Arusha: Nassari, Heche na Bananga wahojiwa na polisi

Taarifa ni kwamba nassari atafunguliwa kesi ya uhaini kwa kauli yake kuwa yeye ni rais wa jamhuri ya Meru na kwamba atamzuia kikwete kuingia arusha iwapo serikali itaendelea na mpango wake wa kuwahamisha wamachinga katika mji wa arusha. babanga atafunguliwa mashitaka ya kumdhalilisha mkuu wa nchi baba ritz
Ni mimi kachero mkuu wa polisi!



Polisiccm wanajidanganya sana ktk Nchi hii.
Hebu ngoja siku itafika tu na wewe unayejiita kachero wa police na utajuta kuwa na wasifa huo na ukawepo hapa JF!
Yani hakunaga Duniani Nguvu ya Umma iliyowahi kudai haki na kushindwa.

Mi nahisi siku si nyingi tutajuaga tunaelekea wapi ktk Nchi hii ya Asali na Maziwa inayofaidisha watu wawili watatu ktk wa 42M.
 
Hizo kauli ukitoa ndani ya nchi yoyote lazima dola na vyombo vyake ikutazame vizuri,hii inaonesha jaji hakukosea hukumu ya Lema.
 
Duh! -- Ile nyomi ya msimamo pale NMC iliwafanya mabwana zao kuweweseka kwani chama cha magamba wafute kabisa wazo la kukusanyisha umati kama ule -- popote pale hapa Tanzania!

Au Tusema yule dogo Nchimbi kaanza na gia kubwa? Atakwama tu asipoangalia!

Nadhani huyu bado hajaanza vitu vyake kwani bado hajaapishwa. Lakini umenikumbusha kitu kimoja kwamba Watanzania tutegemee utendaji mbovu kabisa katika Wizara ya ndani kuhusu jamaa huyu kushika wizara nyeti kama hiyo. Naingiwa hofu kabisa na uwezo wake wa kimaamuzi.

Habari nilizozipata ni kwamba kama siku kumi hivi zilizopita alikwenda New habari ku-officiate draw ya shindano lao la promotion la Mchongo tukio ambalo lilizusha utata mkubwa kutokana na yeye kutokuwa makini katika masuala haya ya ku-officiate functions.

Nchimbi angekuwa makini angeuliza kwanza iwapo kulikuwapo ofisa kutoka Gaming Board kusimamia draw ile, maana kuwepo kwake ni lazima kisheria. Hakuwapo mtu wa Gaming Board na hivyo draw ilifanyika kienyeji na kuzua utata mkubwa kwani kuna watu wawili (badala ya mmoja) walikuja kudai zawadi ya gari (toyota Vitz).

Inasemekana kwamba Nchimbi baada ya kuokota kuponi ya kwanza mshindi alipigiwa simu, ambapo namba haikujibiwa. Waendesha draw (new Habari) wakamuomba Nchimbi aokote kuponi nyingine na huyo akapigiwa simu, ikajibiwa na kuambiwa kuwa ni mshindi.

kumbe yule wa kwanza alikuwa ni kiziwi, na alikuwa ameandika kwenye kuponi yake kwamba mawasiliano yote naye yawe katika SMS. Siku ya pili wote wawili wakaja kudai zawadi, huyo kiziwi alikuja na kikundi cha wapambe wake wakiwemo sign readers.

Yote haya yasingetokea iwapo Ofisa wa Gaming Board angekuwapo, na Waziri Nchimbi hakuona lazima ya kuuliza kwanza iwapo afisa huyo alikuwapo. Angeambiwa hakuwapo asinge-officiate hiyo draw kinyume cha sheria.

Huyo ndiyo Waziri wetu wa Ndani ambaye kateuliwa na JK.


Kaazi kweli kweli.
 
Jamani hivi polisi wanajua kuwa wanalipwa kwa pesa za watanzania wote sio ccm? je Chadema ikija shinda wataingia wapi?
 
Ngd Ally Bananga, Mbunge wa Arumeru, Mh Joshua Nassari na Mwenyekiti wa BAVICHA Ndg John Heche waitwa polisi kwa mahojiano kufuatia Mkutano wa CHADEMA jana viwanja vya NMC Arusha.

