ARUSHA: Msichana akutwa gesti amefariki

ARUSHA: Msichana akutwa gesti amefariki

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,637
Arusha. Amina Jamali (18) amekutwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni ya Lightness iliyopo jijini Arusha.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Salumu Hamduni ameieleza Mwananchi Digital leo Jumamosi Desemba 5, 2020 kuwa taarifa za awali ni kuwa msichana huyo amekufa kifo cha kawaida.

Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kaloleni Magharibi, Hassan Sharifu amesema baada ya kupata taarifa za kifo hicho alifika eneo la tukio na kubainisha kuwa watu wa karibu wa msichana huyo walikuwa wakimtafuta bila mafanikio.

Amesema walipoona kimya kwa kuwa walimwona akiingia kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni walikwenda kumtafuta na walipogonga mlango haukufunguliwa lakini walipoufungua na kuingia ndani walimkuta amefariki dunia huku akiwa akitokwa damu puani.




©@Mwananchi
 
Mh! Yaani umeona MTU kaingia gesti. Unaendamtafuta kwingine kwanza,ukikata tamaa ndio unarudi gest.

NB: Usione watu wanafeki majina wakiingia gesti,umejaribu kastaili ulikokasikia kwa masela,mtoto wa watu chalii.

Unarara mbere
 
Mwanaume aliyewasiliana nae mara ya mwisho jumba bovu litamuangukia
Hapo ukute ulikua unamsalimia tuu, halafu chatting za nyuma ukawa unaomba mkutane.

Kuua,
Kubaka,
Pengine Mwanafunzi,
Pengine hajatimiza hio 18 bado,
Mara kinyume na maumbile,

Bado na malupu lupo ya hakimu..

Hapo, kila ukifumba na kufumbua macho Usoni unaona dawa ya panya, Kamba na kwa mbaaali ibirisi akikoka moto...
Maturubai na Mikeka lazime ihusike.

Asalaaalee,
 
Kuna nyimbo flani za misiba huwa sizipendi, nikizisikiliza tu ghafla nasinyaa nakuwa volkano tuli. Nakosa pozi.
"Kamanda" ya Daz Nundaz na "Kifo" ya Remi Ongala.

Ukiwa mzima enjoy sana life, piga starehe! Maana ka-life haka ni kafupi kama mkia wa mbuzi halafu katamu kweli. The future is now kula maisha!
 
Kwani kuna ubaya gani? Shida sio kufia guest tatizo unafia hapo ukiwa na mpango gani, kwa mfano ww umesafir katika mji ambao huna ndugu ukaamua kuchukua guest ili usiku upite ila kwa bahati mbaya ukafia humo! Hapo kutakuwa na ubaya???
Huyo Ni mwenyeji wa hivyo viunga ndio maana alitafutwa na nduguze mitaani walipoona hawajampata wakaelekezwa na mtu aliye muona akiwa anaingia guest ...so hakuwa mgeni kama jinsi ambavyo wewe unavyotaka ieleweke
 
Back
Top Bottom