Arusha: Mwandishi wa habari atekwa ateswa kisha kupigwa picha za uchi

Kwa maana nyengine unaona kitendo alichofanyiwa huyu mwandishi wa habari unaona ni haki. Kweli mtu mweusi amelaaniwa hawa wazungu hawakoseagi kuita hizi nchi shithole
Usifanye mawazo yako yawe yangu, tafadhali. Kwanza sikukujibu wewe, pili wakati tukio hilo bado liko katika upelelezi, wengi wetu humu tumekwisha toa hukumu. Du!!
 
Dah so sad, jirani yangu huyu baada ya kusoma taarifa hii nimeenda kwake amerudi lakini kajifungia dah unyama huu ukomeshwe
 
Issue iko Polisi na watuhumiwa wamekamatwa. wamekamatwa mapema hivi!!?, isije ikawa mpango mkakati wa kualalisha waanga wote wa matukio haya na yanayofanana haya huko nyuma, wakawaaminisha watz kuwa watu wasiojulikana ndio wamepatikana wakati hawa ni panya road tu,
Polisi wakipatiwa taarifa na wasamaria wema inayojitosheleza wako sharp sana. Ona walivyowakamata wahusika ndani ya masaa 24 baada ya tukio! Na mhusika (mwandishi wa habari) bila shaka atakuwa amethibitisha hao waliokamatwa ndiyo waliomteka. Of course watakuwa walikodiwa na mnene mmoja ambaye atakuwa alikwazwa na huyo mwandishi wa habari. So upelelezi unaendelea kumbaini huyo mnene! Inawezekana akawa wa chama cha siasa fulani.
 

Mwandishi wa habari wa kujitegemea jijini Arusha, Lucas Muyovera amenusurika kuuawa kwa kipigo baada ya kutekwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumatatu Mei 14,2018.

Mwanahabari huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Mkoa Mount Meru akipatiwa matibabu inaelezwa hali yake ni mbaya baada ya watu hao wapatao watano kumteka Jana majira ya saa tatu usiku katika eneo la Ngulelo jijini Arusha.

Kwa mujibu wa Mwandishi huyo watu walimpakia kwenye gari yao na baadaye kumpeleka katika mto ambao hajaufahamu na kuanza kumshambulia wakiwa wamemvua nguo zote na kumdhalilisha.

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha Claude Gwandu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

"Ni kweli Mwandishi mwenzetu,Lucas Myovela wa kituo cha Sunrise cha jijini hapa jana usiku alitekwa,akapigwa sana,akapigwa picha za video akiwa uchi na kisha akalazimishwa kutoa password ya simu yake wakampora pesa, Issue iko Polisi na watuhumiwa wamekamatwa,bado tunafuatilia kwa karibu",amesema Gwandu.

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limethibitisha tukio hilo likidai bado wanafanya uchunguzi.
Hawajamlawiti kweli!!..... Maana huko kumvua nguo ndyo sijaelewa
 
Cha maaana uhai,marinda kama katatuliwa itakuwa siri yake,familia yake itabaki na furaha kwa kusalimika mpendwa wao
Mkuu kwa wanaume wa Dar kutolewa "kizibo" ni jambo la kawaida ila kwa mwanaume wa bara ni kosa kubwa sana !
 
pole sana ndugu mwandishi..hv mungu wa dar na kundi lake hawahusiki kweli???????? maana wamekuwa kama al qaeda au IS wa TZ
 
Back
Top Bottom