waziri2020
Senior Member
- May 31, 2019
- 190
- 451
Jeshi la Polisi Mkoani hapa linamsaka mfanyakazi wa ndani (jina linahifadhiwa) akituhumiwa kumuua mwajiri wake, Janerose Dewasi (66) Mkazi wa Njiro block D jijini hapa baada ya kukutwa amefariki dunia nyumbani kwake kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali.
Tukio hilo ni mwendelezo wa tukio jingine kama Hilo lilitokea siku chache zilizopita baada ya mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite, Ruth Mmassy (40)kudaiwa kuuawa na mtoto wake mzazi eneo la Njiro jijinibhapa.
Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Justine Masejo alithibitisha kutokea tukio hilo jana na kueleza kuwa wanamsaka mfanyakazi wa ndani ambaye alikuwa anaishi na marehemu huyo na alitoweka baada ya tukio hilo.
Kamanda Masejo alisema mwili wa mwanamke huyo aliyekuwa anaishi na mfanyakazi wa ndani kwenye nyumba yake eneo hilo la block D amekutwa amepigwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso huku akibainisha kuwa Jeshi la Polisi linamsaka mfanyakazi wa ndani ambaye anadaiwa kutoroka muda mfupi kabla ya kugundulika tukio hilo.
"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa anaishi na mtumishi wa kazi za ndani ambaye alianza kazi wiki moja iliyopita ila alitoweka ghafla mara baada ya tukio hilo" alisema
Alifafanua kuwa mfanyakazi huyo alitoweka muda mfupi kabla ya kugundulika tukio hilo.
Kamanda alisema Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wenye nyumba kuwa makini na wafanyakazi wa ndani wanaowapa kazi kwa kujua historia zao.
Mmoja wa majirani wa nyumba hiyo, Tedy Minja alisema mtuhumiwa huyo alikuwa hajulikani sana mtaani kwani alianza kazi muda si mrefu na alikuwa akishinda muda mrefu akiwa ndani bila kutoka.
Kamanda Masejo aliwasihi viongozi wa dini kuendelea kutoa maombi Kwa Jamii ili kujitenga na matendo maovu.
Ends........