Wito wa mgomo na maandamano ya kupinga Ukiukwaji wa Katiba, haki za Binadamu, ukatili wa police na udhalilishaji wa serikali kwa raia hapa nchini na hasa hapa Arusha. Damu ya mashujaa iliyomwagika kudai Uhuru, haki Uzalendo wa taifa iwe WINO wa kuasisi Taifa jipya.
Jasho la mateso na unyanyasaji liwe ISHARA ya utumwa wa mzawa ktk taifa lake na CHOZI la uchungu wa Umaskini, maradhi, ujinga na ufisadi liwe NISHATI ktk kuwasha taa ya HEKIMA, UJASIRI na NGUVU ya UMMA kuleta mapinduzi ya Kiraia.
KULAANI NA KUPINGA OCD-ARUSHA KUWAITA WANANCHI "PANYA".
Nawasilisha!
Ilikuonyesha kumuunga mkono kamanda Godbless Lema, madereva wa daladala na Toyo kesho wataanza mgomo hapa Arusha....
Nawasilisha
Duh hatari kubwa kwahiyo kesho nitoke na kile kiNoah changu kazi kweli kweli.
Watakao pata hadhaa ya usafiri ni walalahoi wakubwa watapeta na miVX yao kama kawaida nadhani hili zoezi la kuandaa migomo lingeangalia nani mwathirika mkuu.
Hongereni ujumbe umefika.
Mkuu juzi daladala ziligoma watu waliteseka lakini jaama walikomaa mpaka haki ikatendeka...kuna wakati inabidi uteseke ili ufaidi baadae...hata wewe wakati unanunua hicho kinoah chako lazima kwa njia moja ama nyingi uliteseka yaani kuna vitu ulikuwa una vikosa kwa sababu ulikuwa na lengo la kununua Noah lakini leo unafaidi.....Duh hatari kubwa kwahiyo kesho nitoke na kile kiNoah changu kazi kweli kweli.
Watakao pata hadhaa ya usafiri ni walalahoi wakubwa watapeta na miVX yao kama kawaida nadhani hili zoezi la kuandaa migomo lingeangalia nani mwathirika mkuu.
Hongereni ujumbe umefika.
duh....hii imetulia...ngoja nianze safari ya kwenda ofisini leo....