LiverpoolFC
JF-Expert Member
- Apr 12, 2011
- 11,348
- 3,219
Taarifa ni kwamba nassari atafunguliwa kesi ya uhaini kwa kauli yake kuwa yeye ni rais wa jamhuri ya Meru na kwamba atamzuia kikwete kuingia arusha iwapo serikali itaendelea na mpango wake wa kuwahamisha wamachinga katika mji wa arusha. babanga atafunguliwa mashitaka ya kumdhalilisha mkuu wa nchi baba ritz
Ni mimi kachero mkuu wa polisi!
Duh! -- Ile nyomi ya msimamo pale NMC iliwafanya mabwana zao kuweweseka kwani chama cha magamba wafute kabisa wazo la kukusanyisha umati kama ule -- popote pale hapa Tanzania!
Au Tusema yule dogo Nchimbi kaanza na gia kubwa? Atakwama tu asipoangalia!
Hili ndiyo bado cjajua kama wanalitambua kweli!Jamani hivi polisi wanajua kuwa wanalipwa kwa pesa za watanzania wote sio ccm? je Chadema ikija shinda wataingia wapi?
Mkutano ulikua na shida gani?
Mkutano ulikua na shida gani?
kuu tunategemea utatujuza zaidi nini kinaendelea huko maana hawa magamba hawana dogo mbona hawakuwaita wale vijana wa ccm walioandamana kule dar ? polisi kwa kukosa kazi bana
Wakati mwingine watawala wetu wanatakiwa wawe na ngozi ngumu. Wako too sensitive. Joshua Nassari alisema ikifika Jumatatu (kama sikosei) bila ya watu waliomuua mwenyekiti wa CHADEMA USA River kukamatwa basi rais Kikwete hatokanyaga Arusha. Lakini nadhani hili atakuwa amepitiwa maana Nassari hana uwezo wa kufanya hivyo. Hata hivyo mbona hawa polisi hawakumiita Tendwa wakati aliposema washiiri (wazee wa Kimeru) wamekataa Lema asikanyage Meru?
Kwa upande wa Heche nadhani itakuwa kauli yake kwamba baadhi ya mawaziri kwenye hii reshuffle ya juzi ni marafiki zake Ridhwani.
tatizo ni matumizi ya lugha kwa wanasiasa wa tz... hadi kuendelea katika nyanja ya siasa vyama vinahitaji kusimamisha viongozi makini wenye tija kwa taifa
Polisi wa Tanzania ni wavivu wa kufikiria, ukiona hivyo basi wamesukumwa na baba riz1. Polisi wetu ni sawa na mbwa asiye na meno, Kwanini wasiwaite Mawaziri majambazi wanaoiba mali za umma?