanda hicho kitakuwa kikisafirisha nyama nje ya nchi hivyo hivi sasa soko la mifugo ni la uhakika.
Awali Mkurugenzi wa kiwanda hicho, lrfhan Virjee alisema kiwanda hicho kina uwezo wa kuchakata tani 20 za nyama ya ng'ombe sawa na Ng'ombe 500 kwa siku na tani 20 za nyama ya mbuzi na kondoo,Sawa na mbuzi 4000
"Kwa sasa kiwanda hiki kinafanya kazi kwa asilimia 30 ya uwezo wa kuchinja na kuchakata nyama kwa mifugo ya mbuzi na kondoo na asilimia 10 kwa mifugo ya ng'ombe"alisema
Virjee alimweleza rais kuwa lengo la kiwanda hicho ni kufikia uzalishaji wa asilimia 80 kufikia mwishoni mwa mwaka 2021 na kukuza masoko mapya ya bidhaa zetu
Alisema mpaka sasa kiwanda kimeshatoa ajira 150 za moja kwa moja kwa Watanzania wakiwemo madaktari watatu wa wanyama kutoka serikalini wanaofanya kazi za ukaguzi wa afya na ubora wa mifugo hapo kiwandani.
Awali Waziri wa Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema kiwanda hicho ndio kikubwa kwa sasa hapa nchini kati ya viwanda 10 vilivyopo nchini.
Virjee alieleza baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na kuiomba serikali kusaidia upatikanaji wa ng'ombe wa bei nafuu kwa kuruhusiwa kununua mifugo kutoka moja kwa moja kwa wafugaji na hivyo kusaidia kuingia kwenye soko la ndani kwa bei nafuu.
Alisema kwa sasa wanauza Nyama katika masoko ya nchi za uarabuni ,Oman,Qatar,Kuweit,Bahrain ,Falme Za kiarabu(UAE) na Kenya.
Hata hivyo alimwomba Rais Samia kuharakisha mazungumzo na nchi ya China ili kufikia makubaliano ya ubora wa Nyama .
Aidha Virjee alimweleza Rais Samia Uwekezaji wa kiwanda Cha Maziwa Cha Kilimanjaro Dairy Milk LTD ,kilichopo Unga limited jijini Arusha ,ambapo alimwonyesha aina mbalimbali za maziwa wanazozalisha ambapo Rais Samia alifurahia bidhaa hizo muhimu Kwa jamii.
Kwa upande wake waziri wa viwanda Profesa Kitila Mkumbo alisema kiwanda hicho kwa Sasa ni kati ya viwanda vikubwa 618 vya kusindika Nyama hapa nchini na kwamba kiwanda hicho ni cha kwanza kwa ukubwa kati ya viwanda 10 vya kusindika Nyama nchini.
Ends.....