Source: sunrise radio arusha
 
Mkutano uliadhimia kitu gani au kulikuwa na tatizo gani ndugu lililopelekea wao kuitwa katika mahojiano!?
 
kuu tunategemea utatujuza zaidi nini kinaendelea huko maana hawa magamba hawana dogo mbona hawakuwaita wale vijana wa ccm walioandamana kule dar ? polisi kwa kukosa kazi bana
 
kuu tunategemea utatujuza zaidi nini kinaendelea huko maana hawa magamba hawana dogo mbona hawakuwaita wale vijana wa ccm walioandamana kule dar ? polisi kwa kukosa kazi bana

Kwa upande wa Nassari aliwataka wamachinga kuendelea na biashara zao bila kuogopa vitisho vya halmashauri kuwataka Jumatatu waondoke mitaani.

Nassari alisema Atatoa Amri ya kumzuia J.K Kukatiza Arusha kwani yeye Ni Raisi wa Arusha Na Lema ni Waziri Mkuu.
 
Wakati mwingine watawala wetu wanatakiwa wawe na ngozi ngumu. Wako too sensitive. Joshua Nassari alisema ikifika Jumatatu (kama sikosei) bila ya watu waliomuua mwenyekiti wa CHADEMA USA River kukamatwa basi rais Kikwete hatokanyaga Arusha. Lakini nadhani hili atakuwa amepitiwa maana Nassari hana uwezo wa kufanya hivyo. Hata hivyo mbona hawa polisi hawakumiita Tendwa wakati aliposema washiiri (wazee wa Kimeru) wamekataa Lema asikanyage Meru?

Kwa upande wa Heche nadhani itakuwa kauli yake kwamba baadhi ya mawaziri kwenye hii reshuffle ya juzi ni marafiki zake Ridhwani.
 
Wakati mwingine watawala wetu wanatakiwa wawe na ngozi ngumu. Wako too sensitive. Joshua Nassari alisema ikifika Jumatatu (kama sikosei) bila ya watu waliomuua mwenyekiti wa CHADEMA USA River kukamatwa basi rais Kikwete hatokanyaga Arusha. Lakini nadhani hili atakuwa amepitiwa maana Nassari hana uwezo wa kufanya hivyo. Hata hivyo mbona hawa polisi hawakumiita Tendwa wakati aliposema washiiri (wazee wa Kimeru) wamekataa Lema asikanyage Meru?

Kwa upande wa Heche nadhani itakuwa kauli yake kwamba baadhi ya mawaziri kwenye hii reshuffle ya juzi ni marafiki zake Ridhwani.

Hata mi nadhani hatokanyaga Arusha kutokana na aibu...
 
Polisi wa Tanzania ni wavivu wa kufikiria, ukiona hivyo basi wamesukumwa na baba riz1. Polisi wetu ni sawa na mbwa asiye na meno, Kwanini wasiwaite Mawaziri majambazi wanaoiba mali za umma?
 
hii inasikitisha lakini nadhani ukombozi unakaribia...polisi wa ccm waendelee tu na moto huu tuone utawafikisha wapi...!
 
Polisi! polisi! polisi! Mshahara mnalipwa shilling elfu 80 kwa mwezi na bado mnawaendekeza wezi ccm.
 
busara inahitajika sana, polisi wapo sahihi kuwahoji kwani kauli ya nasari imevuka mipaka yake kama mbunge, nadhani anahitaji kuwekwa chini nakuelezwa Rais ni nani na mamlaka yake yakoje na pia mipaka ya mbunge ni yapi. Kijana huyu asilewe na kura za wana Arumeru Mashariki, atambue waliompigia walitaka mabadiliko kumpta atakayedai mahitaji yao na siyo kumtukana rais.
Nashauri Chadema wawape vijana wao mafunzo ya ndani kuhusu uzalendo na pia hiyo italeta maana ya magwanda wanayovaa kwamba ni walinda amani na siyo wavuruga amani.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom