Arusha: Polisi wasema Nabii Abraham Peter alinyofolewa viungo vya sehemu za siri baada ya kuuawa

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,207
4,703
Taarifa imetolewa kwa mujibu wa Gazeti la Nipashe

Inamuhusu Nabii Abraham Peter almaarufu Katapila wa Jijini Arusha

Taarifa rasmi ya uchunguzi wa polisi inaeleza kuwa baada ya kuuawa viungo vyake nyeti vilinyofolewa.

----

Nabii huyo baada ya kuuawa Oktoba 14 mwaka huu, mwili wake ulitelekezwa na watu wasiojulikana, ukiwekwa lango la kuingilia Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru).

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Jastine Masejo, alisema nabii huyo alikwenda Arusha kwa ajili ya kutoa huduma ya maombi, akitokea jijini Dar es Salaam.

“Mpaka sasa tumeshawahoji watu wanne ambao ni wachungaji waliokuwa naye kabla ya umauti kumkuta. Huyu Nabii Abraham aliwasili Arusha Oktoba 12, mwaka huu,” alisema.

Kwa mujibu wa jeshi hilo, Nabii Katapila ni mkazi wa Dar es Salaam na kiongozi wa kiroho aliyekwenda mkoani Arusha kutoa huduma.

Kamanda Masejo alisema kuwa nabii huyo na wachungaji hao awali walifanya maombi katika Mlima Duluti uliopo Wilaya ya Arumeru, Oktoba 14, mwaka huu na walirejea mjini Arusha na kupata mlo katika maeneo yaliyopo karibu na mlima huo.

Alisema kuwa baada ya kula, kila mmoja aliondoka na usafiri wake na kwamba Nabii Abraham alipokodi usafiri wa pikipiki kwenda kwa mchungaji mwenyeji wake alikokuwa amefikia jijini Arusha. Hata hivyo Kamanda Masejo hakutaja jina la mchungaji huyo.

"Baadaye usiku, mwili wake ulikutwa kwenye lango la Hospitali ya Mount Meru, ukiwa na majeraha yaliyosababishwa na kitu chenye ncha kali.

“Kifo chake ni cha utata kwa sababu haijajulikani kwa nini alitelekezwa kwenye mlango wa hospitali, huku mwili wake ukiwa na majeraha," alisema Kamanda Masejo.

Kutokana na utata huo, Kamanda Masejo alisema bado wanafanya uchunguzi kubaini kama ni mauaji ya kupangwa au ajali.

Kamanda huyo alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kifo cha Nabii Abraham kilisababishwa na kuvuja damu nyingi.

Mwili wa Nabii Abraham umeshafanyiwa uchunguzi wa kitabibu na ndugu wa marehemu wameruhusiwa kuusafirisha kwenda Kitunda, Pwani.

Nipashe ilizungumza na rafiki wa nabii huyo anayejulikana kwa jina la Master King Prophet John, ambaye alidai kifo cha Nabii Katapila kina utata.

Alisema marehemu alikuwa mmisionari ambaye hana kanisa na alikuwa akitoa huduma za kinabii katika kanisa lolote au kokote anakoitwa.

"Tumejiuliza kwamba ni vita vya watumishi hao waliomwita kwenye maombi au ni vibaka waliodhani ana mali au ni ajali tu ya barabarani?" Alisema.

Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom