Arusha Moto, Makruta walikiona cha mtema kuni

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,224
Hawa makruta kutoka CCP walienda matejo, wakashika machalii kibao na gongo. siku ya kwanza walifanikiwa.

Siku nyingine wakaenda, hiyo ilikuwa wiki iliyopita. Kumbe watu walikuwa wamejipanga, wakajikusanya watu 15. Wale mapolisi walipokuja, wakawekwa chini ya ulinzi, wakaambiwa vua mabuti na mjifunge mashati, wakateremshwa mtoni wakatelekezwa hawana viatu.

Ndo Defender za FFU zikatumwa na hawajaona mtu.

Arusha ni Noma.
 
Hao watoto ni wajingawajinga sana. Acha wapate cha mtema kuni. Sijui kwanini ccp wamefanya Arusha kuwa ndio field ya hao makuruta!? Wamejaa mjini, wanakamata watu hovyo. Mtu hana kitambulisho inakuwa tabu wakati ajira hakuna. Wanataka tutembee na kitambulisho cha kura!?

Kukamata gongo ni sawa lakini hao waliopo mjini wamekuwa kero kwa raia! Nadhani hawajui kwamba wanatakiwa kuwalinda raia na sio kuwabugudhi!
 
Hawa makruta hafu wanatembea makundi kama watoto wa primary school...

Wanakera sana bora hata raia wamewapa tamu yao
 
Rais Slaa atakuwa na kazi kubwa ya kufanya reshuffle ya hii taasisi ya ccm 2015!
 
hili ni jambo baya kabisa.... polisi wanatakiwa kifunga kabisa hao vijana waliofanya hivyo
 
Walitakiwa wawavue magwanda wawatandike viboko vya kutosha wawaache na makofuli tu, wangeacha unoko
 
Gongo yenyewe na mirungi wakichukua wanaenda kuuza tena kwa bei chee! Kuna mtu alishaniambia huwezi kuwa na rafiki polisi, lazma akuchome siku japo kwa wenzie! Naamini kwa dhati sasa!
 
Gongo yenyewe na mirungi wakichukua wanaenda kuuza tena kwa bei chee! Kuna mtu alishaniambia huwezi kuwa na rafiki polisi, lazma akuchome siku japo kwa wenzie! Naamini kwa dhati sasa!



Hawafai urafiki, wakiishiwa wanakuchongea kwa wenzao wanakuja wanakushika unawapa hela au wanakunyanganya bidhaa zako na kwenda kuuza cheap mbaya
 
Polisi ni uozo mtupu kuanzia chini mpaka juu...ukienda na case ndio umewapa dili yani hawa majamaa ni sawa na wanyama..
 
Bado waende kwa machalii wa ngalelo..hapo ndo kitaeleweka

Ngalelo ipi hiyo mkuu machalii wa ngaleloo wameji chokea mbaya!sifa ziende kwa wauza gongo na banana woote,angalau siku hizi tunaweza kupokea simu hadharani,enzi za kina marehemu Edii,warbus,spyder ,ama nyokaa. Palikuwa soo. Hawa wa sasa wanaogopa polisi mbaya labda upite umelewa ndo wanafanya sherehe. Ahsante mungu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom