Arusha na CCM

Arusha na CCM

Jamani tutambue zama hizi si za kuchagua chama!! Ni kuchaguavkiongozi atayetuvusha kulingana na hali ya uchumi wetu.

Ni ajabu kusikia "CHAMA KWANZA WANANCHI BAADAE" Hiyo ni dhana ya kutaka uongozi tu na si maendeleo ya wapiga kura aka wananchi
 
Naomba kudeclare interest. Mimi siamini kuwa tutapata rais bora toka CCM hata wakimteua nani. Ila naona kitendo cha kumtema Lowassa na wakifanikiwa kumtema Membe, wapinzani tutakuwa na kazi kweli kweli. Watakaobaki wachache ndani ya CCM watakuwa wamoja na wakichanganya na nguvu ya dola na watendaji wakuu wa ngazi zote serikalini CCM watapata ushindi mkubwa kwa kutumia kura na bao la mkono.

Lowasa hatathubutu kuhama chama maana atapelekewa bill ya kodi ya michango yoote aliyopokea kutoka kwa marafiki zake (Kumbuka waliopata hela ya escrow walidaiwa kodi). Pili, Mawaziri wakuu wanaotakiwa kupata marupurupu ya kustaafu ni wale waliostaafu na sii waliojiuzulu. Lowasa alijiuzulu na si alistaafu. Kama atathubutu kuingia chama kingine haya marupurupu yatakatwa.

Sababu nyingine ni kuwa Watanzania ni wepesi kusahau. Baada ya wiki moja utasikia wale wale waliokuwa kindaki ndaki team lowasa watakuwa kindaki ndaki wa mgombea atakayeteuliwa na jina Lowasa litakuwa limefutika midomoni mwao.

Kwa maamuzi haya ya CCM utashangaa upinzani tusipokuwa makini tutapoteza hata baadhi ya majimbo tulonayo.

Imefikiri sana mkuu, ni kweli swadakta kabisa ulivyosema
 
Back
Top Bottom